Sunday, September 9, 2012

Mwanafunzi auawa achunwa ngozi ang'olewa meno, ubongo na nyeti zake

Na Theonestina Juma, Bukoba
MTOTO Beatha James (12) mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Nyaligamba Kata  Muhutwe wilayani Muleba ameuwawa kikatili na watu wasiojulikana kwa kuchinjwa shingo na  kuchunwa ngozi, kunyofolewa ulimi, nyeti zake na ameg’olewa meno.
Kama hilo halitoshi kichwa cha marehemu kimekutwa na matundu makubwa kana kwamba wauwaji hao wametoa ubongo wake.
Tukio hilo la aina yake ambayo inawakumbusha watu mauaji kama  hayo yaliokuwa yakitokea Mkoani Mbeya yamemkumba mwanafunzi huyo, Septemba 7 mwaka huu baada ya mwili wake kuokotwa na watu waliokuwa wakilinda mazao yao yasiliwe na wanyama wahararibifu ambao waliweza kuutambua mwili huo na kutoa tarifa.
Mwili huo hulipatikana katika katika maeneo ya kaboya karibu na kambi ya  Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ ) Wilayani Muleba nje ya kata nyingine tofauti na kata alimokuwa akiishi.
Mwili wa mtoto  Beatha ulikutwa ukiwa umechunwa ngozi, shingo imekatwa, ulimi umetolewa, meno yameng’olewa , sehemu zake za siri zikiwa zimeondolewa, amenyolewa nywele  huku akiwa na matundu kichwani kana kwamba alitolewa ubongo.
Akizungumza na gazeti hili mama mkubwa wa mtoto Beatha ambaye alikuwa akiishi naye katika kitongoji cha  Bitende, Bi. Eyudosia  Salvatory  alisema marehemu aliondoka nyumbani Agosti 29 mwaka saa 3.30 asubuhi akielekea kwa mama yake mwingine aitwaye Mariagoreti  Ishengoma
Bi. Salvatory alisema pamoja na kupata taarifa za kupatikana kwa  mwili wa mtoto huyo lakini ulikutwa ukiwa kuwa umeharibika pamoja na sura yake  kupota kabisa hali iliowalazimu kuweza kumtambua kwa mavazi yake aliokuwa amevaa kwa siku hiyo.
“Tulimtambua  kwa mavazi aliyokuwa amevaa kabla ya kukutwa na mkasa huo na chupa ya maziwa  aliyokuwa nayo’’alisema mama mkubwa wa marehemu.
Kwa upande wa Mtendaji wa Kijiji  cha Bisore Bw.Dominic  Damasenyi alikiri kutokea kwa tukio hilo na taarifa zilitolewa kwake na wanafamilia ambapo naye  alitoa katika uongozi wa  Kata na polisi.
Bw.Damasenyi  alisema  madaktari  walifika eneo la tukio kupima na kisha kutoa ruksa za  shughuli za mazishi kwa wanafamilia kuendelea.
Naye Diwani wa kata ya Muhutwe Bw.Justus Magongo  akizungumza na gazeti hili alikiri kuwepo kwa tukio hilo katika kata yake na kueleza kuwa mtoto huyo alikutwa ameuwawa akiwa ameondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili ikiwemo kuondolewa baadhi ya viungo vyake vya mwili kama matiti, meno na sehemu zake za siri.
Hata hivyo kwa upande wa taarifa za kuchunwa ngozi, Dini huyo alisema kuwa hawezi kuthibitisha kama kweli alichunwa ngozi  kwani yawezekana ikawa alibabuka au kweli alichunwa kwa sababu wakati wa uchunguzi wa madaktari hakuwepo na hajapata taarifa za uchunguzi wa kina.
Aliwataka wananchi kuachana na vitendo vya ushirikina kufanya hivyo ni kuwatesa wananchi bila sababu mali zinapatikana kwa juhudi na maarifa sio ushirikana na nguvu za giza.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mayondwe Bw.Swahibu Mfuruki alisema  maiti ya mtoto  huyo ilikutwa imetelekezwa katika Kata yake maeneo ya Kawalinda karibu na kambi  ya Jeshi ya Kaboya.
Bi.Salvatory  alielezea mazingira ya kupotea kwa mtoto huyo hadi anapatikana akiwa ameuawa alisema kuwa siku mtoto huyo anapotea  alienda kwa mama yake mwingine Bi. Ishengoma ambapo alipofika kwake alimtuma kwa jirani wa huyo mama aliyejulikana kwa jina la Erasmo Sosthenes  ambapo alitumia muda  mwingi bila kurejea hali iliowalazimu kupiga simu kumuulizia.
Hata hivyo, majibu waliopewa ni kuwa hajafika na maziwa bado hayajachukukuliwa.
Alisema ilipotimu saa7.00 mchana walianza kumtafuta ndipo alijitokeza mama mmoja  aliyemtaja kwa jina la Bi.Aneth akawaeleza kuwa  wakati akiwa shambani saa 4. asubuhi alimuona mtoto Beatha akiwa amefuatana na  mwanaume mmoja  aliyekuwa amebeba mfuko wa (Rambo)  salfulet ambapo alimuuliza  anakwenda wapi na kumjibu  kuwa  anamuelekeza  mwanaume huyo njia ya kwenda Maziba  ziwani maeneo ya Bubabo.
Kutokana na hali hiyo,  wananchi waliamua kufuatilia njia hiyo wakishirikiana na wanafamilia kumtafuta mtoto huyo walipofika maziba walielezwa na wananchi wa eneo hilo kuwa wamemuona mtoto huyo akiwa amefuatana na mwanaume lakini hawakujua walikoelekea.
Wakati wakielezwa  wasifu wa mwanaume anayedaiwa kumchukua mtoto huyo na watu ambao wanatunzwa  kwenye nyumba ya mkazi wa eneo hilo waliyemtaja kwa jina la Bw.Jacob wakati wakielekea kwa mtu huyo walikutana na mtoto wa Jacob alipowaona alikimbilia kwa baba yake.
Alisema walipofika kwake wananchi walimhoji walipo watu hao  anaoishi nao akasema hawapo na hajui majina yao wala wanakoishi walifika kutafuta kazi  nyumbani kwake  isipokuwa mmoja wao alimueleza kuwa  ana ‘dili’ la hela  la kwenda kuiba mabati  maeneo ya Igurubiri
Alisema  wananchi walimchukua hadi muhutwe  akiambatana na mtoto wake anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka ( 13 )mwanafunzi wa darasa la saba walipombana alisema mwanaume huyo alifika kwao akiwa na mtoto aliyevaa sketi ya kitenge na fulana walilala lakini walidamka na waliondoka  usiku akiwa ameshikwa na vijana ambao hakutaja idadi yao wala majina yao kumpeleka asikokujua.
Alisema  baada ya maelezo hayo ya mtoto, walipiga simu polisi  wakafika  wakaweleza watoe nauli ya usafri kwa ajili ya kumpeleka Jacob kituo cha Muleba kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa  mtoto.
Polisi  walipigia simu na kufika eneo la tukio siku hiyo,  wakiwa na madaktari  kwa ajili ya kufanyia uchunguzi mwili wa marehemu ambapo baada ya kazi hiyo walikabidhi wanafamilia mwili huo kwa lengo la kuendeea na shughuli za mazishi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment