Na
Theonestina Juma, Kagera
ZAIDI ya majambazi 10 wakiwa na bunduki takriban
tisa wameteka magari matano likiwemo
lilikodiwa na wanajeshi 10 wa nchini Rwanda waliokuwa wakienda Jijini
Dar Es Salaam kununua magari na wameporwa mamilioni ya fedha pamoja na abiria
wengine wilayani Biharamulo mkoani Kagera.
Kwa mujibu
wa habari zilizopatikana mjini Bukoba, na kuthibitishwa na diwani wa kata ya Rusahunga
Bw.Amon Mizengo na kamanda wa Polisi Mkoani Kagera, Phillip Kalangi tukio hilo
limetokea Januari 24, mwaka huu saa 12.00 asubuhi katika kijiji cha Kikoma
barabara ya Biharamulo -Rusumo katika eneo la mizani ya Nyakahura wilayani
humo.
Jumla ya
fedha walizoporwa abiria hao pamoja na wanajeshi ni milioni 4.2 za Kitanzania,
Dola 175,000, Faranga za Rwanda 85,500 pamoja na simu za mkononi.
Habari hizo
zinadai kuwa magari yaliotekwa yalikuwa yamewabeba wafanyabiara waliokuwa
wakienda katika mnada wa ng’ombe wa Rusahunga wilayani humo.
Aidha gari
lingine ni aina ya hiace lililokuwa limebeba wanajeshi 10 wa nchini Rwanda
waliokuwa wakienda katika bandari la jijini Dar Es Salaam kwa shughuli la
kununua magari kulingana na hati zao sa kusafiria ambapo walikuwa wamevaa kiraia tu.
Hata hivyo
haijajulikana kama walikuwa wakienda Jijini Dar Es Salaama kwa shughuli za
kiserikali ama zao binafsi.
Pia magari mengine ni yale yaliokuwa yakienda nchi jirani ya Rwanda,
huku mengine yakitoka Ngara kwenda Kahama mkoani Shinyanga .
Pia magari mengine ni yale yaliokuwa yakienda nchi jirani ya Rwanda,
huku mengine yakitoka Ngara kwenda Kahama mkoani Shinyanga .
Hata hivyo
magari hayo ambayo namba zao za usajili hazijajulikana,wala wamiliki wao na
idadi ya abiria waliokuwemo, inaelezwa kuwa walipofika eneo hilo majambazi hao
walikuwa wakiwasimamisha kwa kuwanyonyeshea bunduki.
"Hakuna
mawe wala magogo yaliokuwa yamepangwa barabarani,majambazi hao walikuwa
wakiwaonyooshea bunduki tu madereva hao na wao wanasimamisha, hakuna
waliojeruhiwa katika tukio hilo"alisema Bw.Mizengo licha ya habari zaidi
kueleza kuwa majambazi hayo yalikuwa yamepanga mawe na magogo barabarani.
Habari zaidi
zina sema kabla ya kutekeleza azima yao walifyatua risasi kadhaa hewani.
Katika
utekaji huo, majambazi hayo wamewapora abiria mali zao zote waliokuwa nazo na kisha
kutokomea kusiko julikana.Hata hivyo majambazi hao wanasadikiwa kuwa ni wa
kutoka nchi jirani ya Burundi kutokana na lugha ya Kirundi waliokuwa
wakizungumza wakati wa tukio hilo.
Bw. Mizengo alisema
kuwa katika tukio hilo limempata na Askari polisi mmoja wa kituo cha Nyakahura
ambaye jina lake halijapatikana aliyekuwa anaenda Kahama Mkoani
Shinyanga.
N
No comments:
Post a Comment