Na Theonestina Juma, Ngara
NG’OMBE 30 wenye thamani ya zaidi ya
milioni 22 wameibiwa na watu wasiojulikana huku wengine 16
wakipatikana wakiwa wametelekezwa kati
kati ya porini la Keza Wilayani Ngara .
Kwa mujibu zilizopatikana Mjini Bukoba na kuthibitishwa
na Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera, Philip Kalangi tukio
hilo lilitokea Agosti 5, mwaka huu saa
2: 00 usiku katika tarafa ya Rulenge Wilaya ya Ngara.
Kamanda Kalangi alisema watu wasiojulikana
walivamiwa nyumbani kwa mfugaji Simon Wakataraka (45) mkazi wa kijiji cha
Murusagamba tarafa hiyo na kuwaiba ng’ombe
wapatao 46 ambapo kati yao 30 hawajapatikana hadi hivi sasa huku wengine 16
wakipatikana wakiwa wametelekezwa porini.
Alisema baada ya ng’ombe hao kuibiwa walitoa
taarifa ya wizi polisi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za vijiji
waliweza kutoa taarifa sehemu mbalimbali kuhusu wizi wa
mifugo hiyo ambapo walianza ufuatiliaji na kufanikiwa kuwapata ng’ombe hao
Agosti 9 mwaka huu katika pori la Keza wakiwa wametelekezwa.
Alisema juhudi zinaendelea katika maeneo
mbalimbali za kuwatafuta ng’ombe
wengine na watu waliojihusisha na wizi huo wa mifugo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na
usalama wa wilaya ya Ngara ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo ,Bw.Costantine
Kanyasu alipoulizwa ni namna gani
walivyojipanga katika kukabiliana na wizi wa mifugo ambao umeanza kujitokeza
katika wilaya hiyo yakiwemo matukio mengine ya uhalifu ambapo alidai kuwa
tayari kamati yake imeshatoa maelekezo kwa Jeshi la polisi kufanya doria ya
mara kwa mara.
Alisema doria zinazohitajika kufanyika ni kwa ajili
ya kuimarisha mawasiliano na nchi zinazo pakana na Ngara
ambazo ni Rwanda na Burundi ili kushirikiana katika kudhibiti
wizi na matukio mengine ya uhalifu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment