Na
Theonestina Juma, Bukoba
MAKAMU wa
Askofu waKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Dkt. Methodius Kilaini amewataka
waumini kanisa Katoliki Mkoa Kagera kushiriki kikamilifu katika wiki ya sherehe
ya Muadhama Laurean Kadinali Rugambwa anayetarajiwa kuzikwa masalia yake rasmi
Oktoba 6, mwaka huu katika kanisa kuu la Jimbo la Bukoba.
Rai hiyo
imetolewa leo na Askofu Dkt.Kilaini wakati akihubiri katika misa ya pili
iliofanyika katika la kanisa la Rumuli ikiwa ni kuanza kwa wiki ya maadhimisho
ya Kadinali Rugambwa.
Askofu
Kilaini alisema kwa kumuenzi zaidi matendo ya Kadinali huyo, mweusi wa kwanza
Mwafrika, waumini wanapaswa kushiriki katika sherehe zake zilizoanza
kuadhimishwa katika Jimboni humo Septemba 30, mwaka huu ambapo kilele cha
maadhimisho hayo yatakuwa Oktoba 7, mwaka huu.
Alisema
katika sherehe hizo za kuhamisha masalia ya Kadinali Rugambwa Oktoba 6,
shughuli hizo zitaanza asubuhi katika parokia ya Kashozi alikozikwa kwa muda
ambapo yatafanyika maandamano kutoka katika parokia hiyo hadi kanisa kuu la
Bukoba mjini.
Alisema shughuli
za kuzika rasmi masalia yake yatafanyika kuanzia saa 9.00 alasiri ndani ya
kanisa kuu ambalo alitaka akizikwe ambapo kanisa hilo tayari limeshakamika kukarabatiwa.
Akielezea kwa wiki nzima shughuli zitazofanyika, alisema
kuwa ni pamoja na kusomwa misa katika kijiji alikozwaliwa cha Rutabo,
alikobaziwa parokia ya Kagondo na Rutabo
alikojenga seminari ,Bunena mjini Bukoba na kisha Kashozi ambako siku anatangazwa kuwa
Askofu alikuwa akifanya shughuli za kiuchungaji katika parokia yote hayo ni
kuadhimisha kumbu kumbu yake.
Alisema enzi
za uhai wa kadinali Rugambwa alikuwa kiungo wa Waafrika, maaskofu wa kiafrika
na waumini nje ya nchi hadi ikafikia hatua wazungu wakaanza kuwapa waafrika
nafasi za uongozi.
“Kadinali
Rugambwa alikuwa kama bendera iliowekwa juu ya milingoti ili kila mtu aione,
hii ni kutokana na yeye aliweza kukaa na wazungu katika kiti kimoja kujadili
mambo mbali mbali yahusuyo jamii na dini, hivyo yeye alikuwa kama kiungo”alisema
askofu Kilaini.
Alisema
katika Tanzania Kadinali Rugambwa ni muasisi wa Baraza la maaskofu na alikuwa
mchungaji mwema kutokana na kuwapenda waumini, watawa na mapadri wake.
Halidhalika
alikuwa mpenda maendeleo, ambapo katika enzi za uhai wake aliweza kuanzisha
miradi mbali mbali za kanisa kama ujenzi wa shule za sekondari, hospitali na
vtuo vya afya ambapo alikubalika kwa dini zote kulingana na maelezo ya watu
mbali mbali waliokuwa naye karibu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment