Wakati dunia nzima ikisherekea mwaka mpya, katika Manispaa ya Bukoba Kata ya Hamugembe wamepokea mwaka mpya kwa mabomu ya machozi yaliokuwa yanarushwa na jeshi la polisi mjini hapa.
Mvua za mabomu ya machozi yalianza kumiminika katika kata ya Hamugembe saa 1.15 usiku wakati makundi ya vijana walipofurika barabarani kusherekea mwaka mpya kwa kuchoma matairi na majani kati kati ya barabara na kuzuia baadhi ya magari kupita.
Kutokana na Jeshi la polisi Mkoani Kagera kupiga marufuku, ufyatuliaji wa fataki na uchomaji moto matarairi barabarani, baadhi ya watu hasa wa kata ya Hamugembe hawakuweza kutekeleza hilo na hivyo kuamua kuingia mitaari kushoma matairi.
Katika harakati za polisi kushusha mambomu ya machozi mithili ya mvua kwa lengo la kuwatawanya vijana hao ili kurudi majumbani kulala, hawakuweza kuelewana na jeshi hilo, na hivyo nao kuanza kupambana nao kwa kuwarushia mawe mithili ya mvua.
Blogi hii ilishuhudia, vijana wakichoma matairi ya magari katika eneo la mitaga kata ya Hamugembe huku baadhi yao wakisikika kuwaita polisi wako wapi waje wapambane nao.
Hata hivuo kutokana na kuwahitaji, haichukua muda baadaye milioni ya mabomu ya machozi yalianza kurindima zaidi ya mara tano katani hapo.
Katika majimbizano hayo, watu hao waliponda mawe gari la polisi na kuvunja kioo cha gari hilo lililokuwa likiendeshwa na askari aliyejulikana kwa jina laRashid na kunusurika kutwangwa jiwe sehemu za kichwani.
Hii si mara ya kwanza Bukoba kupokea mwaka mpya kwa mabozi ya machozi, kwani hata mwaka jana wakati wakiupokea katika kata hiyo hiyo, walipigwa mabomu ya machozi na hivyo kuonekana kwao kama jambo la kawaida.
No comments:
Post a Comment