Tuesday, August 21, 2012

Mahakama Kuu kanda ya Tabora yatengua Ubunge wa Dkt.Kafumu CCM

Pichani ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Igunga Mh. Dk. Dalaly Peter Kafumu  akiwa na Kada wa CCM Dr.John Pombe Magufuli. (Picha na Maktaba)

Hukumu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na Wakazi wa Jimbo la Igunga pamoja na baadhi ya watanzania imetolewa leo na Mahakama Kuu Kanda ya Tabora ambapo imemuengua wadhifa wa Ubunge, mbunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CCM Dk. Dalaly Peter Kafumu. 

Hukumu hiyo imetolewa kufuatia kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa akigombea nafasi hiyo ya Ubunge kupitia chama cha CHADEMA Joseph Kashindye. 

Hukumu hiyo inaendeleza wimbi la chama tawala CCM kupoteza majimbo na kuweka alama katika Demokrasia ya Tanzania huku Wananchi wakijiuliza tunatoka wapi tunakwenda wapi.

Hivi sasa kwa mujibu wa Mahakama hiyo jimbo la Igunga lipo wazi

No comments:

Post a Comment