Utangulizi
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inapenda kutoa taarifa kwa umma, kuhusu tetesi zilizokuwa zimeenea hapa nchini kutoka
kwenye vyombo mbali mbali vya habari
kuhusu
kuwepo kwa mgonjwa wa Ebola,wilayani Karagwe
mkoa wa Kagera.
Mnamo tarehe 3 Agosti 2012, Wizara ya Afya na Ustawi Wa Jamii ilipokea taarifa kutoka kwa mganga mkuu wa wilaya ya Karagwe ya kuwepo kwa mgonjwa aliyekuwa anahisiwa kuwa na dalili za ugonjwa
wa Ebola, katika hospitali ya Wilaya ya Nyakahanga. Aidha,taarifa
hiyo ilibainisha kuwa mgonjwa huyo alikuwa ni
mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka (6|) kutoka katika kijiji cha Nyakatundu wilayani Karagwe. Mgonjwa huyu
alikuwa na dalili za homa kali, kulegea,
kutokwa damu puani, kutapika
damu, na kukojoa
damu.Maelezo kutoka kwa mama mzazi zilieleza kuwa mtoto
huyu alianza kuugua kuanzia tarehe 30
Agosti 2012, ambapo alipatiwa dawa ya Septrin baada ya hospitali
binafsi kuonyesha kuwa ana ugonjwa wa“Typhoid”.
Uchunguzi wa awali katika hospitali ya Nyakahanga ulionyesha kuwa mtoto
huyu alikuwa anasumbuliwa na uambukizo kwenye haja ndogo (Urinary Tract Infection).Vile vile
alifanyiwa uchunguzi wa kimaabara na Vipimo
vya malaria, Hepatitis na Typhoid havikuonyesha kuwepo kwa magonjwa haya.
Hospitali inaendelea kumpatia matibabu mtoto huyu na imewaweka
mgonjwa na mama yake anayemtunza kwenye chumba maalum (Isolatiom room) kwa ajili ya uangalizi zaidi.
Aidha mnamo tarehe
4 Agosti 2012, timu za wataalamu
kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii kwa kushirikiana na timu ya mkoa wa Kagera imeweza
kufika na kumfanyia uchunguzi wa kina pamoja na kuchukua sampuli za damu kwa
ajili ya uchunguzi zaidi katika maabara ya
Taifa ya uchunguzi wa magonjwa na Maabara za nje ya nchi, ili kubaini kama
ameathirika na ugonjwa wa Ebola.
Timu hiyo ya wataalamu imetoa taarifa kuwa
hali ya
mgonjwa huyu kwa
sasa imeimarika ikiwa pamoja na kutokuwa
na homa, kutapika na kukojoa damu kumekoma pia, uchunguzi uliofanywa kwa mama wa mtoto
umeonyesha kuwa hana dalili zozote za ugonjwa wa Ebola.Vile vile hakuna
taarifa ya mtu mwingine yeyote kwenye familia hiyo au kwenye
maeneo ya kijiji hicho au cha jirani kuwa na dalili za ugonjwa huo.
Kufuatia taarifa hii, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na
Mkoa wa Kagera imechukua hatua zifuatazo;
Imepeleka timu ya wataalamu mbali mbali kutoka Wizarani na mkoa kwa
lengo la kwenda kufuatilia
na kutoa taarifa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa
huo.
Imetoa
elimu ya Afya kuhusu njia za
kuzuia kuenea ugonjwa wa Ebola pamoja na dalili za ugonjwa huu, kwa wananchi
na watumishi wa afya katika hospitali ya Nyakahanga
Kupeleka vifaa kinga katika hospitali ya
Nyakahanga pamoja na
maeneo ya mipakani
Kutoa matangazo kwa jamii kwa kutumia
vipaaza sauti na kupitia
radioni (Radio Karagwe) kuhusu ugonjwa huu. Aidha, vipeperushi pia vimetolewa.
Hitimisho
Wizara inapenda kuufahamisha umma kuwa mpaka sasa
hakuna
mgonjwa yeyote
aliyethibitishwa kuwa na ugonjwa wa Ebola hapa nchini.Aidha, Wizara ya Afya imejiaanda kikamilifu
kukabiliana na ugonjwa huu iwapo utatokea hapa nchini.
Kwa sasa
timu za wataalum
zipo katika mikoa ya Mara, Mwanza, Kagera,
Kigoma, Kilimanjaro na Arusha, kutoa elimu juu
ya ugonjwa huu kwa wataalamu na kwa wananchi na vilevile kufuatilia ugonjwa huu sehemu za
mipakani.
Wizara inaendelea
kutoa wito kwa wananchi kutoa taarifa
haraka kwenye kituo chochote cha kutolea
huduma za afya, mara wanapoona dalili za
ugonjwa huu.
Imetolewa na:
kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii
Tarehe 6 Agosti, 2012
No comments:
Post a Comment