Na
Theonestina Juma, Bukoba
ZIKIWA
zimebaki takriban siku 10 mwili wa aliyekuwa Kadinali wa kwanza Mwafrika,Muadhama
Laurean Rugambwa kuhamishiwa katika jengo la Kanisa katoliki mjini Bukoba,
uongozi wa kanisa hilo umetoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioanza kunufaika
tukio hilo bila ridhaa yao.
Hatua hiyo
imekuja siku chache baada ya baadhi ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba
kutengenezesha fulana zenye nembo ya kanisa hilo pamoja na picha ya Kadinali
Rugambwa wakiziuzwa kwa sh. 12,000 bila
ridhaa ya uongozi wa kanisa hilo.
Kutokana na
hali hiyo Katibu wa Askofu wa Jimbo la Bukoba, Padri Deodatus Rwehumbiza akizungumza
na gazeti hili jana (leo) alisema waumini watakaonunua bidhaa za
wafanyabiashara ambao zimetengenezwa bila baraka za kanisa hilo, hawatapewa
kipaumbele siku ya sherehe hiyo kama ilivyo kwa waumini watakaovaa sare
yalioandaliwa na uongozi wa kanisa hilo na watawaona kana kwamba hawajavaa sare
za sherehe hiyo.
Alisema watu
hao hawatapata mafao kama wale watakao vaa sare zao kwani bidhaa hizo
wamezitengeza kwa ajili ya kuwezesha siku ya tukio watakaohudhuria waweze kufahamika
kiurahisi na kununua sare hizo wanachangia ufanisi wa sherehe hiyo na kwamba
sare zao zinafahamika na hivyo hao ndiyo watakaopewa nafasi ya kwanza.
Alisema kwa
wale watakaokuwa na sare za kughushi na kwa kuwa wameshambulia hilo mapema na
kuwataarifu, watakaokaidi watawaona kama wale waliotoka mitaani na kuingia
katika shehere hiyo.
Hata hivyo,
gazeti hili lilipotaka kujua kwa siku hiyo hawatawathamini, Padri Rwehumbiza
alisema kuwa watawathamani, lakini kupata hudhuma kama wale watakaovaa sare
zao, haitakuwa rahisi mfano kama sehemu za kukaa zitakazoandaliwa.
Katibu hiyo
alitoa kauli hiyo, baada ya gazeti hili kutaka kujua, iwapo waumini wao watakuja kanisani siku hiyo wakiwa wamevaa
mavazi yaliotengenezwa na wafanyabiashara bila ridhaa ya uongozi wa kanisa
hilo, watafanyaje.
Alisema
kutokana na kuwa makini katika maandalizi ya sherehe ya Agosti 6 na 7,ya kuhamisha mwili wa Kadinali Rugambwa
kutoka katika kanisa ya Kashozi alikozikwa kwa muda, tayari walishabaini ujanja
wa baadhi ya wafanyabiashara hao na wamekuwa wakiwataarifu waumini wao juu ya
jambo hilo.
Alisema
mmoja wa mfanyabiashara wa mjini hapa ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake,
walifika katika duka lake na kukuta fulana ambazo zilitengenezwa rasmi
kuhusiana na siku ya tukio hilo.
“Tulifika katika
mmoja ya duka mjini Bukoba na kukuta
fulana zinazohusiana na sherehe ya kuhamisha mwili wa Kadinali Rugambwa,… na
kubariki kanisa kuu….tulijifanya kama wanunuzi, tulinunua sh.12,000 na kukatiwa
risiti”alisema
Alisema
kutokana na hali hiyo tayari walishatoa taarifa kituo cha polisi kuhusiana na
tukio hilo, ambapo katika mahojiano zaidi mfanyabiashara huyo alisema kuwa
fulana ndizo zilikuwa bidhaa za kwanza kuingizwa sokoni ambapo walikuwa na
mpango wa kuteneza vitambaa.
Hata hivyo,
Padri Rwehumbiza alipotakiwa na gazeti hili kueleza kama fulana hizo
zimetengezwa mjini Bukoba au nje ya mjini hapa alisema kuwa haijajulikana
fulana hizo zimetengenezwa wapi, wala haijajulikana wako wafanyabiashara
wangapi, zaidi hilo sasa ni jukumu la polisi kufuatilia.
Kuhusiana na
hatua walikofikia ya maandilizi ya sherehe hizo, Katibu huyo alisema kuwa
yanaendelea vizuri na kwamba yatafanyika jinsi yalivyo pangwa na kwamba zaidi
ya wageni 5000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria.
Kuhusiana na
viongozi wa kitaifa alisema kuwa mialiko
wametuma kwa wote ambapo majibu
yanayopatikana hayaoneshi kukatisha tamaa.
Septemba 23,
mwaka huu katika kanisa katoliki la Rumuli yalisikika matangazo ya kanisa hilo
yakieleza juu ya kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotengeneza fulana na
vitenge yenye maandishi kuhusiana na matukio ya sherehe hizo, bila idhini ya
kanisa hilo.
Katika
matangazo hayo yalieleza kuwa fulana hizo zina maandishi kwa nyuma, ambapo hata
bei zao hawajaafikiana nao na uongozi wa kanisa.
Sare
zinazouzwa na kanisa hilo katika maduka yake mjini hapa, fulana na vitenge vinauzwa
sh. 13,000 ambapo fulana za wafanyabiashara binafsi zinauzwa sh. 12,000.
|
No comments:
Post a Comment