Thursday, July 30, 2015

Olesendeka huwezi kuhamia dini nyingine leo na kupewa ukadinali Chadema wangekuwa wavumilivu kwa Lowassa

indexMahmoud Ahmad Arusha
………………………………………
Uvumi ulioenezwa na mitandao ya kijamii kuwa mh.Christopher Ole Sendeka anahamia chadema ameikanusha na kusema kuwa haina tija na niupotoshaji wa jamii na kuwa yeye atabakia kuwa muuumini wa chama cha Mapinduzi wala hajaona chama mbadala zaidi ya chama hicho.
Sendeka ameyasema hayo leo wakati akiongea na vyombo vya habari jijini hapa na kuwataka wanaoeneza kuacha mara moja kumuhusisha na kuhamia kwenye chama hicho kwani yeye ni muumini wa CCM.
Alisema kuwa hajaona chama mbadala zaidi ya chama cha Mapinduzi hivyo yeye ni muumini mzuri wa chama hicho na asihusishwe na kuhamia cha chochote zaidi ya kuwa mwanachama mwaminifu wa CCM.
“Chama sio gulio la kukusanya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu bali ni sehemu ya kujadili na kuondoa matabaka kati ya watawala na watawaliwa na kimbilio la wanyonge bila kujali uwezo wake kifedha”alisema Sendeka
Alisema chadema ingebaki salama kama chama hicho kingembakisha mh.Edward Lowasa kuwa mwanachama wa kawaida kwa muda na si mgombea moja kwa moja.
“Huwezi kuingia kwenye dini siku hiyo hiyo nab ado hujashika mafundisho ya dini vizuri ukapewa ukadinali na usheikh hapo hapo hilo litakuwa tatizo kubwa kwa utakaowaongoza hivyo CHADEMA ingevuta subira na kuwapa nafasi wanachama wazoefu wa chama hicho hiyo ndio demokrasia.
Akabainisha kuwa hata ukiwa na hasira leo huwezi kupambana ngumi na Tyson utajikuta umepigwa vibaya katika ulingo kwa kuwa na hasira unatakiwa utafakari na kuondoa jazba iliuweze kudhidhibiti hasira kabla hujaamua.
Sendeka alisema kuwa yeye atabaki kuwa mwanachama wa ccm na kuwa teyari ni mmoja wa wagombea wanaotaka nafasi ya ubunge kwenye jimbo la Simanjiro na kuwa anauhakika wa kushinda kwenye kura za maoni ya chama hicho.
Alisema kuwa kampeni za kumpata mgombea zinaenda vizuri ndani ya chama cha Mapinduzi bila ya kuwa na kukashifiana wala matusi hivyo anawataka wagombea kwenda na mwendo huo yatakaosaidi kuondoa makundi ndani ya chama hicho.

No comments:

Post a Comment