Na Theonestina Juma
WATU saba wamefariki dunia papo hapo Wilayani Ngara, baada ya gari waliokuwa wamepanda
kutoka Ngara kwenda Kahama mkoani Shinyanga kugongana uso kwa uso na lori
lililokuwa limebaba mchanga katika eneo la ziro ziro, Benako njia ya kwenda Kahama
.
Akizungumza na gazeti hili jana ( leo) jioni Mkuu wa wilaya ya Ngara,
Costantine Kanyasu amesema ajali hiyo limetokea jana saa 6.00 mchana katike eneo la Ziro Ziro Benako
barabara kuu ya kutoka wilaya ya Biharamulo kwenda Rwanda.
Alisema katika ajali hiyo, kati ya watu hao saba waliopoteza
maisha papo hapo, wanawake ni wanne na wanaume ni watatu akiwemo na mtoto mchanga
anae kadiriwa kuwa na wiki moja ambapo jinsi yake bado haijatabuliwa.
Bw.Kanyasu alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva aliyekuwa
akiendesha gari la abiria aina ya hiace lenye namba ya usajili T 527 CLA ambaye alikuwa mwendo kasi ambapo hakuchukua
tahadhari alipofika katika eneo hilo la kona.
Katika ajali hiyo, dereva na tingo wa hiace hiyo ni miongoni
mwa abiria walipofariki dunia papo hapo.ambapo miili yao yamehifadhiwa katika
hospitali ya Omurugwanza wakisubiri kutambuliwa na ndugu zao.
Alisema katika ajali hiyo watu 10 wamejeruhiwa vibaya ambapo baadhi yao wamekimbizwa katika hospitali
ya Teule ya wilaya ya Omurugwanza huku
wengine nao wakilazwa katika hospitali ya Nyamiaga wilayani humo.
Mkuu huyo amewataka madereva kuwa makini wakati wakiwa
wamebeba abiria kwani wanakuwa wamebeba roho za watu hasa nyakati hizi za
sikukuu.
Hata hivyo, habari zaidi kutoka eneo la tukio zinadai kuwa hiace
hiyo ilikuwa imebabi wahamiaji haramu ambapo hata hivyo kwa upande wa mkuu wa
wilaya hiyo, amesema kuwa si kweli kwani ni abiria wa kawaida tena wa raia wa
Tanzania.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment