MAKAMU wa
Askofu waKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba, Dkt. Methodius Kilaini amewataka
waumini kanisa Katoliki Mkoa Kagera kushiriki kikamilifu katika wiki ya sherehe
ya Muadhama Laurean Kadinali Rugambwa anayetarajiwa kuzikwa masalia yake rasmi
Oktoba 6, mwaka huu katika kanisa kuu la Jimbo la Bukoba.
Rai hiyo
imetolewa leo na Askofu Dkt.Kilaini wakati akihubiri katika misa ya pili
iliofanyika katika la kanisa la Rumuli ikiwa ni kuanza kwa wiki ya maadhimisho
ya Kadinali Rugambwa.
Askofu
Kilaini alisema kwa kumuenzi zaidi matendo ya Kadinali huyo, mweusi wa kwanza
Mwafrika, waumini wanapaswa kushiriki katika sherehe zake zilizoanza
kuadhimishwa katika Jimboni humo Septemba 30, mwaka huu ambapo kilele cha
maadhimisho hayo yatakuwa Oktoba 7, mwaka huu.
Alisema
katika sherehe hizo za kuhamisha masalia ya Kadinali Rugambwa Oktoba 6,
shughuli hizo zitaanza asubuhi katika parokia ya Kashozi alikozikwa kwa muda
ambapo yatafanyika maandamano kutoka katika parokia hiyo hadi kanisa kuu la
Bukoba mjini.
Alisema shughuli
za kuzika rasmi masalia yake yatafanyika kuanzia saa 9.00 alasiri ndani ya
kanisa kuu ambalo alitaka akizikwe ambapo kanisa hilo tayari limeshakamika kukarabatiwa.
Akielezea kwa wiki nzima shughuli zitazofanyika, alisema
kuwa ni pamoja na kusomwa misa katika kijiji alikozwaliwa cha Rutabo,
alikobaziwa parokia ya Kagondo na Rutabo
alikojenga seminari ,Bunena mjini Bukoba na kisha Kashozi ambako siku anatangazwa kuwa
Askofu alikuwa akifanya shughuli za kiuchungaji katika parokia yote hayo ni
kuadhimisha kumbu kumbu yake.
Alisema enzi
za uhai wa kadinali Rugambwa alikuwa kiungo wa Waafrika, maaskofu wa kiafrika
na waumini nje ya nchi hadi ikafikia hatua wazungu wakaanza kuwapa waafrika
nafasi za uongozi.
“Kadinali
Rugambwa alikuwa kama bendera iliowekwa juu ya milingoti ili kila mtu aione,
hii ni kutokana na yeye aliweza kukaa na wazungu katika kiti kimoja kujadili
mambo mbali mbali yahusuyo jamii na dini, hivyo yeye alikuwa kama kiungo”alisema
askofuKilaini.
Alisema
katika Tanzania Kadinali Rugambwa ni muasisi wa Baraza la maaskofu na alikuwa
mchungaji mwema kutokana na kuwapenda waumini, watawa na mapadri wake.
Halidhalika
alikuwa mpenda maendeleo, ambapo katika enzi za uhai wake aliweza kuanzisha
miradi mbali mbali za kanisa kama ujenzi wa shule za sekondari, hospitali na
vtuo vya afya ambapo alikubalika kwa dini zote kulingana na maelezo ya watu
mbali mbali waliokuwa naye karibu.
Ukiona tangazo kama hili limetundikwa juu ujue mambo yameiva, ni kweli Oktoba 6, hiyoooo, masalia ya Kadinali Rugambwa kuhamishwa na kuzikwa rasmi.
Hii sehemu ya barabara ya Jamuhuri karibu na Kanisa kuu Jimbo la Bukoba likiwa katika ukarabati kwa ajili ya sherehe ya kuhamisha masalia ya Kadinali Rugambwa.
Hii ni barabara ya Kashozi inayoelekea katika parokia ya Kashozi alikozimwa kwa muda Kadinali Rugambwa ambapo masalia yake yatapitishwa wakati akienda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele.
Hii sehemu ya jengo la kanisa kuu Katoliki la Jimbo la Bukoba linavyoonekana kwa upande wa kushoto.
Sehemu ya kasani kuu Jimbo la Bukoba ambamo atazikwa rasmi Kadinali wa kwanza Mwesi Mwafrika Kadinali Laurean Rugambwa anakotarajiwa kupimzishwa milele hapo Oktoba 6, mwaka huu linavyoonekana kwa mbele licha ya kuwa bado mafundi wanasawazisha maeneo yaliobaki.
Hivi ndivyo kanisa hilo linavyoonekana.
Sehemu hii ya geti la lango kuu la kanisa hilo, ambalo masalia ya Kadinali Rugambwa unatarijia kupitishwa wakati akingizwa kanisani humo tayari kwa kuhifadhiwa milele.
