Mwanamke ni lazima ujue kupika. Hakuna kisingizio kuwa nimesoma
boarding tangu std one, mama hajanifundisha kupika, sina muda wa kupika
n.k.
Kupika kwa mwanamke ni heshima, ni sifa na ni wajibu. Kama unaweza
kupata muda wa kuwa facebook basi unaweza kupata muda wa ku google
mapishi mbalimbali na kujifunza. Sio rahisi ukapika kila siku lakini
haifai mwanamke wiki nzima hujapika kabisa nyumbani kwako. Jitahidi kwa
hali yoyote uwe ndio mpishi bora kuliko msichana wako wa kazi, hii
inaleta heshima. Sio siku ukiingia jikoni watu wanatamani umwachie tu
dada apike.
Jifunze mapishi mbalimbali kuanzia breakfast, appertizers, main
course, soup, juices, disserts n.k. na kutoka maeneo mbalimbali yani
Indian, Thai, American, Tanzanian n.k.
Sio kazi ya siku moja lakini
tangu unapoanza kujua kupika anza kijifunza kidogo kidogo, waweza weka
ratiba kila mwezi unajifunza mapishi mapya mawili au moja baada ya mwaka
utakuwa mbali sana. Tumia internet vizuri yaani itakufanya uwe chief
cook hadi watu wa nyumbani kwako watamani uwapikie kila siku.
Anza sasa,
anza leo, anza usingoje kesho. Pia mnaweza kuwa mnajifunza pamoja na
nashost wako wakaribu mara moja kwa mwezi badala ya kupiga tu story
mkazipiga jikoni mkijifunza mapishi. Inasaidia sana kuboresha urafiki na
kuongeza ujuzi.
No comments:
Post a Comment