Mungu aliona si vyema adamu aishi peke yake akaamua kumtafutia
msaidizi wa kufanana naye. Wanawake tumeumbwa kwa kusudi kamili la Mungu
na tunajukumu la kuwa wasaidizi. Nafasi ya mwanamke katika jamii,
familia, ndoa, kanisa na taifa ni kubwa sana.
Angalia jinsi wanawake
wanavyohangaika na watoto, kuanzia wakiwa tumboni hadi wakiwa watu
wazima. Mwanamke ni mjenzi wa familia, mwanamke ni muunganishi wa
familia na mwanamke ni mrutubishaji wa familia.
Moyo wa mwanamke unauwezo mkubwa sana, yani huwa nakaa nafikiria moyo
wa mwanamke nashindwa kuuelewa kabisa, wanawake wanatendwa kila siku
lakini wanasamehe, wanajitahidi kuachilia japo ni ngumu na wanaamua
kuendelea kutenda mema.
Unakuta mama anagundua mumewe anatembea nje, na
hata anafikia kulala nje, mama huyu atalia, ataumia lakini atampikia
chakula, atamfulia, atamuombea ataamua kumsamehe na hata akiletewa mtoto
wa nje anamtunza. Hivi ni wanaume wangapi wanaoweza kuwasamehe wake
zao wanaotembea nje? Na pale anaporudia na kurudia na wakati mwingine
kulala nje???
Mungu awakumbuke wanawake wote.
Mungu asikie kilio chako unacholia ndani ya shuka na bafuni.
Mungu akuonekanie na kukurejeshea furaha ya maisha.
Mungu akutetee wewe ukiyepewa mimba na kuachwa.
Mungu akutunze wewe uliyetelekezwa na mume na ukaachiwa watoto.
Mungu awe mume wa wajane wote.
Mungu ailainishe mioyo ya waume wote, waitambue thamani ya wake
walionao, Mungu awafunike macho yao wasione wengine zaidi ya wake zao.
Mungu alituumba kwa kusudi, tufurahie uanamke wetu na kamwe
tusikubali changamoto za maisha zituondolee furaha. Mungu aliona dunia
haitakuwa njema bila sisi ndio maana akaamua kutuumba, sisi ni wa
thamani saanaaa….
No comments:
Post a Comment