Bi
Asha Ismail mkazi wa Kitomanga mkoani Lindi akitwishwa ndoo ya maji na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda baada ya
kuzindua kisima cha maji kilichojengwa na kampuni ya CCP inayojenga
bomba la mafuta kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam. Mhandisi
Baltazari Mrosso akitoa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi
linalotoka Mtwara mpaka Dar es salaam kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda wakati anakagua maendeleo ya ujenzi
wa bomba hilo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akizindua na
kuweka jiwe la msingi la kiwanda cha saruji cha MEIS eneo la Machole
mkoani. Sehemu iliyoandaliwa kitakapojengwa kiwanda cha saruji cha MEIS eneo la Machole mkoani. Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda akitembelea
baadhi ya maeneo ya kiwanda cha saruji cha MEIS baada ya kikizindua.
No comments:
Post a Comment