Na Theonestina
Juma, Kagera
MKAZI mmoja wa wilayani Ngara mkoani Kagera anashikiliwa
na Jeshi la polisi mkoani hapa kwa tuhuma ya kumuua mwanae wa kike mwenye umri
wa mwezi mmoja kwa madai kuwa mkewe amemchosha kumzalia watoto wa kike pekee
.
Mtu huyo
anayedaiwa kushilikiwa na jeshi hilo ametambuliwa kuwa ni Bw. Kahungu ambapo
tukio hilo limetokea Januari 19 mwaka huu wilayani humo.
Kwa mujibu
wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa polisi
mkoani hapa, Bw. Phillip Kalangi, kwa kipindi kirefu, Bw. Kahungu alikuwa
akimtuhumu mkewe Bi. Vanencia kumzalia watoto wa kike pekee.
“Katika
uchunguzi wa awali wa Jeshi la polisi ubaini kuwepo kutoelewana katgi ya
wanandoa hao, mke na mume ambapo Bw.
Kahungu alikuwa akituhumu mkewe kumzalia
watoto wa kike pekee wakati yeye anataka wa kiume”alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo, wakati mkewe akiwa mjamzito yeye alikuwa na mategemeo
makubwa kuwa mkewe atamzalia mtoto wa kiume.
Hata hivyo,
bila kutarajiwa baada ya mkewe kujifungua mtoto wa kike na kupita takribani
mwezi mmoja, Bw. Kahungu alimuua mtoto huyo ambaye jina lake halijajulikana kwa
kumnyonga shingo.
Bw. Kahungu
anatarajiwa kufikishwa ,mahakamani wakati wowote ,mara baada ya uchunguzi wa
polisi kukamilika.
mwisho
No comments:
Post a Comment