Hii ni barabara ya Jamhuri ambayo masalia ya mwili wa Kadinali Rugambwa utapitishwa wakati wa kuingizwa katika ikulu yake ya milele(PICHA ZOTE NA THEONESTINA JUMA)
MWANAMKE mmoja makazi wa kijiji cha Buhororo wilayani Ngara,
amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani kwa madai yakila mara alikuwa akipata ujumbe kutokana na
watu kama majini yaliokumtaka ajinyonge.
Kwa mujibu wa habari
zilizopatikana kutoka wilayani Ngara na kuthibitishwa na Kaimu Mtendaji wa kijiji hicho, Bw. Paul Bwinyo tukio
hilo la aina yake lilitokea Septemba 26, mwaka huu kijijini hapo.
Mwanamke aliamua kujitia kitanzi amejulikana kuwa Bi.Christina
Zemitembe (37) na kwamba alijinyonga nyumbani kwao alikokuwa akiishi na mama
yake mzazi Bi.Zemitembe (70).
Alisema siku ya tukio, mwanamake huyo aliamuaka asubuhi na
kupanda juu ya meza na kisha kujitia kitanzi, ambapo kwa wakati huo mama yake
mzazi alikuwa ameenda shambani.
Imeelezwa kuwa muda wa saa saba mama yake aliporejea kutoka
shambani alikuta mlango wa nyumba yake ukiwa umefungwa kwa ndani jambo ambalo
lilimlazimu kuomba msaada kwa majirani.
Alisema majirani hao walilazimika kuharibu mlango ambapo
walipoingia ndani hawakuweza kuamini kilichotokea, kwani tayarimwanamke huyo alishajitia kitanzi na kubaki
akining’ngia juu.
Mmoja wa shuhuda wa tukio hilo aliyejitambulisha kwa jina la
Bi. Winfrida Thomas akielezea hali aliokuwa nayo mwanamke huyo kabla ya kujiua,
alisema kila mara Bi. Christina alikuwa akisema juu ya kutaka kujiua kwa
kujinyonga.
“Mwezi Aprili mwaka huu Christina alikuwa akisikika akisema kuwa amekuwa akipata
maono (ujumbe) kutoka watu kama majini ambayo yanamtaka ajinyonge.”alisema.
Hata hivyo, Bi. Thomas alisema kuwa kutokana na maneno yake
hayo walidhani kuwa alikuwa akitania na hawakujua kama kweli alikuwa
akidhamiria kutenda kitendo hicho,Jehi la Polisi Mkoani Kagera, bado
linafuatilia juu ya tukio hilo.
Yap, niko tayari kwa siku hiyo muhimu katika historia ya maisha yangu, ikizingatiwa kuwa wakati Kadinali Rugambwa akifariki dunia nilikuwa kidato cha tatu, bado kinda sasa mazishi yake rasmi mimi bonge la mama.
Changia kanisa kwa kununua sare zao rasmi ili kufanisha sherehe hizo.Hiki kitenge nilichojifunga ni moja ya aina ya sare itakayotumika siku hiyo ya Oktoba 6, mwaka huu, siku ambayo mwili wa Kadinali Rugwambwa utahamishwa kutoka katika Parokia ya Kashozi alikozikwa kwa muda na kisha kupumzishwa katika nyumba yake ya milele katika kanisa Kuu la Jimbo la Bukoba.Siku hiyo maelfu ya wageni wanatarajiwa kufurika katika Manispaa ya Bukoba.
ZIKIWA
zimebaki takriban siku 10 mwili wa aliyekuwa Kadinali wa kwanza Mwafrika,Muadhama
Laurean Rugambwa kuhamishiwa katika jengo la Kanisa katoliki mjini Bukoba,
uongozi wa kanisa hilo umetoa onyo kali kwa wafanyabiashara walioanza kunufaika
tukio hilo bila ridhaa yao.
Hatua hiyo
imekuja siku chache baada ya baadhi ya wafanyabiashara katika Manispaa ya Bukoba
kutengenezesha fulana zenye nembo ya kanisa hilo pamoja na picha ya Kadinali
Rugambwa wakiziuzwa kwa sh. 12,000 bila
ridhaa ya uongozi wa kanisa hilo.
Kutokana na
hali hiyo Katibu wa Askofu wa Jimbo la Bukoba, Padri Deodatus Rwehumbiza akizungumza
na gazeti hili jana (leo) alisema waumini watakaonunua bidhaa za
wafanyabiashara ambao zimetengenezwa bila baraka za kanisa hilo, hawatapewa
kipaumbele siku ya sherehe hiyo kama ilivyo kwa waumini watakaovaa sare
yalioandaliwa na uongozi wa kanisa hilo na watawaona kana kwamba hawajavaa sare
za sherehe hiyo.
