Na Theonestina Juma
MWANAMKE mmoja makazi wa kijiji cha Buhororo wilayani Ngara,
amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai ya kila mara alikuwa akipata ujumbe kutokana na
watu kama majini yaliokumtaka ajinyonge.
Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana kutoka wilayani Ngara na kuthibitishwa na Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Paul Bwinyo tukio
hilo la aina yake lilitokea Septemba 26, mwaka huu kijijini hapo.
Mwanamke aliamua kujitia kitanzi amejulikana kuwa Bi.Christina
Zemitembe (37) na kwamba alijinyonga nyumbani kwao alikokuwa akiishi na mama
yake mzazi Bi.Zemitembe (70).
Alisema siku ya tukio, mwanamake huyo aliamuaka asubuhi na
kupanda juu ya meza na kisha kujitia kitanzi, ambapo kwa wakati huo mama yake
mzazi alikuwa ameenda shambani.
Imeelezwa kuwa muda wa saa saba mama yake aliporejea kutoka
shambani alikuta mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa kwa ndani jambo ambalo
lilimlazimu kuomba msaada kwa majirani.
Alisema majirani hao walilazimika kuharibu mlango ambapo
walipoingia ndani hawakuweza kuamini kilichotokea, kwani tayari mwanamke huyo alishajitia kitanzi na kubaki
akining’ngia juu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la
Bi. Winfrida Thomas akielezea hali aliokuwa nayo mwanamke huyo kabla ya kujiua,
alisema kila mara Bi. Christina alikuwa akisema juu ya kutaka kujiua kwa
kujinyonga.
“Mwezi Aprili mwaka huu Christina alikuwa akisikika akisema kuwa amekuwa akipata
maono (ujumbe) kutoka watu kama majini ambayo yanamtaka ajinyonge.”alisema.
Hata hivyo, Bi. Thomas alisema kuwa kutokana na maneno yake
hayo walidhani kuwa alikuwa akitania na hawakujua kama kweli alikuwa
akidhamiria kutenda kitendo hicho,Jehi la Polisi Mkoani Kagera, bado
linafuatilia juu ya tukio hilo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment