Kwa taarifa zilizopatikana kutoka
kwenye vyombo mbalimbali vya habari, zinasema kuwa msanii aliyekuwa
akiugua kwa muda mrefu, mwigizaji mahiri Bongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’
amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Marehemu
Sajuki alikuwa amelazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya
kuwa amedondoka jiji Arusha mwishoni mwa mwaka uliopita.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amen
No comments:
Post a Comment