Alisema watu
hao hawatapata mafao kama wale watakao vaa sare zao kwani bidhaa hizo
wamezitengeza kwa ajili ya kuwezesha siku ya tukio watakaohudhuria waweze kufahamika
kiurahisi na kununua sare hizo wanachangia ufanisi wa sherehe hiyo na kwamba
sare zao zinafahamika na hivyo hao ndiyo watakaopewa nafasi ya kwanza.
Alisema kwa
wale watakaokuwa na sare za kughushi na kwa kuwa wameshambulia hilo mapema na
kuwataarifu, watakaokaidi watawaona kama wale waliotoka mitaani na kuingia
katika shehere hiyo.
Hata hivyo,
gazeti hili lilipotaka kujua kwa siku hiyo hawatawathamini, Padri Rwehumbiza
alisema kuwa watawathamani, lakini kupata hudhuma kama wale watakaovaa sare
zao, haitakuwa rahisi mfano kama sehemu za kukaa zitakazoandaliwa.
Katibu hiyo
alitoa kauli hiyo, baada ya gazeti hili kutaka kujua, iwapo waumini wao watakuja kanisani siku hiyo wakiwa wamevaa
mavazi yaliotengenezwa na wafanyabiashara bila ridhaa ya uongozi wa kanisa
hilo, watafanyaje.
Alisema
kutokana na kuwa makini katika maandalizi ya sherehe ya Agosti 6na 7,ya kuhamisha mwili wa Kadinali Rugambwa
kutoka katika kanisa ya Kashozi alikozikwa kwa muda, tayari walishabaini ujanja
wa baadhi ya wafanyabiashara hao na wamekuwa wakiwataarifu waumini wao juu ya
jambo hilo.
Alisema
mmoja wa mfanyabiashara wa mjini hapa ambaye hakuwa tayari kumtaja jina lake,
walifika katika duka lake na kukuta fulana ambazo zilitengenezwa rasmi
kuhusiana na siku ya tukio hilo.
“Tulifika katika
mmoja ya duka mjini Bukobana kukuta
fulana zinazohusiana na sherehe ya kuhamisha mwili wa Kadinali Rugambwa,… na
kubariki kanisa kuu….tulijifanya kama wanunuzi, tulinunua sh.12,000 na kukatiwa
risiti”alisema
Alisema
kutokana na hali hiyo tayari walishatoa taarifa kituo cha polisi kuhusiana na
tukio hilo, ambapo katika mahojiano zaidi mfanyabiashara huyo alisema kuwa
fulana ndizo zilikuwa bidhaa za kwanza kuingizwa sokoni ambapo walikuwa na
mpango wa kuteneza vitambaa.
Hata hivyo,
Padri Rwehumbiza alipotakiwa na gazeti hili kueleza kama fulana hizo
zimetengezwa mjini Bukoba au nje ya mjini hapa alisema kuwa haijajulikana
fulana hizo zimetengenezwa wapi, wala haijajulikana wako wafanyabiashara
wangapi, zaidi hilo sasa ni jukumu la polisi kufuatilia.
Kuhusiana na
hatua walikofikia ya maandilizi ya sherehe hizo, Katibu huyo alisema kuwa
yanaendelea vizuri na kwamba yatafanyika jinsi yalivyo pangwa na kwamba zaidi
ya wageni 5000 kutoka ndani na nje ya nchi wanatarajiwa kuhudhuria.
Kuhusiana na
viongozi wa kitaifa alisema kuwa mialiko
wametuma kwa woteambapo majibu
yanayopatikana hayaoneshi kukatisha tamaa.
Septemba 23,
mwaka huu katika kanisa katoliki la Rumuli yalisikika matangazo ya kanisa hilo
yakieleza juu ya kuwepo kwa baadhi ya wafanyabiashara waliotengeneza fulana na
vitenge yenye maandishi kuhusiana na matukio ya sherehe hizo, bila idhini ya
kanisa hilo.
Katika
matangazo hayo yalieleza kuwa fulana hizo zina maandishi kwa nyuma, ambapo hata
bei zao hawajaafikiana nao na uongozi wa kanisa.
Sare
zinazouzwa na kanisa hilo katika maduka yake mjini hapa, fulana na vitenge vinauzwa
sh. 13,000 ambapo fulana za wafanyabiashara binafsi zinauzwa sh. 12,000.
Mwili wa Mwadhamu Kadinali Rugambwa unatarajiwa kuhamishwa rasmi Oktoba 6,saa 9.00 alasiri
mwaka huu ukitokea katika parokia ya Kashozi alikokuwa amezikwa kwa muda kupekelekwa katika Kanisa kuu la Jimbo
hilo lililochukua zaidi ya miaka 10 kukamilika kwa ukarabati wake.
