Na Theonestina Juma, Kagera
ZIKIWA zimepita siku takribani 21 tu
Askari polisi kuuawa kikatili wilayani Ngara na wananchi, wengine wawili
kutoka wilayani Ngara wameuawa tena kikatili kwa kucharangwa mapanga
na wanachi wilayani Karagwe wakiwadhania kuwa ni majambazi na kisha
kuteketeza kwa moto gari waliokuwa nayo.
Tukio hilo la kusikitisha
limetokea Januari 6, mwaka huu saa 2.30 katika kijiji Kasheshe kata
ya Rugu upande wa wilaya ya Karagwe wakati walipofika kijijini hapo kwa
kile kinachodaiwa kufuatilia mtu mmoja alikuwa na meno ya tembo.
Askari
aliyeuawa wamejukana kuwa ni pamoja na Sanjeti Thomas Migiro mwenye
namba E1446 mwenyeji wa mkoani Mara na Askari wa usalama barabarani
Koplo Damas Kisheke mwenye namba E 8889 mkazi wa Kamachumu Muleba
mkoani hapa wote watumishi wa jeshi hilo kituo wilayani Ngara.
Katika
tukio hilo ambalo kulikuwepo na askari watatu mmoja aliyejulikana kwa
jina la Braiston aliyekuwa na bunduki la jeshi hilo alikimbia na
kuwaacha wenzake wakisulubishwa hadi kufa kwa kuogopa wananchi kumpora
silaha hiyo.
Habari zaidi zinasema kuwa katika tukio hilo gari la
askari Damas aina ya IPSUM ilichomwa moto na wananchi hao , na hii ni
ikiwa zimepita kama wiki mbili tu wananchi hao kuchoma moto gari la watu
waliodaiwa kuwa ni majambazi.
Imeelezwa kuwa chanzo cha mauaji hayo
ya kutisha, polisi hao walifika wilayani humo, kumtafuta mtu aliyekuwa
na meno ya tembo ambapo walifanya kazi hiyo hadi saa 2.30 na kufanikiwa
kumkamata akiwa na meno saba na kuanza kuondoka eneo la tukio.
Hata
hivyo, kulingana na maelezo zaidi kutoka eneo la tukio zinadai kuwa
polisi hao walikuwa na biashara yao binfasi na mmoja wa wananchi wa
kijijini hapo, ambapo inasemekana kuwa walitaka kumdhulumu mwananchi
huyo mali yake, na hivyo kuamua kuwapigia simu wananchi wa kijiji hicho
kuwa kuna majambazi wako kijijini hapo na wanaondoka kuelekea Ngara.
Kutokana
na wananchi hao kuchoshwa na vitendo vya ujambazi, polisi hao wakiwa
safarini kurudi Ngara, walikuta mawe na magogo yakiwa yamepangwa
barabarani huku wananchi wakiwataka washuke kutoka katika gari lao
walikataa na mmoja wao kufyatua risasi iliomjeruhi mwananchi mmoja.
Aliyejeruhiwa
na risasi katika sehemu ya kiganja chake cha mkono ametajwa kuwa ni
Jovinary Gabanu (35) mkazi wa kijijini hapo ambaye amelazwa katika
hospitali teule ya wilaya ya Nyakahanga.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa
wakati wananchi wakipambana na polisi hao wawili, askari wenzao
waliwahi walifika eneo la tukio, ambapo inasemekana kuwa walisikika
mmoja wa askari hao akitamka maneno kwa kusikitika ahh…afande ‘Damas
umetuaibisha’ ambapo hapo ndipo ilichochea zaidi hasiara za wananchi na
kuanza kuwapiga na kuwaua papo hapo.
Mwananchi mmoja wa kijiji hicho,
aliyejitambulisha kwa jina la Bernedetha Salvatory (64) alisema milio
ya risasi zilianza kusikika kabla ya saa 2 usiku na kutokana na kuwa na
woga kufuatana na kuvamiwa mara kwa mara na majambazi hakuweza kufika
eneo la tukio hadi leo asubuhi.
Katika eneo hilo ambalo limefurika
watu, huku kamati ya ulinzi na usalama wakihaha kila kona mwenyekiti wa
kamati hiyo ambaye ni Mkuu wa wilaya hiyo Bi. Dary Rwegasira alifika
eneo la tukio ili kujua ni kitu gani kilichotokea huku akiwataka
wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Hata hivyo, habari
kutoka ndani ya Jeshi la polisi zinaeleza kuwa kuwa wakati polisi hao
wakitafuta mhalifu huyo kijijini hapo, hawakuweza kuripoti katika kituo
cha polisi cha wilayani Karagwe ili kuweza kupewa polisi mwingine wa
kuwaongozana nao kutokana na wananchi wa kata hiyo kuwa na mahusianano
mabaya na jeshi la polisi.
Chanzo cha polisi hao kuwa na mahusiano na
Jeshi la polisi ni kutokana na siasa na kazi ambapo baadhi ya wanasiasa
wamekuwa wakiwachochea wananchi kuwachukia polisi kuwa wanawanyanyasa
ambapo wananchi wa kata hiyo inadaiwa kuwa ndiyo chanzo cha aliyekuwa
Mkuu wa upelelezi mkoani Kagera, Peter Matagi kuhamishwa.
“Unajua
wananchi wa kata hii hawana mahusiano mazuri na askari polisi na chanzo
ni baadhi ya wanasiasa, hawataki kumwona polisi katika eneo hili hadi
kufikia polisi hawa kuuawa kikatili kiasi hiki chanzo ni hicho”alisema
mwananchi mmoja wa wilayani humo.
Hata hivyo, askari Braiton
aliyekimbia alipatikana usiku huo saa 9,ambapo Kamanda wa polisi Mkoa
Kagera Phillip Kalangi akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu ya
kiganjani alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa alikuwa safarini
kuelekea eneo la tukio kutokana na kuwa mbali.
Baadhi ya wananchi wa
kijiji hicho wameone Alisema “kwa sasa sina taarifa kamili juu ya tukio
hili, lakini niko njiani kuelekea eneo la tukio, tuwasiliane mchana
ndipo nitakuwa na taarifa kamili”
Miili ya polisi hao yamehifadhiwa
katika hospitali teule ya wilaya ya Kagarwe ya Nyakahanga yakisubiri
utaratibu wa kusafirishwa makwao.
sha kusikitishwa na jinsi polisi
walivyowahi kuchukua miili ya askari wenzao na plate namba ya gari hilo
pamoja na meno ya tembo na kuondoka nayo, wakati kwa raia wakiuawa
hivyo, polisi huleta daktari kuwapima kwanza.
Hili ni tukio la pili
kutokea mkoani kagera ndani ya siku 21 ambapo Desemba 15 mwaka jana
katika kata ya Mugoma wilayani Ngara askari wawili waliuawa kikatili kwa
kucharangwa mapanga baada ya kumuua raia wema kwa kutwanga risasi baada
ya kutokea kutoelewana kati yao na raia huyo.
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya Nyakahanga
wilaya ya Karagwe Dr Andrew Cesari
amedhibitisha kupokea miili ya
marehemu hao na alisema kuwa uchunguzi
wa kitabibu umebainisha kuwa vifo vya marehemu hao vilitokana na kipigo
kikali kilichosababisha majeraha ya
kuvuja damu nyingi na kupelekea mauti hayo.
No comments:
Post a Comment