Sunday, January 26, 2014

Serikali yakatakiwa kufuta nauli za vivuko maeneo ya vijijini

Na Theonestina Juma, Kagera
 WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoa wa Kagera wametakiwa kufuta gharama za  vivuko kwa watembeao kwa mguu kutokana na hiyo ni huduma kwa jamii na sio biashara.
Ushauri huo umetolewa jana na Mbunge wa Viti  Maalum (CCM), Bi. Elizabeth Batenga wakati akizungumza katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika mjini hapa.
Alisema”wanachi wanaovuka vivuko vilivyoko katika mkoa wa Kagera wanatakiwa kufutiwa tozo, kutokana na wanaovuka vivuko hivyo ni wale wasio kuwa na uwezo, wakati mnapanga kuongeza gharama mimi ninaona mfute, kwani hiyo ni huduma kwa wananchi”
 Hivi wale wanaotembea barabarani, wanatozwa na nani si wanatembea bia kutozwa chochote si ni huduma inayotolewa kwa wananchi sasa ni kwa nini wanaovuka vivuko wao watozwe fedha kwa ajili ya nini, hapa si kuwaonea ?alihoji
Bi. Batenga alisema wakati TEMESA wakiangalia kutaka kuongeza viwango vya nauli ya vivuko vyake, wafikirie kutafuta ni kwa namna gani wanavyoweza kuondoa tozo hizo kwa wananchi hasa ikizingatiwa kuwa vivuko hivyo viko maeneo ya vijijini ambako kuna wananchi wengi.
“Huko vijijini mwananchi kupata hata sh. 200 kwake ni shida, lakini cha kushangaza mwananchi anayevuka kwenda ng’ambo ya pili kwenda kulima anatozwa, hela kwa ajili ya kuvuka… si dhani kama ni haki… serikali itafute namna ya kuwafanya hawa wananchi”alisema
Alisema katika maeneo hayo ya vijijini, wananchi wanaoishi katika upande wa pili wanalazimika kulipia nauli kuvuka kwenda upande mwingine kwenda msibani hali inayowafanya kufikia hatua ya kushindwa kutembeleana kwa kukosa nauli.
Hata hivyo kwa upande wa Mkuu wa mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe akizungumzia suala hilo alisema TEMESA wanatakiwa kuangalia ni watu wa aina gani wa kuwatoza, kwa wale wasiokuwa na uwezo waachwe wavuke bure.
Aidha wanapaswa kuangalia kama ni vyombo vya moto to ndiyo vitozwe hela na wavuka kwa miguu waruhusiwe kuvuka bila malipo.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Kapteni Dauda Kateme akizunguzia vivuko hivyo, alisema yeye anashindwa kuwaelewa TEMESA kwani wamekuwa wakitoza ushuru magari ya halmashauri hiyo, wakati kivuko  cha Kyanyabasa kiko katika halmashauri yake.
Alisema TEMESA ikiwa ni kama chombo kinachofanya biashara wao wakitakiwa kulipa ushuru wanakataa kwa madai kuwa wao wanatoa huduma na si biashara.
Awali Kaimu Meneja wa TEMESA mkoa Kagera, Bw. Wilson Nyitwa, alisema kuwa TEMESA inampango wa kupandisha nauli za vivuko vyake ambavyo ni Kyanyabasa na mto Ruvuvu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema wao biashara bali ni huduma, ambapo kwa siku katika kivuko cha Kyanyabasa hupata kiasi cha sh. 40,000 ilihali kivuko  cha Kyanyabasa hupata sh.70,000 kwa siku.
Alisema kwa kiasi wanachotoza kwa sasa hakisaidii kitu chochote, wakati hata mishahara imepanda kwa watumishi hivyo inafikia hatua wanashindwa kujiendesha hasa ikizingatiwa kuwa wao hawapati ruzuku kutoka serikalini.
Hata hivyo, kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Zipora  Pangani alisema kulingana na uzoefu wake katika kivuko cha mto Pangani, wananchi kuruhusiwa kuvuka bure kitawafilisi kabisa TEMESA  kwani kiasi hicho kidogo wanachopata ndicho kinawasaidia katika kujiendesha.
Alishauri mpango huo wa kutaka wananchi wavuke bure isubiriwe hadi uchaguzi Mkuu 2015 upite bila hiyo itasu

No comments:

Post a Comment