Thursday, March 13, 2014

Mambo yalivyokuwa Dodoma leo kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge maalum la Katiba

Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakimsindikiza Mjumbe wa Bunge Hilo na Mgombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan(Aliyenyanyua fomu)kurudisha fomu kwa Katibu wa Bunge Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akitoa maelekezo kwa wapambe wa mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba kabla ya kupokea Fomu hizo Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu akizipitia Fomu kabla ya Kuzikabidhi kwa Katibu wa Bunge tayari kwa uchaguzi utakaofanyika joini ya leo Mjini Dodoma.
Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila akisaini fomu za mgombea Nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba na Mgombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Bi. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi fomu Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Thomas Kashilila (Kulia) Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
Kina Mama wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiimba kwa furaha baada ya fomu za Mgombea wa Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Samia Suluhu Hassan Mapema Leo asubuhi Mjini Dodoma.
(PICHA NA HASSAN SILAYO- MAELEZO, DODOMA)

No comments:

Post a Comment