Aidha Oktoba 7, mwaka kutafanyika sherehe
nyingine ya kubarikiwa kwa kanisa hilo na kumbukumbu ya miaka 100 ya
kuzaliwa kwa kadinali huyo wa kwanza Mwafrika.
Muadhama Kadinali Rugambwa
alizaliwa Julai 12, 1912 katika
kijiji cha Bukongo Rutabo Kamachumu wilayani Muleba katika familia ya
kifalme na kufariki dunia mwaka 1997.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe hatimaye ametatua mgogoro wa shule ya
sekondari ya Wasichana ya Ruth Msafiri kati ya Wananchi na aliyekuwa Mbunge wa
jimbo la Muleba Kaskazini Ruth Blasio Msafiri kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi
2010.
Mhe. Massawe alikabidhi
shule hiyo kwa Wananchi wa Kata ya Katoke jana tarehe 17/09/2012 ili waendeleze
ujenzi baada ya kuwa na mgogoro zaidi ya miaka miwili kati ya Wananchi na aliyekuwa
mbunge wao 2005 hadi 2010 kwa kudai shule hiyo ni mali yake binafsi baada ya
kuwa ameshindwa ubunge mwaka 2010.
Shule hiyo ya Sekondari ya
Wasichana ya Ruth Msafiri iliyoko katika kitongoji cha Kimbugu, Kijiji Katoke
Tarafa Izigo Halmashauri ya Wilaya Muleba ilianzishwa na Ruth Blasio Msafiri
wakati huo akiwa Mbuge wa Jimbo la Muleba Kaskazini mwaka2009.
Kulingana na taarifa
mbalimbali kutoka kwa wananchi na seriklai ya kijiji Katoke Ruth Msafiri alitoa
wazo la kuanzisha shule ya wasichana na kuomba ardhi katika serikali ya kijiji
na kupewa Ekari 40 za ardhi kwa kuwa walikubaliana shule hiyo iwe ya wananchi
wa Kata ya Katoke.
Pia wananchi walikubaliana
shule hiyo iitwe kwa jina la Ruth Msafiri baada ya kuwa yeye ndiye aliyeanzisha
wazo la kuwa na shule ya wasichana katika kata hiyo. Vilevile Bi Ruth Msafiri
alianza kuomba michango kwa niaba ya wananchiili kuanzisha ujenzi wa shule hiyo mwaka 2009.
Wananchi walichangia nguvu
zao pia mfuko wa jimbo ulichangia Shilingi 3,000,000/=, Benki ya NMB ilichangia
shilingi 5,000,000/= Wizara ya Maliasili na Utalii shilingi 6,000,000/=, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kikwete alichangia mabati 300 na ndipo
ujenzi wa shule hiyo ulianza.
Baada ya uchaguzi Mkuu 2010
Ruth Msafiri hakubahatika kuchaguliwa tena kuliwakilisha jimbo la Muleba
Kaskazini na ndipo mgogoro ulianza na akadai kuwa shule ni mali yake jambo
ambalo wananchi hawakukubaliana naye na kuanza kulalamika na malalamiko hayo
yalimfikia Mkuu wa Mkoa.
Tarehe 20/02/2012 Mkuu wa
Mkoa alitembelea kijiji cha Katoke na kufanya mkutano wa hadhara na wananchi na
alisikiliza mgogoro huo kwa undani na akaagiza wananchi wapitie kwenye ngazi
husika za kisheria kuanzia ngazi ya kijiji Balaza la Kata na Balaza la Madiwani
la Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ili kulidhia kuwa shule hiyo ni mali ya wananchi.
Aidha baada ya hatua zote
Mkuu wa Mkoa alizoagiza kufuatwa nay eye
kuridhia jana tarehe 17/9/2012 Mhe. Massawe aliikabidhi shule hiyo kwa wananchi
ili kuendeleza ujenzi kwaajili ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2013.
Kutokana na furaha ya kukabidhiwa
shule yao wananchi wakiongozwa na Mhe. Massawe na Mkuu wa Wilaya ya Muleba
walianza kuchangia ujenzi wa shule hiyo kwa kutoa fedha taslim, ahadi na zaidi
ya shilingi 1,800,000/= zilichangwa pia mawe, mchanga, sementi, misumari na
mbao vilihaidiwa kuchangiwa na wananchi hao.
Shule hiyo ina jengo la
utawala pia na vyumba viwili vilivyo pauliwa tayari, na msingi wa vyumba vitatu
ambavyo havijakamilika. Wananchi walimhaidi Mkuu wa Mkoa kufikia mwezi Oktoba
2012 majengo hayo tayari yatakuwa yamekamilika kwa ajili ya Januari mwakani.