Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Sunday, October 14, 2012
Mwandishi wa NIPASHE Iringa afariki dunia
Saturday, October 13, 2012
RPC Mwanza, Liberatus Barlow auawa na majambazi usiku wa manane
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Liberatus Barlow ameuawa na majambazi usiku wa kuamuakia leo katika maeneo ya Kitangiri Jijini Mwanza.
Habari zilizopatikana kutoka jijini humo na kuthibitishwa na IGP Said Mwema zinasema kuwa Kamanda Barlow aliuawa na majambazi wakati akitoka kumsindikiza dada yake baada ya kuhudhuria kikao cha harusi.
Hata hivyo habari zaidi zinasema kuwa tayari mwalimu mmoja aliyejulikana kwa jina la Doroth anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo kwa ajili ya kulisaidia katika uchunguzi wa watu waliomuua kamanda huyo kwa kummiminia risasi .
Mwalimu Doroth ndiye inasemekana kuwa alikuwa dada yake aliyetoka kumsindikiza mufa mufupi kabla ya kuuawa.
Kamanda Barlow aliuawa usiku saa tisa.
Friday, October 12, 2012
Kagera watangaza unyanjano wa migomba janga la mkoa, miche zaidi ya mil.1 yaathiriwa ,hupata hasara ya sh. bil.16 kila mwaka
Na Mwandishi wetu, Bukoba
UGONJWA wa
migomba ya unyanjano umeubabishia mkoa Kagera hasara ya sh. bilioni 16 kila
mwaka, imeelezwa.
Kutokana na
hali hiyo mkoa Kagera umetangaza ugonjwa huo unaoshambulia migomba kuwa ni janga la
mkoa.
Hatua hiyo
ilifikiwa jana na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa Kagera kilichofanyika
jana mjini hapa na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali kutoka taasisi binafsi na serikali.
Wajumbe hao
walisema kutokana na hasara kubwa ambayo wakulima wa mkoa huo wameshaupata na
wanaendelea kuupata kutokana na ugonjwa
wa unyanjano wa migomba umeathiri uchumi wa mkoa huo.
Akitoa taarifa ya kuenea kwa ugonjwa huo wa unyanjano
, Mshauri wa kilimo mkoani hapa, Bw. Diyonysius Mabugo alisema kutokana na
ugonjwa huo umesababisha uzalishaji kushuka kwa asilimika 10 hadi 17 jambo
ambalo linahitaji mikakati ya kuudhibiti ikiwa ni pamoja na kutangaza gonjwa
hilo kama janga la mkoa.
Bw.Mabugo
alisema mavuno ya ndizi umepungua kwa asilimia tatu na uuzaji wa zao hilo pia
umepungua kwa asilimia 35 jambo ambalo linahitaji mikakati kabambe ya kupambana
nalo.
Alisema
kutokana na hali hiyo hata ulaji wa ndizi umepungua kwa silimia 25 huku bei
yake ikipanda zaidi hadi asilimia 46 na kusababisha kaya nyingi kupata mlo mmoja
kuongezeka hadi asilimia 15 ambapo upungufu wa chakula umetoka asilimia 14 mwaka
2006 hadi 64 kwa mwaka huu.
Akielezea
ufahamu wa ugonjwa huo kwa wakazi wa mkoani Kagera ambao uliweza kuonekana kwa
mara ya kwanza kwa wakulima wa kijiji cha Kabale tarafa ya Izigo wilayani Muleba
Septemba 2005 na kuthibitishwa na wataalam kuwa ni unyanjano Januari 2006 ni
asilimia 97.
Alisema pamoja na utafiti kuonesha kuwa ni
asilimia 93 ya wanakagera wanaufahamu wa ugonjwa huo Uganda wakiwa ni asilimia 74
na Rwanda asilimia 61 lakini katika utumiaji wa kanuni bora za kuudhibiti ugonjwa wa
Unyanjano Tanzania mkoani Kagera ni asilimia 13,Uganda asilimia 55 na Rwanda ni
asilimia 47.
Alisema changamoto inatokana na kutokuwepo kwa mpango
kazi madhubuti wa kupambana na mnyauko bacteria (BXW).
Pia Wakulima hawamilikishwi katika kuandaa
mipango ya kudhibiti BXW na mipango ya kudhibiti BXW si endelevu.
Halikadhalika wakulima ambao mashamba yao
hayajashambuliwa hawashituki na siasa mufilisi za kugeuza BXW kuwa mtaji
wa kisiasa.
Alisema hadi Juni mwaka huu ugonjwa huo
umeshaathiri jumla ya kaya 56,520 katika vijiji 389 kwenye kata 110.
