Na Theonestina Juma, Kagera
JESHI la polisi mkoani Kagera linapata wakati mugumu wa kupata ukweli wa
mazingira ya utekwaji wa diwani wa ( CCM ) Bw.Arnold Rwesheleka, kata ya Chonyonyo Wilayani Karagwe, na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi na kisha
gari lake kulitekekeza kwa moto katika pori la kimisi.
Akiongea na waandishi wa
habari ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoa wa Kagera Philip
Kalangi alisema mazingira ya utekwaji wa diwani huyo pamoja na
maelezo yake yanatia mashaka.
Alisema maelezo ya mlalamikaji
yanajichanganya hali hiyo imesababisha jeshi hilo kuwa na mashaka ya
mazingira ya kutekwa kwa diwani huyo (CCM) alitekwa na watu watatu
wasiojulikana wakiwa na bunduki aina ya piston ila alifanikiwa kutoroka kabla
ya kudhuruwa.
Alisema jeshi la polisi
liliopofika eneo la tukio mazingira yalionyesha kulikuwa na maandalizi
ya kuchomwa kwa gari hilo na huko alikodai kuwa ,alienda kusalimia na
alikuwa hajaenda huko takribani miezi mitano.
“Tulishazoea kukagua maeneo mengi
yanayokuwa yamefanyiwa uhalifu na matukio mbalimbali lakini mazingira, aliyoteketezwa
gari lake yana utata”alisema kamanda Kalangi.
Alisema jeshi la polisi linaendelea
na uchunguzi wa kina na tayari kamanda wa upelelezi wa makosa ya jinai
mkoa ( RCO ) Bw.Henry Mwaibambe yuko Karagwe kwa ajili ya uchunguzi wa tukio
hilo.
Alisema kutokana na utata wa
mzingira ya utekwaji huo wanatafuta kumbukumbu mbalimbali za mlalamikaji
zikiwemo za gari pamoja na bima ya gari kuangalia kama kulikuwa na
matatizo kabla ya gari hilo kuteketezwa na moto.
Na Theonestina Juma

Awali diwani huyo alidai
katika kituo cha polisi kuwa alitekwa na watu watatu wasiojulikana wakiwa na
bunduki aina ya piston ila alifanikiwa kutoroka kabla hawajamdhuru baada
ya kuwatoroka kwa kuwafungia ndani ya gari lake na kwa hasira wakateketeza gari
lake kwa moto.
Alisema Bw. Rwesheleka alipita katika kizuizi cha
polisi cha Chanyamisa majira ya saa 11.jioni akisema kuwa anaelekea katika
kijiji cha Nyakasimbi kumuona bibi yake ambaye alidai kuwa ni mgonjwa.
Alisema kuwa majira ya saa mbili za
usiku ambapo diwani akiwa safarini kurudi Chonyonyo alikutana na mtu mmoja
ambaye alimsimamisha na kisha kumtisha kwa kumuonyesha silaha, akamwamuru
diwani huyo kugeuza gari na kurudi barabara ya Benako ambapo diwani huyo
alilazimika kufuata maagizo hayo.
Alisema wakati diwani akiendelea na
safari kuelekea aliko elekezwa mbele kidogo walikutana na watu wengine wawili
ambapo huyo mwenye silaha aliyekuwa ndani ya gari alimwamuru asimamishe gari
ndipo watu hao walianza kupakiza mizigo ndani ya gari.
Alisema kutokana na maelezo ya
diwani huyo kuwa wakati watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiendelea
kupakiza mizigo ndani ya gari, diwani alifanikiwa kutoroka na kutokomea porini
ambapo alikimbia kisha akifanikiwa kuingia katika barabara iendayo
Karagwe ndipo ghafla likatokea gari aina ya Hiace lililokuwa likitokea
Benako kwenda karagwe na kumpa msaada.
Alisema kuwa wakati diwani huyo
akiwa ndani ya Hiace aliambiwa na wasafiri kuwa wameona gari lake likiwaka moto
katika maeneo ya Nyakasimbi ambapo majira ya saa 3.30 usiku Bw.Rwesheleka
alifika katika kituo kidogo cha polisi Chanyamisa na kutoa taarifa kuwa katekwa
na majambazi.
Alisema baada ya kutoa taarifa polisi
waliondoka na diwani huyo mpaka eneo la tukio na kukuta gari hilo likiendelea
kuteketea kwa moto,kamanda aliongeza kuwa polisi wanaendeleana uchunguzi zaidi
juu ya tukio hilo kwani mazingira yake yanatatanisha na wataendelea kutoa
taarifa zaidi pindi watakapo wakamata wahusika.
tika maeneo ya Nyakasimbi ambapo majira ya saa 3.30 usiku Bw.Rwesheleka
alifika katika kituo kidogo cha polisi Chanyamisa na kutoa taarifa kuwa katekwa
na majambazi.
Alisema baada ya kutoa taarifa polisi
waliondoka na diwani huyo mpaka eneo la tukio na kukuta gari hilo likiendelea
kuteketea kwa moto,kamanda aliongeza kuwa polisi wanaendeleana uchunguzi zaidi
juu ya tukio hilo kwani mazingira yake yanatatanisha na wataendelea kutoa
taarifa zaidi pindi watakapo wakamata wahusika.
No comments:
Post a Comment