CHAMA
cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA) kimelibariki Tamasha la
Pasaka na kutoa wito kwa mashabiki mbalimbali wa muziki huo hapa nchini
kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo linalotarajia kuanza Aprili 20
jijini Dar es Salaam.
Chamuita
inatambua mchango wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex
Msama ambaye ni muandaaji wa matamasha ya Pasaka na Krismasi kwa
kutambua mchango wake wa kufanikisha matamasha hayo, kwenye tamasha
litakalofanyika jijini Dar es Salaam watamkabidhi cheti cha kutambua
mchango wake, Msama.
Akizungumza
na mwandishi wa makala hii, Mwenyekiti wa Chamuita, Addo Novemba
anasema Msama ni mmoja wa mifabo ya kuigwa kwa jamii kutokana na
kufanikisha maendeleo ya muziki huo hapa nchini hasa kuwanyanyua
waimbaji chipukizi.
Novemba
anasema kwenye tamasha la mwaka huu watashiriki kikamilifu kwa sababu
wanatambua anayoyafanya Msama kwa kumtumikia Mungu ipasavyo.
Novemba
anasema utekelezaji wao wa tamasha la mwaka huu watakuwa bega kwa bega
na Msama katika ufanikishaji wa tamasha hilo lenye lengo la kuzungumza
na Mungu kupitia waimbaji na viongozi mbalimbali wa Tanzania na nje.
Aidha
Novemba anatoa wito kwa Watanzania kuipenda nchi yao hasa kupitia kauli
mbiu ya Uzalendo Kwanza, Haki huinua Taifa, hivyo Watanzania wajiandae
kuipenda nchi yao zaidi ya wanavyoipenda.
“Watanzania
Tamasha la Pasaka ni la Msama hivyo ni la kwetu sote, walipende kwa
sababu ni lao kwa kujitokeza kwa wingi kwenye matamasha yanayoandaliwa
naye.”
Novemba
anasema Msama anaepusha mambo mengi yanayomchukiza Mungu kwa kuandaa
matamasha ya kumrudia Mungu kwa kutenda mema ambayo yatampendeza Mungu.
“Msama
anasaidia kuachana na mambo mabaya yanayomchukiza Mungu kama ulevi wa
kupindukia ama kuzungumzia mambo ya umbea na badala yake wajitokeze
kwenye matamasha ya Pasaka na Krismasi,” alisema Novemba.
No comments:
Post a Comment