Pichani ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba, Dkt.Anatory Amani akikagua baadhi ya bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali mkoani Kagera katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Kyakailabwa nje kidogo ya Manispaa hiyo.Dkt. Amani alikuwa mgeni rasmi siku ya ufunguzi.
MAONESHO ya NANE NANE 2012 Mkoa wa Kagera yanaendelea Katika uwanja wa Kyakailabwa baada ya kuanza tarehe 01/08/2012 na
kufunguliwa rasmi tarehe 03/08/2012 na Meya wa Manispaa ya Bukoba Mhe. Anathory
Amani aliyetembelea maonesho hayo na kujionea teknolojia mbalimbali za
ujasiliamali na uzalishaji wa kisasa katika sekta ya kilimo.
Wananchi
mnahamasishwa kufika Kyakailabwa na kutembelea mabanda ili kujionea na
kujifunza tekinolojia mbalimbali za uzalishaji wa mazao wenye tija. Wananchi
pia na wafanya kazi mtapata nafasi ya kupata elimu juu ya usindikaji mazao ya kilimo,
ufugaji na uvuvi kutoka kwa wataalam mbalimbali ili wananchi kujikwamua kutoka
katika kilimo kisichokuwa na tija.
Aidha
Meya wa Manispaa ya Bukoba Mhe. Anathory Amani akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kutembelea mabanda mbalimbali katika maonesho hayo aliwasistiza
wakulima kuwatumia wataalam waliopo katika kuboresha kilimo na kuwa walimu wa
wakulima wenzao ili kuinuana kwa kuzalisha kwa wingi.
Pia
Mhe. Amani aliwasihi wananchi kuacha dhana potofu kuwa mbolea za viwandani
zinaharibu ardhi bali aliwashauri kuwa na utaratibu wa kulima sehemu ndogo itakayokuwa
na uzalishaji wenye tija ili kukabiliana na gharama kubwa ya mbolea kuliko
kulima sehemu kubwa isiyokuwa na uzalishaji wenye tija.
Maonesho
ya NANE NANE 2012 Mkoa wa Kagera yameandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo
wadau mbalimbali kama Sekta binafsi, Taasisi mbalimbali za serikali na
zisizokuwa za Serikali, wafanyabiashara ndogo ndogo na wakubwa, wakulima na
wafugaji wanashiriki katika maenesho hayo yenye hamasa kubwa. “Kilimo kwanza, zalisha kisayansi na teknolojia
kukidhi mahitaji ya ongezeko la idadi ya watu.”
Imetolewa
na:
Sylvester
Raphael,
Afisa
Habari Mkoa,
KAGERA.
No comments:
Post a Comment