Pia ugonjwa huo umeathiri jumla ya miche 1,131,192
kwa mwaka huu na mwaka 2011 uliathiri miche ya migomba 596,034
Hata hivyo, Mkuu wa mkoa Kagera Kanali Fabian
Massawe alisema kwa sasa ungonjwa huo ni janga la mkoa ambapo wanasubiri
serikali nayo iweze kulitangaza kama janga la taifa, kwani tayari
wameshawasiliana na waziri wa Chakula, kilimo na Ushirika, Mhandisi Christopher
Chiiza aliyekuwa mkoani hapa.
Mwisho.
Tuesday, October 9, 2012
Chiiza, Mkaguzi anakwenda kumkagua shemeji yake kweli anaweza kutoa taarifa iliokamili ya ubadhilifu?
Waziri wa Chakula, kilimo na Ushirika, Mhandisi Christopher Chiiza pamoja na Bi.Restuta wakiwa katika mkutano na bodi ya KCU 1990
Mjumbe wa bodi wa KCU, Bw. Shadrack Babu akizungumza katika mkutano huo

Mwanafunzi wa kidato IV azuiliwa kufanya Mitihani Bukoba kisa ana mimba ya miezi 9,anatarajiwa kujifungua muda wowote
Na Theonestina Juma,
Bukoba
MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Bukoba, aliyetakiwa kuanza kufanya mtihani wake wa mwisho jana, amezuiliwa kufanya mtihani huo, kutokana na kuwa na mimba ya miezi tisa.
Mwanafunzi huyo aliyejulikana kwa jina la Agnes Vedasto (16-18) mwenye namba ya mtihani S.0304/0003 amekumbwa na tatizo hilo baada ya jana kuwasili shuleni hapo kwa lengo la kutaka kufanya mitihani hiyo.
Hata hivyo, kabla ya kuingia darasa kuanza kufanya mtihani huo, aliingia Afisa elimu Taalum, Bi. Christina Shadrack na Afisa elimu Vifaa na takwimu wa Manispaa ya Bukoba, Bw. Wandele Pamba wakiwa wanasambaza vifaa vya mtihani kutokana na shule hiyo ndicho kilikuwa kituo cha mwisho, waliuzwa na Mkuu wa shule hiyo, Bw. Deus Gaspar kama mwanafunzi huyo anaweza kuruhusiwa kufanya mtihani.
Mkuu huyo wa shule hiyo Bw. Gasper alisema alilazimika kumrudisha nyumbani mwanafunzi huyo ambapo alisema kuwa miezi mitatu ya mwishoni mwanafunzi huyo alikuwa hajaonekana shuleni hapo.
Bw. Gasper alisema uongozi wa shule hiyo ulijua kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito, ambapo aliitwa mzazi akakiri kuwa mwanae ni mjamzito.
Hata hivyo, kutokana na tayari jina lake lilishapelekwa baraza la mtihani, lakini lilirudi na wanafunzi wenzake wakamtaarifu juu ya hilo na yeye kuamua kufika shuleni hapo siku ya kuanza mtihani akiwa na vifaa vya shule, amevaa sare huku tumbo likiwa limetangulia.
“ Uongozi wa shule ulijua kuwa mwanafunzi huyo ni mjamzito, na tulishamrudisha nyumbani, lakini tayari jina lake lilishaenda baraza la mtihani na limerudi… na wanafunzi wenzake wamemwambia kuwa jina lake limo kwenye orodha na hivyo naye amelazimika kuja shule kufanya mtihani”alisema mkuu wa shule hiyo.
Hata hivyo, kwa upande wa Afisa elimu wa Manispaa ya Bukoba, Simon Mwombeki alisema kwa mujibu wa sheria ya elimu namba 25 ni kosa mwanafunzi kupata ujauzito akiwa shule, kuoa wala kuolewa, hivyo mwanafunzi huyo tayari amekosa sifa.
Afisa huyo alisema, mama yake mzazi mwanafunzi huyo ambaye hakutaja jina lake, jana alifika ofisini kwake kumwomba mwanae aruhusiwe kufanya mtihani huo lakini haikuwezekana.
Alisema kulingana na maelezo ya mama mzazi wa mwanafunzi huyo, mwanae huyo anatarajiwa kujifungua kati ya tarehe 25 au 26 mwezi huu.
Jumla ya wanafunzi wanaofanya mtihani huo katika shule ya sekondari ya Bukoba ni 223 badala ya 224.

Wavuvi wavamia ziwa Victoria na majambazi waua moja na kuwapora mali zao
Na Theonestina Juma, Bukoba
MAJAMBAZI wapatao watatu waliokuwa na visu na mapanga wamewavamia wavuvi watatu na kumuua mmoja wao kikatili na kisha kuwapora mali zao zote ikiwemo samaki tani moja katika kisiwa cha Gozba ndani ya ziwa Victoria upande wa Wilaya ya Rorya.
