Mchungaji Ekman akizungumzia uamuzi wake wa kurejea kanisa Katoliki katika mahojiano ©TidningenDagen. |
Kupitia katika tovuti yao mchungaji Ekman amesema kwa muda mrefu yeye na mkewe wamekuwa wakipata changamoto kutoka kwa kikundi cha waamini wa kanisa Katoliki ambao wamekuwa wakifafanua mambo mbalimbali kuhusu kanisa hilo na mambo ambayo wamekuwa hawayapendi bila sababu ya msingi hali ambayo ndiyo imewafanya kuamua kurudi Katoliki.
"Tunalipenda kanisa letu ambalo tumekuwa moja ya waanzilishi tukitumika kwa zaidi ya miaka 30, yawezekana hakuna kitu chochote lakini tumejawa shukrani nyingi kwa muda wote ambao tumekuwa pamoja, lakini kwasasa tumesikia mwito kamili kutoka kwa Bwana kwenda hatua hii mpya" amekaririrwa mchungaji Ekman na kuendelea kwamba na sasa wameitikia mwito na wanaamini kwamba kanisa lao la The Word of Life liko katika mikono salama na kwamba litazidi kuimarika na kuzaa matunda.
Uamuzi wa mchungaji huyo na mkewe umewaacha waumini wao katika njia panda juu ya uamuzi huo. Kwa mujibu wa mchungaji Ekman amesema wanahitaji kujua imani ya kanisa Katoliki vyema kitu ambacho kimewasaidia wao kujua kwamba ni Yesu Kristo ndiyo amewaongoza wao kujiunga na kanisa hilo, nakusema wameona upendo wa ajabu wa Yesu na baraka zilizomo katika maisha ya sakramenti takatifu. Ekman amesema wameona sababu ya kuwa na msingi mzuri wa kitumishi ambao ndio unaofanya kanisa hilo kuwepo kizazi hadi kizazi.
Mchungaji Ekman ni mwanzilishi wa kanisa lake The Word of life ministry toka mwaka 1983 maeneo ya Uppsala nchini Sweden na amekuwa mchungaji katika kanisa hilo kwa zaidi ya miaka 30 huku tovuti yake ikielezwa kulitangaza vyema kanisa lake na kufanya kanisa kubwa katika nchi za Scandnavia huku huduma yake ikienea kimataifa katika mataifa ya ulaya mashariki, mataifa ya kisoviet zamani pamoja na Asia huku mafundisho yake yakipatikana katika vitabu zaidi ya 60 ambavyo vimetafsiriwa katika lugha mbalimbali.
No comments:
Post a Comment