YER. 17:7-8
“Amebarikiwa mtu yule anayemtegemea BWANA, Ambaye BWANA ni tumaini
lake. Maana atakuwa kama mti uliopandwa kando ya maji, Uenezao mizizi
yake karibu na mto; Hautaona hofu wakati wa hari ujapo, Bali jani lake
litakuwa bichi; Wala hautahangaika mwaka wa uchache wa mvua, Wala
hautaacha kuzaa matunda.”
OMB. 3:24-26
“BWANA ndiye fungu langu, husema nafsi yangu, Kwa hiyo nitamtumaini
yeye. BWANA ni mwema kwa hao wamngojeao, Kwa hiyo nafsi
imtafutayo. Ni vema mtu autarajie wokovu wa BWANA Na kumngojea kwa
utulivu.”
KUM. 31:6
“Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana
BWANA, Mungu wako, yeye ndiye anayekwenda pamoja nawe, hatakupungukia
wala kukuacha.”
ZAB. 28:7-9
“BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami
nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu
nitamshukuru. BWANA ni nguvu za watu wake, Naye ni ngome ya wokovu kwa
masihi wake. Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako, Uwachunge,
uwachukue milele.”
ZAB. 27:14
“Umngoje BWANA, uwe hodari, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.”
ZAB. 55:22
“Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza, Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.”
ISA. 41:10
“usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni
Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa
mkono wa kuume wa haki yangu.”
Mungu wa mbinguni akufariji, kukutunza na kukuhifadhi katika pendo
lake. Usikate tamaa wala kuvunjika moyo, hao waisrael unaowaona leo
hautawaona tena milele, Bwana atakupigania nawe utanyamaza kimya.
No comments:
Post a Comment