Na Theonestina
Juma, Bukoba
BIBI kizee
mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja anayedaiwa kuwa ni mkazi wa
kata ya Karagabaine amenusurika kuuawa kwa kutuhumiwa ni mchawi baada ya
kukutwa ndani ya chumba cha wanafunzi wa kike usiku wa manane.
Tukio hilo
la aina aina yake ilivovutia hisia za wakzzi wengi wa Manispaa ya Bukoba limetokea
jana Januari 31, mwaka huu katika mtaa
wa KambaMilembe kata ya Hamugembe mjini hapa.
Bibi huyo
aliyekuwa amevaa kiguo cheusi kukuu kilichomfunika sehemu ya mauungo yake na kifuani
inadaiwa kuwa aligunduliwa na baadhi ya wanafunzi wa vyuo vilivyoko katika jengo
la Vijana mjini hapa.
Akizungumza na
gazeti hili mwangalizi wa nyumba hiyo, aliyejulikana kwa jina la mama Halima,
alisema yeye alipigia simu saa 8 usiku na wanafunzi hao kuwa wameingiliwa na
mtu ndani ya chumba chao.
“Mimi
nilipigiwa simu usiku wa manane, kuwa kuna mtu ameingia ndani ya chumba chao,
kwa njia ya mazingara, niliwaambia kuwa kama wanauwezo wa kumlinda hadi asubuhi
asiondoke wafanye hivyo, ili ukuche waweze kuangalia namna ya kufanya”alisema
mama Halima.
Mama akizungumzia
ni namna gani wanafunzi hao wa kike walivyogundua mtu kuwemo ndani ya chumba
chao, alisema kuwa hiyo inatokana na wafunzi kuwa kila mmoja kuwa na imani yake
kwani kuna wale wanaosali sana.
“Unajua kuna
wengine wanaimani zao, na ni makabila mchanganyiko, lakini kuna msichana mmoja ndiye alihisi kama ndani
kuna upepo mzito sana, jambo alilolazimika kuwaamisha wenzake, kuwa ndani kuna
kitu, waamuke waache taa, ndipo walipowasha taa walimkuta huyo bibi akiwa
ameketi pembeni mwa vitanda vyao”alisema
Hata hivyo
alisema kuwa, alipofika katika hosteli hiyo alfajiri na kumkuta bibi huyo,
ambapo alikuwa hazungumzi, huku akiwazuia watu kuingia humo zaidi ya viongozi
na watu ambao hakuweza kuwatilia shaka kama wanaweza kumdhuru bibi huyo.
Mama alisema
alisema kuwa yeye ameishi katika nyumba hiyo kwa kipindi cha miaka 21 na
hakuweza kutokea na tukio hilo, ambapo hili ndilo tukio la kwanza kutokea
katika nyumba hiyo, ambayo wanafunzi hao walianza kuishi humo Agosti mwaka
jana.
Kutokana na
hali hiyo, baadhi ya watu walioshika dini waliitwa kuweza kusoma sala mbali
mbali ili aweze kufunguka ambapo hata hivyo, bibi huyo hakuweza kuzungumza na
hivyo uongozi wa mtaa, Bw. Athuman Yunus kwa kushirikiana na uongozi wa kata hiyo walilazimika kupiga simu kituo cha polisi.
Bi. Kizee huyo
ambaye kwa wakati huo, alikuwa maefungiwa humo na mwangalizi wa nyumba hiyo,
ambayo mumiliki wake anadaiwa kuwa anaishi Jijini Arusha kwa kushirikiana na wanafunzi kwa lengo la kuokoa maisha yake baada ya kundi
la watu waliokuwepo eneo hilo la tukio kutaka atolewe nje ili aweze kuuawa.
Hata hivyo
polisi walifika eneo la tukio, takriban saa 3. Asubuhi na kufanikiwa kumwondoa kwenye nyumba hiyo
pasipo kudhuriwa na umati huo na kumpeleka katika kituo cha polisi.
Pamoja na
hayo, baadhi ya watu walidai kuwa Bi kizee huyo alionekana katika kituo cha
mabasi cha Bugabo mjini hapa ilihali wengine wakidai kuwa alionekana katika baadhi
ya viunga vya mjini hapa huku wengine wakidai kuwa ni kichaa.
Hata hivyo,
jinsi gazeti hili lilivyomshuhudia bibi huyo, ni mtu ambaye haoneshio dalili ya
kuwa na ukichaa wowote, kutokana na afya yake ilivyo na alivyokuwa msafi, huku
akionekana mnene na mwenye siha njema.
Desemba
11,mwaka 2012 nyumba ya mwalimu wa shule
ya msingi Kashai, Bi. Benedetha Katabaro (56) ilinusurika kuchomwa moto baada ya kutuhumiwa mchawi na kuwahifadhi watoto sita kama msukule
ambapo aliweza kuokolewa kwa mabomu ya machozi na risasi za moto.
Halikadhaka Machi 13,
mwaka 2012 watoto wawili wa familia moja waliokolews na Jeshi la polisi mjini
hapa baada ya kuzingirwa na wananchi wakitaka kuwauawa kwa tuhuma za a tuhuma
ya kutaka kumwiba mtoto mchanga kwa njia ya uchawi katika mtaa wa Kashabo kata ya Hamugembe mjini
hapa.
No comments:
Post a Comment