Pichani ni Mkuu wa Mkoa Kagera Kanali Fabian Massawe akimtuza fedha msanii, wa mjini Bukoba ajulikaye kama Babu Rweyemamu mara baada ya kumaliza kuwaburudisha waliohudhuria katika unzinduzi huo, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kagera, Bi. Constansia Buhuye.
Na
Theonestina Juma, Bukoba
HOSPITALI ya
Mkoa Kagera imefanikiwa kujenga jengo la daraja la kwanza lililogharamu zaidi
ya sh. milioni 418 kwa lengo la kuboresha huduma za matibabu mkoani hapa.
Hayo
yamebainishwa leo na Mganga Mfawidi wa Hospitali ya Mkoa Kagera, Dkt. Andrew Lugakingira
katika risala yake kwa mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkuu wa Mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe
katika uzinduzi wa jengo hilo mjini hapa.
Dkt.
Lugakingira alisema jengo hilo ambalo lilianza kujengwa katika mwaka wa fedha
2008/2009 kwa awamu mbili limeghramu jumla ya sh. milioni 418, 119,938 ambapo
lilikamilika Februari mwaka jana na kukabidiwa rasmi Machi mwaka huo.
Alisema
lengo la kujenga jengo hilo la daraja la kwanza ni kuwahudumia wagonjwa wa mkoa
na Taifa lengo ni kuboresha huduma na kuongeza mapato ya hospitali hiyo.
Alisema jengo
hilo limegawanyika katika sehemu mbili ambazo alizitaja kuwa ni pamoja na
sehemu ya kuwahudumia wagonjwa wa kulala na wan je.
Kwa majaribio
ya kuanza kutoa huduma katika jengo hilo kwa mwezi mmoja wa Julai mwaka huu jumla ya wagonjwa 132 waliweza
kuhudumia ambapo wagonjwa 29 walilazwa na kati yao wanawake wakiwa ni 12 na
wanaume 17.
Alisema kwa
kipindi hicho waliweza kuingiza jumla ya sh. milioni 5,337,200 taslimu huku
wengine nao wakichangia kupitia huduma ya bima ya afya.
Alisema
kiasi hicho kitachangia bajeti ya hositali hiyo kwa silimia 2.1 kutoka asilimia
9.8 hadi asilimia 11.9.
Aidha kwa
kuaingatia hali ya huduma ya daraja la kwanza ilikifikiwa ikiwa ni madhumuni ya
kuongeza mapato ya hospitali kwa kutoa huduma kwa wenye uwezo wa kulipia huduma
zaidi.
Halikadhalika
alisema kuwepo kwa jengo hilo kutasaidia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba ,
kuboresha huduma inayotolewa kwa wote pamoja na kuwahudumia wagonjwa wa bima ya
afya na taasisi zenye mikataba ya huduma
za afya zinazohitajika.
Hata hivyo
kwa upande wa Mkuu wa Mkoa Kagera ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi
huo, alisema serikali kupitia wizara ya afya na Ustawi wa jamii inaendelea
kuboresha utoaji wa huduma za afya katika ngazi zote za kutolea huduma.
Alisema
lengo la serikali ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya kwa
wakati muafaka.
Mkoa wa Kagera kwa kutumia timu ya uendeshaji wa huduma za
afya, ina jukumu la kuhakikisha kwamba lengo la serikali linafikiwa kwa kiwango
cha juu.
Alisema
majukumu wanazotakiwa kuzisimmaia huduma za afya zinazotolewa na sekta ya umma
na sekta binafsi.
Aidha
alisema jengo hilo lilijengwa si kwa ajili ya viongozi wa mkoa na taifa pekee
bali hata wananchi wengine nao watapata huduma kwani huo ni mradi.
Alisema
kutokana na jengo hilo kugharimu pesa nyingi za serikali ambao ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali
unatakiwa kulindwa na kuenziwa pamoja na samani zilizomo.
Alisema
itakuwa haina maana endapo jengo hilo na samani zake za kisasa zilizomo
vitaachwa bila matunzo na usimazi mzuri hivyo wanatakiwa wakitunze kidumu.
No comments:
Post a Comment