Na
Theonestina Juma
DIWANI wa
kata ya Chonyonyo [CCM] wilayani Karagwe, Bw.Arnold Rweshekerwa amenusurika
kuuawa na kundi la majambazi waliomteka nyara katika eneo la Kyanyamisa kabla
ya kuwatoroka akiwa amewafungia ndani ya
gari lake kati kati ya pori la Kimisi usiku.
Kwa mujibu
wa habari zilizopatikana mjini hapa na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa
Mkoa wa Kagera, Phillip Kalangi, tukio hilo la aina yake limetokea Agosti 10
mwaka huu saa 2.00 katika eneo lenye kibao kinachoonesha sehemu ya hifadhi ya
akiba katika pori la Kimisi kuelekea wilayani Ngara.
Hata hivyo,
baada ya kunusurika kuuawa na majambazi hayo, wameteketekeza gari la diwani
huyo kwa kitu kinachokisiwa kuwa ni bomu, ambapo diwani huyo alipoteza maisha
takriba saa mbili baada ya kusikia taarifa ya gari lake kuteketezwa kwa moto.
Habari hizo
zinaeleza kuwa, Diwani huyo alikuwa ameenda kijiji cha Kyanyamisa kumtembelea
bibi yake mzaa mama, ambapo wakati akirudi nyumbani kwake kata ya Chonyonyo,
alikutana na watu wawili njiani, wakiwa na piston ambapo walimtishia nayo na kumtaka ageuze gari kurudi alikotoka.
Katika
harakati za kugeuza gari hilo, huku watu hao wakiwa wamepanda ndani ya gari
lake hilo ambalo halijajulikana aina
wala namba yake, hatua kama tano hivi alikutana na watu wengine tena.
Alisema watu
walikuwa na mifuko minne yaliojaa bunduki, magazine na risasi, ambapo akiwa
anawaendesha kwenye gari lake, watu hao walikuwa wakifanya kazi ya kuingiza
risasi kweye magazine walizokuwa nazo.
Hali
kadhalika watu hao walipofika karib u na kibao hicho chenye maandishi ya
hifadhi ya akiba walimwamuru diwani huyo kuzima taa ya gari lake na hivyo watu
hao waliendelea na kazi kuingiza risasi hizo kwenye magazine kwa kutumia tochi
walizokuwa nazo.
Katika
maelezo hayo yanaeleza kuwa, wakiwa kati kati ya pori la kimisi majambazi hayo
walimwamuru Diwani huyo kusimamisha gari lake, kwa muda ambapo muda huo aliweza
kuwaangalia mawazo yao yalikokuwa kwa wakati
huo, alilazimika kufunga [Lock} milango
yote na kisha kuruka kwenye dirisha la dereva na kutokomea porini.
“Diwani
aliwafungia wale majambazi ndani ya gari lake, na kurukia kwenye dirisha la
dereva, na hivyo hawakuwa na namna ya kuondoka ndani ya gari na inasemekama
hunda baada ya kutoka ndani ya gari wameliteketekeza kwa bomu”alisema mmoja wa
chanzo .
Habari hizo
zinasema kuwa, Diwani huyo alitembea zaidi ya kilomita mbili akirudi Karagwe,
ambapo aliona pikipiki moja ikiwa na watu wawili wenye silaha wakitokea
Kyanyamisa kuelekea Ngara ambapo alishindwa kuwasimamisha kwani alihofia huenda
wakawa ni wenzao, kutokana na alipokuwa nao aliwasikia wakiwasiliana na watu
wengine.
Hata hivyo,
aliendelea kutembea ambapo aliiona hiace
moja ikitokea mji mdogo wa benako wilayani Ngara saa 3.30 usiku, ambapo
aliwasimimamisha na kisha kumpakia, na aliwaeleza
kisa chote na watu hao kumuelezea juu ya kuona gari likitekea kwa moto kati
kati ya pori.
Watu hao
wanadaiwa kuwa Kiswahili chao ni kama cha wanaotoka nchi jirani, ambapo hadi
hivi sasa, polisi wanaendelea a uchunguzi wao juu ya tukio hilo, kutokana na
diwani huyo alikuwa peke yake kwenye gari hilo hivyo wanashindwa kumuulizia
nani.
“tukio hilo
lipo, na gari limetekezwa kweli kati
kati ya pori lakini suala la utekaji wa diwani huyo, inakuwa ngumu
kuthibitishwa kwani wakati wa tukio hilo likitokea, alikuwa peke yake kwenye
gari hilo, na huenda kuna mambo mengine
yaliojificha ”alisema kamanda Kalangi.
Katika
tukio, watu hao hawakuweza kumdhuru diwani huyo licha ya kumpora simu yake ya
mkononi, sh.100,0000 na viatu vyake alivyokuwa amevaa kwa wakati huo.
Diwani huyo
amelazwa katika hospitali teule ye
Nyakahanga baada ya kupoteza fahamu.
Hatua ya
utekeaji wa diwani huyo imekuja saa kadhaa baada ya Agosti 10 ikiwa ndiyo siku
ya mwisho ya agizo la, Rais Jakaya Kikwete ya kuwataka majambazi na wanaomiliki
silaha kinyume cha sheria kujisalimisha na kusalimisha silaha zao.
Halikadhalika na wahamiaji haramu kuondoka nchini kabla ya
operesheni kubwa kuendeshwa katika mikoa
mitatu ya Geita, Kagera na kigoma kwa kushirikisha majeshi yote ya usalama nchini.
Hadi juzi
silaha 19 zimesalishwa katika wilaya za Karagwe, Ngara, Biharamulo na wahamiaji
haramu 2000 wameondoka nchini kwa njia inayojulikana na kwa wale ambao
wamepitia njia za vichochoroni idadi yao haijajulikana.
Tangu Rais
kikwete atangaze kuendeshwa kwa operesheni hiyo, hali ya utekaji ulikuwa
umetulia katika pori hilo ambapo magari ya abiria yalikuwa yakisafiri katika
pori hilo hata saa 4. Usiku tofauti na hapo awali.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment