Na Theonestina Juma, Bukoba
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani
Kagera, Bi. Bernadeta Mushashu amefanikiwa kutetea nafasi yake huku, Bi. Elizabeth
Batenga aliyedumu katika nafasi hiyo takribani miaka 20 akishindwa na kijana wa
miaka 30.
Bi. Mushashu alifanikiwa kutetea
nafasi hiyo iliyokuwa ikiwaniwa na wagombea 10 katika uchaguzi wa Wabunge wa Viti Maalum uliofanyika mjini
Bukoba ambapo masimamizi Mkuu alikuwa ni Mkuu wa Mkoa Kagera, Bw.John Mongela.
Katika uchaguzi huo, Bi.
Bernadeta alipata jumla ya kura 432 kati ya kura halali 626 zilizopigwa huku
kura 11 zikiwa zimeharibika ambapo jumla ya kura zote zilizopigwa zilikuwa ni
637.
Katika uchaguzi huo uliokuwa
na mchuano mkali, nafasi ya pili ilichukuliwa na Bi. Oliver Semuguruka (30)
ambaye alikuwa na mri mdogo kuliko wagombea wote aliibuka na kura (314) akifuatiwa na Bi. Betenga aliyepata
kura (255), ambapo wote wanatoka Wilayani Ngara.
Wengine ni Bi. Janath Kayanda
ambaye ni Katibu wa CCM Mkoa Tabora alipata kura (133), akifuatiwa na Uwageni
Baragarwa (49) huku Mbunge wa zamani wa Jimbo la Muleba Kaskazini, Bi. Ruth
Msafiri akiambulia kura (20).
Wengine ni pamoja na Bi. Elizabeth
Ngaiza (9),Bi. Levina Jovin,Bi. Grace Mahumbuka na Bi. Domina Balyagati kila
mmoja akiambulia kura (7)
Nafasi ya wawakilishi kupitia
vyuo vikuu ilikuwa ikiwaniwa na watu wawili ambapo Bi. Goldliver Kaijage
aliimbuka mshindi kura ( 487) dhidi ya Martha Bishanga aliyeambulia kura (113)
jumla ya kura zote zilikuwa (517) halali zilikuwa (514) na (4) ziliharibika.
Aidha nafasi ya wawakilishi
kupitia asasi za kiraia pia iliwaniwa na watu wawili ambapo Bi. Grace Mahumbuka
alipata jumla ya kura (260) akimshinda Bi. Agnes Mkuta aliyepata kura (253).
Hata hivyo Msimamizi wa
uchaguzi huo, Bw.Mongela alisema hao wagombea waliofaulu katika hatua hiyo
ya awali wanapaswa kuongeza nguvu kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi mkubwa
ili kuwawezesha kupata nafasi ya uwakishi Bungeni.
Halikadhalika kwa upande wa
wawakilishi kupitia vyuo vikuu na asasi za kiraia wanao wanatarajiwa kuchukuana na wengine katika ngazi ya taifa.
Akizungumza katika mkutano
huo baada ya kutangazwa washindi Mbunge mkongwe wa Viti Maalum Mkoani hapa, Bi.
Batenga aliwaaga wajumbe wa mktano huo na kuwashukuru kwa kumwamini na
kumwezesha kukaa bungeni kwa pindi hicho chote.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment