Na Mwandishi Wetu
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mizengo
Pinda amechomoza kwenye zoezi la upigaji kura kuchagua mgeni rasmi
katika tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20 hapa Tanzania.
Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya
tamasha hilo, Abihudi Mang’era sambamba na Waziri Mkuu, wengine
wanaofuatia katika zoezi hilo ni Mkurugenzi wa kampuni za IPP, Dk
Reginald Mengi na Askofu Mkuu wa Taasisi ya WAPO Mission International,
Sylvester Gamanywa, mchungaji wa kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat
Gwajima, Mchungaji wa kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee
wa Upako’ pia wanamfuatia Waziri Mkuu katika zoezi la upigaji kura
linaloendelea.
Mang’era anaendelea kuwakumbusha watanzania namna ya kuwapigia
kura waimbaji, mgeni rasmi na mikoa ambako ukitaka kumpigia mwimbaji
andika pasaka acha nafsi kisha andika jina la mwimbaji unatuma kwenda
namba 15327.
Pia kwa mgeni rasmi andika neno pasaka acha nafasi kisha andika
jina la mgeni rasmi unayetaka kumpigia kura tuma kwenda 15327, wakati
mikoa unaandika pasaka acha nafasi jina la mkoa unaotaka kuupigia kura
tuma kwenda namba 15327 piga kura uwezavyo ili upate mwimbaji na mgeni
rasmi na mkoa unaopenda ili tamasha lifanyike.
Aidha Mang’era mbali ya viongozi hao wa dini na serikali, pia
waimbaji Jescar BM na Bahati Bukuku ni mojawapo ya waimbaji
wanaoonekana kuelekea kupata nafasi ya kushiriki katika tamasha hilo kwa
kuwa na kura nyingi.
Mang’era alisema mikoa ambayo inaongoza kupigiwa kura nyingi ni
pamoja na Mwanza, Mbeya, Kigoma na Dar es Salaam inapigiwa kura nyingi
kwa ajili ya kufanyika kwa tamasha hilo.
Makamu Mwenyekiti huyo alisema kampuni ya Msama Promotions ambao
ni waandaaji wa tamasha hilo wanazingatia na kutekeleza yale ambayo
yanayotakiwa na wadau ambao wanachagua wanachopenda.
No comments:
Post a Comment