Wanawake wamekuwa wakilalamika kuwa wanaume wengi wa ki Africa hawako
romantic yaani hawawezi kufanya mambo ya kuonyesha upendo kwa wake zao
mfano kumfungulia mlango wa gari, kumsogezea kiti akae wakiwa restaurant
au hata nyumbani, kumsaidia mizigo wanapokuwa supermarket, kumnunulia
maua au zawadi ndogo ndogo, kumuandalia kikombe cha chai au glass ya
juice siku anapokuwa down au amechoka na kazi fulani na mengine kama
hayo.
Lakini pia ukiangalia upande wa pili jamii na hasa wanawake wenyewe
tunachangia hali hii, mtu akiona kaka yake anamfanyia mkewe mambo kama
haya basi ataanza maneno ooh kaka ameolewa, ooh kaka hafurukuti kwa
mkewe, mara limbwata n.k. yaani hata watu wakiona mtumishi wa Mungu
anamfanyia mkewe basi wataona yule mama hana heshima kwa mumewe.
Hii
inawafanya wanaume waone kuwa kufanya hivi sio sawa wakati ni mambo
yanayoongeza na kuchochea upendo.
Yaani unaweza kuona wata familia
wakiwa outing ni mama tu anayehangaika na watoto mara bembea mara
kuogelea mara huku mara kule, baba akiwa anahangaika nao mama amekaa na
rafiki zake wanapiga story utasikia Mmh mwanamke huyu hafai…
Jamii lazima ifike mahali itambue kuwa mke ni msaidizi wa mume na sio
mtumwa, mke ni sehemu ya mume, ubavu wake na anastawi mahali penye
upendo wa hali ya juu.
Mume ampende mkewe kama Kristo alivyolipenda
kanisa, upendo wa kujitoa, upendo usio na kipimo, upendo usiotafuta
sababu, upendo usioangalia makosa, upendo wa kumuwazia mema siku zote,
upendo wa kujali na upendo wa kutunza.
Changamoto kwetu sote…!
No comments:
Post a Comment