Na Theonestina Juma
HALMASHAURI kuu ya chama cha
mapinduzi (CCM)mkoa wa Kagera,imewafukuza madiwani wake nane katika halmashauri ya Manispaa ya Bukoba
kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kupuuza
ushauri uliotolewa na Mwenyekiti wa CCM taifa Rais Jakaya
Kikwete.
Akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari kwa niaba ya halmashauri kuu ya CCM mkoa, Katibu Mkuu wa chama hicho
mkoa wa Kagera, Bw. Avelin Mushi,alisema kuwa uhamuzi huo umekuja kutokana na
chama kujali maslahi ya wananchi tofauti ya watu binafsi.
Mushi amewataja madiwani hao nane
kuwa ni pamoja na Bw.Yusuph Ngaiza,kata Kashai ambaye pia ni Mwenyekiti
wa ccm wilaya Bukoba, Bw.Samwel Ruangisa(Kitendaguro) meya mstaafu na mkuu wa
mkoa wa mkoa wa kwanza wa mkoa wa Kagera.
Wengine ni Bi.Murungi Kichwabuta(Viti maalumu) Bw.Deusdedith
Mutakyawa(Nyanga) Bw.Richard Gaspar(Miembeni), Bw.Alexander Ngalinda(Buhembe) ambaye
pia alikuwa Naibu meya Bw.Dauda
Kalumuna(Ijuganyondo)na Bw.Robert
Katunzi wa kata Hamugembe.
Bw.Mushi alisema kuwa kufukuzwa kwa madiwani hao ni
kutokana na mgogoro ulidumu kwa muda mrefu juu ya mbunge na meya ambavyo Rais
Kikwete akiwa ziarani Kagera alitoa agizo la wanachama hao kupatakana kwani hakuna
vita visivyokuwa na mwisho wake.
Pia, alisema kuwa vikao vya chama
vimekuwa vikiendelea kwa kufuata kanuni na taratibu kwa kuwaonya juu ya
kuhujumu serikali ya CCM kwa kushirikiana na madiwani kambi ya upinzani
kutotekeleza maendeleo ya wananchi lakini wahusika wote wamekuwa wakikahidi
maagizo ya kuitwa kwenye vikao.
No comments:
Post a Comment