Na Theonestina Juma
BAADHI ya
Wafanyabiashara wa mjini Bukoba wameitaka serikali kufuta kodi wanaozotozwa na
Jeshi la Zimamoto kutokana na wao huduma wanazotoa ni kama majeshi mengine
nchini.
Kauli hiyo
imetolewa jana na baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wakizungumza na Naibu
Waziri wa fedha, Adam Malima katika
ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera mjini Bukoba.
“Unakuta
kila mwezi Jeshi la zima moto linazunguka katika maeneo ya biashara zetu
kukusanya kodi ambazo hatuzijui ni kwa ajili ya nini, wao hawana tofauti na
majeshi mengine zaidi ya sita wanazotoa huduma kwetu bure, mbona Jeshi la
polisi wanatulinda na mali zetu bila kututoza kodi”alisema mfanyabiashara,
Jemsi Mwanga.
Mwanga alienda
mbali zaidi kwa kwa kuhoji kuwa
huenda Jeshi la Wananchi (JWT) ambao wanajukumu kubwa la kulinda mipaka yetu
wakianza kukusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara hali itakuwaje kwao?
Kuhusu
mashine ya EFD wafanyabiashara hao waliitaka Serikali kuwaacha wajinunulie
mashine yao kokote wanakojua na mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)wawauzie kadi (line)
kama ilivyo kwa upande wa simu za kiganjani.
“Tunaomba
serikali iwache wafanyabiashara wanunue mashine za EFD wenyewe halafu TRA
wawauzie line kama ilivyo kwenye simu, na si kuwalazimisha wafanyabiashara
wanunue mashine hizo ambazo bei yake ni ghali”alisema Remigius maafuru mjini
hapa kwa jina la Dkt. Remmy.
Hata hivyo,
kwa upande wa Naibu Waziri, Malima akizungumzia juu ya kodi za Jeshi la Zima
moto, alisema wao wana ‘theory’ yake ambayo wao wameiweka lakini hata wao
katika baraza la Mawaziri wamekuwa wakihoji hilo ambapo hata hivyo utoaji
huduma zao kwa jamii iko tofauti na majeshi mengingine.
Alisema”Nawambieni
wazi hili la asuala la Jeshi la ZimaMoto hata sisi kwenye baraza la Mawaziri
tulihoji, hii kodi ni ya nini? Inakwenda
wapi? Mpaka sasa hata bado tunasubiri majibu lakini kaeni mkijua kuwa kila
Jeshi lina utaratibu wake”
Alisema hata
yeye binafsi suala hilo la zimamoto linamsumbua, kwani hajui tozo hizo ni kwa ajili ya nini kwani hata kwa wakulima,
wafanyabishara wadogo na wa wakati wote wanalalamikia hilo tozo.
Hata hivyo,
Naibu huyo aligeuka kuwa mbogo baada ya Remigius kutoa pendekezo la serikali
kuondoa tozo za kusafirisha fedha nje ya nchi pindi mfanyabiashara kwenda kununua bidhaa nje ya
nchi kwani ni miongoni mwa sababu ya bidhaa kupanda bei na hivyo kumuumiza
mlaji.
Alisema
kamwe haiwezekani na wala serikali haiweze kuondoa tozo hilo na wasije
wakafikiria kuwa iko siku serikali itaondoa tozo hiyo.
“Hivi kuna
nchi yoyote ambayo inasafisha fedha zake kwenda nchi nyingine bila kutoza ushuru,
haiwezekani”alisema.
Awali Kamishina wa TRA Taifa,Patrick Kasera akizungumzia umuhimu wa mashine ya EFD
alisema kuwa ni kumwezesha mfanyabiashara kutunza kumbukumbu za mauzo na
biashara zake, ambapo asilimia kubwa ya wafanyabiashara wengi ambao hawasimamii
katika biashara zao wamekuwa wakiibiwa pasipokujua ni kiasi gani wanachoibiwa.
Halikadhalika
alisema tatizo kubwa kwa Watanzania ni kumbu kumbu ambapo hasara yake ni kukadiriwa kipato chake kutokana na biashara yake na matokeo yake huona kuwa anaonewa na TRA
bila kuwa na uthibitisho.
Alisema
“Kazi ya mashine hizo ni kutunza kumbukumbu vizuri na kukuwezesha kulipa kodi
stahili na anayeona anaonewa hata ona hilo tena, kwani watu wengine
wanafilisika bila kujua kama wao wenyewe hawasimamii biashara zao, lakini kwa
kupitia TFD huweza kubaini hata kama hatakuwepo kwenye biashara zake”alisema.
Alisema
mashine za EFD zinamwezesha kila mtu kulipa kodi vizuri bila kufilisika kwani atapewa makadirio
ambayo anaweza kuyamudu tofauti na hapo
aawali ambapo mtu alikadiriwa tu kodi kumbe kiasi hicho kilikuwa ni kikubwa
tofauti na uwezo wake.
Mwisho.