Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa
Jimbo la BUkoba mjini (CCM), Balozi Khamis Kagasheki amesema kwa sasa ameanza
kuongopa kwa mtu ambaye si raia wa nchi akaomba uraia akapewa na madaraka
makubwa kuwa ni kitanzi.
Balozi Kagasheki ambaye ni Mbunge wa jimbo la
Bukoba mjini alisema hayo hivi karibuni wakati akiwahutubia mamia ya wakazi wa
mjini Bukoba ambapo kwa sasa anaendelea na mikutano yake ya kukutana na
viongozi mbali mbali wanaotokana na
(CCM)kuanzia ngazi ya nyumba kumi
kujadili masuala mbali mbali huku akihimiza ushirikiano na kuondokana na
makundi.
Alisema
kutokana na hali hiyo” ndiyo maana katika nchi ya Marekani imo ndani ya sheria mtu akiomba uraia wa Marekani Katiba yao iko
sawa sawa, kwani yako maeneo wanakuambia
umepewa uraia wala si wa kuzaliwa hivyo
nchini humo yapo maeneo huwezi ukagusa
wala hata usiombe”.
“Hapa naweza
kusema kuna mtu … huwezi kwenda katika nchi za watu wakakupa uraia … tena uraia
wakupewa..wa kuomba .. .matokeo yake wewe unaanza sasa kuwahujumu, kuwaibia,
kuwakejeli,kuwakiburi na kujaa jeuri
haiwezekani kama umepewa uraia unapaswa kufanya kazi na wale raia wa
kuzaliwa wa nchi hiyo nenda kwa
utaratibu wa nchi hiyo”aliongeza
Alisema yote
yanafanyika kwa nia nzuri lakini mtu akipewa uraiwa anapaswa kufanya kazi vyema
na waliozaliwa pale na si kufanya unavyotaka.
“Nenda
kamulize hata leo kuhusu uraia wake umekaaje …. atakuwambia kuwa Waziri wa
mambo ya ndani alitia mkono wake pale ndiyo maana nikapewa, umeshapewa sasa
fanya vizuri …yote haya nayasema kwa nia nzuri sio kwa nia ubaya”alisema
Na kuhoji
kuwa … “Wazungu wanasema, After role …if we can not speak for her…. yaani baada ya yote hayo kama hawataisemea bchi yao
ni nani atakaye isemea? Hayupo!
Alisema
kutokana na hali hiyo, kwa sasa katika harakati zao za kuanza kujenga mji wa
Bukoba kwa wale ambao wana nia ya kuvuruga wawapishe wakae pembeni .
“Mnajua kuna
watu wengine wako humu mjini wana maneno sikuweza kuwataja majina yao … kwa
sababu hata nikiwataja nitakuwa nimejiteremsha kwao… ndiyo sababu sitaki
kuwataja “alisema.
Alisema kwa
sasa wataanza kuaza kukaa vikao mbali mbali kwa nguvu zote ili kujenga kwa
pamoja mji wao kwani Bukoba itajengwa na wana Bukoba wenyewe na kwamba katika
vita iliokuwemo ndani ya Manipaa hiyo, aliyeishinda ni WanaBukoba na wala si
Mbunge na baadhi ya Madiwani.
Alisema
upotevu wa sh. bilioni 2.5 zilizopotea ambazo zingewezesha kuleta mabadiliko
makubwa ndani ya Manipaa hiyo hakuna anayeiona zaidi ya kuona ‘kamunobele’.
Alisema
pamoja na kuwepo kundi la watu wanaosema
kuwa wapo watu wanaosema kuwa Kagasheki
ni mwiba anayewachuma yeye yuko na atakuna nao katika uchaguzi Mkuu unaoratajia
kufanyika mwakani.
“Mimi hapa
bado nilikuwa najifikiria, itakuwaje mwakani… kuna watu nasikia kuwa
wanamwandaa mtu I mwingine aje awe Mbunge wa Jimbo hili, kwa kuwa wapo watu
wanaojifanya wanajua siasa nawambieni fanyeni mtakavyofanya mtanikuta
uwanjani”alisema”
Alisema
waliosema kuwa Madiwani wa CCM wameungana na upizani kumwondoa meya hayo ni
maneno ya kahawa, kwani walikuwa wakitetea haki ya wana Bukoba na hatua
iliofikia ya kuwafukuza madiwani wanane,
hakuna chama chochote kinachoweza kufanya hivyo, kwani kuwafukuza wajue kuwa
CCM kwa heri.
“Hata ngazi
ya CCM haifanyi hivyo, kuna vitu vya
kuangalia… kwa watu wenye akili hawawezi kufanya kama nyie mlivyoamua”alisema
Matamshi hayo
ya Mbunge Kagasheki yanakuja siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi wa
mahesabu ya serikali (CAG ), Bw. Ludovick Utouh kutoa taarifa ya uchunguzi
maalum uliokuwa ukifanywa ndani ya Manispaa hiyo kufuatia ombi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na mvutano uliodumu
kwa miaka miwili kati ya Mstahiki, Meya Dkt. Anatory Amani, Mbunge na baadhi ya
Madiwani kupinga uendeshaji wa Manispaa hiyo katika utekelezaji wa miradi.
Katika
ripoti ya CAG ulibaini kuwepo kwa ufisadi mkubwa uliofanywa katika Manispaa
hiyo wakati wa utekelezaji wa miradi mbali mbali kama viwanja 5,000 ujenzi wa
soko la kisasa, kituo cha kitega uchumi, kituo cha mabasi, kituo cha kuoshea
magari.
Pia si mara
ya kwanza Mbunge Kagasheki kusema kuwa ndiye alimpa urai Dkt. Amani ambaye
inadaiwa kuwa ni raia wa nchini Uganda ambapo pia amekuwa akieleza kuwa yeye
ndiye aliyemchonga hadi akafikia hatua ya kuwa Meya wa Manispaa hiyo, hali
iliomfanya kukorofishana na aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Samuel
Luangisa, ambapo Balozi Kagasheki amekuwa akikiri wazi kumkosea Bw. Luangisa.
No comments:
Post a Comment