MAUZO ya Dhahabu nje ya nchi yemeshuka kwa kiasi cha asilimia 14.8 wakati
mauzo ya almasi yakipaa maradufu kwa kipindi cha mwaka wa fedha
uliopita wa 2012/2013.
Kushuka kwa mauzo hayo ya wachimbaji wakubwa na wadogo, kulisababishwa
zaidi na kufungwa kwa migodi ya Tulawaka, Resolute, kushuka kwa kasi ya
uzarishaji na uuzaji wa nje na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la
dunia.
Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Tawi la Mwanza, Mussa Mziya,
alisema katika kipindi hicho mauzo ya dhahabu kanda ya Ziwa kwa nje ya
nchi yalipungua kwa kiasi hicho kufikia dola za Marekani milioni 1,901.2
(karibu sh. 2.5) milioni kutoka dola 2,232.3 (zaidi ya sh. bilioni
tatu) kwa mwaka 2011/2012.
Kiasi cha dhahabu kwa wachimbaji wakubwa, kilipungua kutoka kilo
39,544.8 mwaka 2011/2012 hadi kufikia kilo 37,796.3 kwa mwaka wa fedha
uliopita wa 2012/2013 huku madini hayo yakianguka kwa asilimia 10.9
kutokana na kuimarika kwa dola.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioisha Juni 2013, thamani ya
madini toka kwa wachimbaji wadogo pia iliporomoka kwa asilimia 55.8
kufikia dola milioni 5.5 (zaidi y ash. Bilioni saba) milioni kutoka dola
milioni 9.4 (zaidi ya sh. bilioni 1.7) zilizopatikana mwaka 2011/2012.
“Thamani ya dhahabu pekee kutoka wa wachimbaji wadogo kwa kipindi tajwa
ilishuka hadi dola milioni 3.9 kutoka dola milioni 8.3 milioni mwaka
2011/2012 kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia
wakati thamni ya almasi kutoka kwa wachimbaji hao wadogo ikipaa,”
alifafanua.
Alisema almasi ya wachimbaji hao ilipanda hadi dola milioni 1.8 kutoka
dola milioni 1.2 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wake.
Mauzo ya almasi nje ya nchi yaliongezeka mara dufu kufikia dola milioni
44.8 milioni katika mwaka 2012/2013 kutoka dola milioni 11.5 mwaka
2011/2012.
Kuongezeka kwa mauzo ya almasi kulichangiwa na uhuishaji mkubwa katika
mgodi wa almasi wa Williamson Diamond, ulioko Mwadui mkoani Shinyanga.
No comments:
Post a Comment