Wednesday, January 1, 2014

Rais Kikwete amwapisha IGP mpya, ni Afande Mangu

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande Ernest Mangu,  Naibu  Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii. PICHA NA IKULU
IDARA YA HABARI MAELEZO
Rais Dk. Jakaya Kikwete amemwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Generali wa Polisi Ernest Jumbe Mangu na Naibu wake Kamishna  Abdulrahan Omar Juma Kaniki katika viwanja vya Ikulu, Dar es Salaam jana jioni.
Katika hafla fupi hiyo iliyoshuhudiwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib Bilal, mawaziri kadhaa, viongozi wa Serikali na baadhi ya makamanda wa jeshi la polisi kiongozi huyo baada ya kiapo cha  kulitumikia jeshi hilo na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, amewaambia waadishi wa habari kuwa kazi yake kubwa itakuwa ni kupambana na uhalifu na kufuatailia migogoro miongoni mw a jamii na makundi mbalimbali, pia ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha mifumo ndani ya jeshi lake. 

Kwa upande wa naibu wake, Bw. Kaniki amesema mbali na majukumu yake ya kumsaidia Mkuu wake wa kazi ataongeza juhudi za ufuatiliaji katika ngazi ya tarafa na vijiji ili kujenga uwezo wa ulinzi shirikishi na kusisistiza kuwa jamii ina fursa kubwa katika kufanikisha suala la ulinzi katika maeneo wanayoishi.
Naye aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi , Said Mwema ameishukuru jamii kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa ambao amekuwa akiupata, kadhalika kumtakia mwenzake aliyempokea kazi ya mafanikio na amesihi jamii iendelee kumpa ushirikiano.
Kuhusu maendeleo ya jeshi hilo Bw. Mwema amesema pamekuwepo na kasi ya uimarishaji wa vitendea kazi katika kipindi kifupi, uimarishaji wa miundombinu ndani ya jeshi hilo na amesema kuna kazi mbili za utafiti wa kisayansi kuhusu mwenendo wa utendaji zilizo katika hatua ya mwisho kukamilishwa zitakazobaini ufanisi na changamoto za jeshi la polisi na kutoa mapendekezo ya kuboresha upande wa jeshi la polisi kadhalika kubaini kiwango cha mahusiano ya jeshi hilo na umma.

No comments:

Post a Comment