Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi
Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini
Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi
wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama
cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika
vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo
wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo
Mwanahabari huyo Daud
Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema
Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .
Kabla
ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo
hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma
kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari
kuondoka katika ofisi yao.
Chanzo cha mwanahabari Mwangosi
kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la
Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka
kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo
askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa
bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka
chini .
Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari
huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali
ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa
chumba cha kuhifadhia maiti .
Katika vurugu hizo zilizodumu kwa
takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe
kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi
yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja
Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.
Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari
JESHI
la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya
siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo
(CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.
Hata
hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa
matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai
viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha
mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.
Kamanda wa polisi wa
mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake
alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa
Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.
"
Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi
wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na
shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi
wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na
wanasiasa "alisisitiza
Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa
kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa
tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha
kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi
hiki cha sensa.
"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa
kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi
kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda
huyo wa polisi.
Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la
sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana
na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi
linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa
kwa jeshi hilo.
Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la
polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa
kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata
Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya
ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu
aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.Majibu ya Dkt SlaaWakati
jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa
kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt
Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na
mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote
litakalojitokeza .
Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya
kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira
hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona
jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.
"Tumemsikiliza
kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu
asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia
simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa
sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu
asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano
yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida
hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.
Pia
alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa
wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na
watapambana kwa lolote .
MWISHO
No comments:
Post a Comment