Tukio hilo lilitokea Oktoba 3, mwaka huu saa 5 asubuhi katika kisichwa cha Gozba upande wa Wilayani Rorya Mkoani Mara ikiwa ni siku yao nne ya wakiwa kisiwani humo wakitega samaki.
Mvuvi aliyeuawa kikatili kisiwani humo, ni Bw. Godfrey Ogwanda (24) maarufu kwa jina la Yambo.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka Katika kijiji cha Bubombi wilayani Rorya, Kaka wa marehemu, Bw. Guka Ogwanda alisema kaka yake wakiwa na wavuvi wenzake wawili walivamia na majambazi hayo, ziwani wakitega samaki ambapo Bw. Ogwanda aliuuawa kwa kundungwa kisu shingoni.
Alisema kabla ya majambazi hayo hawajamuua, Bw. Ogwanda, waliwaona kama wavuvi wenzao , licha ya kuwa walikuwa hawafahamu kabisa, ambapo walileta mtumbwi wao karibu na ya kwao wakiwa hawajui lengo lao.
Alisema mmoja wa wamajambazi hao, waliwaomba kisu cha kutengenezea samaki, ambapo akina kaka yake waliwahoji, wao kama wavuvi wanawezaje kuja kisiwani kuvua sakami bila kuwa na kisu cha kutengenezea sakaki?
Hata hivyo, inadaiwa kuwa watu hao waliwapatia kisu chao walichokuwa nacho, na baadaye majambazi hayo kuwabadilikia na kuwavamia, na kuanza kuwatosa majini na kisha kuchukua mtumbwi wao na kuunganisha na wa kwao na kufunga kwa kamba.
Baada ya kitendo hicho majambazi hayo, waliwaingiza wavuvi waliowatosa majini kwenye mtumbwi wao na kuanza kuchukua mbao walizokuwa nazo ambazo huwa wanatembea nazo ndani ya mtumbwi kwa ajili ya kulalia nyakati za usiku na kuwaamuru kulala kifudi fudi na kuwafunika na mbao hizo na kuwaamwagia barafu waliazokuwa nazo juu ya mbao hizo.
Baada yakitendo hicho, walimdunga kisu Bw. Ogwanda shingoni urefu wa inchi mbili na nusu upande wa mkono wa kulia, na kuanguka chini, na wao majambazi kuanza kupakia samaki za wavuvi hao kwenye mtumbwi wao.
Alisema majambazi hayo waliwapora mafula ya dizeli lita 60 na injini ya mtumbwi wao waliokuwa nayo na kuondoka navyo ambapo Bw. Ogwanda alifia papo hapo kutokana na kuvuja damu nyingi.
Alisema kwa kawaida wavuvi kutoka katika kisiwa cha Sota Shirati, hulazimika kutembea na vyakula vyao, wakati wakisafiri kwenda kutega samaki kutokana na sehemu wanakoenda ni mbali na huwachukua siku nne hadi wiki wakitega samaki.
Halikadhalika wavuvi hao hawatembei na silaha aina yoyote kutokana na kuwepo kwa ukaguzi wanaofanyiwa mfano kama sehemu ya Migingo upande wa Uganda polisi walioko maeneo hayo huwakagua.
Aidha wavuvi hao hulazimika kutembea na kisu kwa jili ya kutengezea samaki pindi inapoonekana kutaka kuharibika, na pia hukitumia wakati wa kupika.
Hata hivyo, gazeti hili likizungumza na Kaimu Kamanda wa Kanda Maalum ya Tarime/ Rorya, Bw. Zakaria Sebastian alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kueleza kuwa hajapata taarifa kamili juu yatukio hilo kutoka katika kituo kidogo cha Polisi cha Shirati.
“Tukio hilo lipo, lakini hadi sasa bado sijapata taarifa kamili kutoka kwa mkuu wa kituo kidogo cha Shirati, na tatizo kubwa kati yao na hapa ni mawasiliano”alisema kamanda Sebastian.

Monday, October 8, 2012
Inaonekana Jeneza lililobeba masalia ya Kardinali Rugambwa lilikuwa nzito sana!
Inaonekana hili Jenela lililobeba masalia ya MwadhamaLaurean Kardinali Rugambwa lilikuwa nzito, hebu angalia inavyoonekana wanatumia nguvu kulibeba.
Baadhi ya watu walilazimika kupanda juu ya paa za nyumba na miti ili mradi tu walione jeneza lililobeba mabaki ya mwili wa Kardinali Rugambwa
Tayari fuata njia ya kuingia kansiani

Subscribe to:
Posts (Atom)