Kusamehewa si sababu ya kundelea kufanya makosa
Kusamehewa
hakukufanyi wewe uendelee na makosa ati sababu unajua kuwa utasamehewa.
Unapoomba msamaha maanisha unachokisema na dhamiria kutoka moyoni
kutokurudia tena kosa na epukana na mazingira yaliyokufanya ukatenda
kosa hilo. Kuna watu kwa makusudi wanafanya makosa na kuyarudia wakijua
kuwa wenzi wao watawasamehe sababu ni wepesi kusamehe. Unakuta mtu
anafanya uzinzi, anasamehewa, anaendelea na wala hajali, au mtu anampiga
mke wake, anasamehewa na anaendelea tena na tena.
Kusamehe hakumaanishi kuwa mtu upo tayari kuhatarisha maisha yako.
Unaweza kumsamehe mtu anayekupiga lakini ukajitenga mbali naye sio
sababu hujamsamehe bali kwa usalama wako watoto kama wapo na yeye pia
maana anaweza kukudhuru akaishia gerezani, mpaka pale atakapoamua kweli
kubadilika. Kusamehe hakumaanishi kuishi katika mateso.
Nawewe uliyesamehewa na kisha ukaendelea na makosa ukijua utasamehewa
kumbuka ghadhabu wa Mungu ipo na hakika usipogeuka na kuiacha njia yako
mbaya hauwezi kuiepuka!
Posted by womanofchrist under
No comments:
Post a Comment