Monday, July 29, 2013

Rais azindua kivuko kipya Mto Ruvuvu



Na Theonestina Juma,Ngara
 RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali itaendelea kuingia gharama kuboresha na kuhumia sekta ya usafiri kwani nchi yoyote ambayo watu wake hawawezi kusafiri,uchumi wake hauwezi kukua kwa kasi.
Rais Kikwete amesema hayo jana  wakati akizindua kivuko cha mto Ruvuvu kilichoko kata ya Rusumo wilayani Ngara mpakani mwa Tanzania na Rwanda.
"Nchi ambayo watu wake hawawezi kusafiri, vyombo vya usafiri ni kidogo uchumi wake hauwezi kukua, hivyo serikali itaendelea kuboresha sekta hiyo"alisema.
Alisema kabla ya kuletwa kwa kivuko hicho wakazi wa eneo la Rusumo walikuwa wakitembea zaidi ya kilomita 50 kwa kuzunguka kupitia barabara kuu kwenda kwenda Ngara Mjini, hivyo kupatikana kwa kwa kivuko hicho ni jambo la kujivunia.
Alisema serikali itaboresha huduma ya usafiri katika sekta ya anga, majini na nchi kavu.
Kutokana na hali hiyo aliwataka wakazi wa eneo hilo kukilinda na kukitunza kivuko hicho ili kiweze kudumu.
Aliwataka wakazi wa eneo hilo kudumisha amani na utulivu ili waweze kupata maendeleo.
Naye Waziri wa Ujenzi,Dkt.John Magufuli katika  uzinduzi wa kivuko hicho alisema kivuko hicho kimenunuliwa na fedha ya serkali zaidi ya sh.bilioni 2.9.
Alisema fedha zote zilizotolewa na serikali kwa ajili ya ununuzi wa kivuko hicho ambacho kilikuwa ni ahadi ya Rais zimetumika zote.
Dkt.Magufuli alisema kivuko hicho kimewekewa waya maalum ambayo inazuia maji yakija kwa kasi hayawezi kukisomba na kukipeleka katika mto Kagera.
Alisema kwa nchi nzima hicho kuna vivuko zaidi ya  25 ambavyo vimenunuliwa kwa fedha za serikali.
Alisema katika kivuko hicho wanafunzi wanaovaa sare huvushwa bure ili baadae huenda wakawa wahandisi wa nchi hii.
Awali  Mtendaji Mkuu wa TemesaTaifa, Mhandisi Marcelline Magesa akitoa taarifa ya kivuko hicho alisema matengenezo ya kivuko hicho kimegharimu sh.bilioni 2.9 na kimetengenezwa nchini Uholanzi.
Alisema kivuko hicho kilisafirishwa vipande vipande na baade kuunganishwa hapo mto Ruvuvu.
Bi.Magesa alisema kivuko hicho kina uwezo wa kubeba magari madogo manne, abiria 50 waliokaa na waliosimama 30 kwa wakati mmoja.
Alisema urefu wa kivuko hicho ni mita 27.8 na upana ni mita 8.75 ambapo kimetengenezwa kwa vifaa maalum kwa ajili ya matumizi ya majini.
Alisema kivuko hicho kinaendana na ubora wa kimataifa ambapo ukaguzi wake umefanywa na Mamlaka wa usafiri wa majini na nchi kavu (SUMATRA) ambayo imewahakikishia kuwa kiko salama kwa usalama wa abira.
Hali kadhalika kivuko hicho kina vifaa vya kisasa vya kutosha kujiokolea kwa rika
zote.

Rais Kikwete amsafisha Waziri Magufuli katika sakata la kujipendelea kujenga barabara nzuri jimboni kwake kabla ya Biharamulo



Na Theonestina Juma, Biharamulo
SERIKALI imewataka makampuni Wakandarasi wa hapa nchini kuiga mfano wa wakandarasi wa barabara ya Kampuni ya CHICCO kwa kufanya kazi nzuri na kujisimamia na kujindesha wenyewe licha ya serikali kutokamilisha malipo yao kwa wakati.
Rais Jakaya Kikwete amesema hayo  jana katika hafla fupi
ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Kagoma Lusahunga wenye
urefu wa kilomita 154 iliofanyika wilayani Biharamulo
Alisema Kampuni hiyo imejenga barabara ya Lusahunga hadi Kagoma kwa muda mfupi ambapo hadi sasa bado wanaidai serikali sh.bilion 40 ambayo watalipwa muda si mrefu.
Alisema lengo la serikali kukazania ujenzi wa barabara ni mkakati mpango wa kufungua nchi ili iweze kupitika kwa mikoa yote ya hapa nchini kuunganishwa kwa lami  licha hadi 2015 hatakamilisha labda kwa Rais ajaye.
Alisema licha ya barabara hiyo kuiwekea jiwe la msingi lakini
ukweli ni kuwa ujenzi wa barabara hiyo imeshakamilika ambapo imebakia mita 500 tu kukamilika.
Kuhusu manung'uniko kuwa Waziri wa Ujenzi, John Mafugufuli kuwa anajipendelea kwa kujengea bara bara ya lami ya Chato Buzirayombo si kweli bali ilikuwa ni mpango wa serikali.
”Si kweli kuwa Dkt.Magufuli alijipendelea kujengwa barabara hiyo kabla ya Kagoma Lusahunga bali ulikuwa ni mpango wa serikali”alisema.
Hata hivyo, Rais Kikwete amewataka wananchi kulinda na kutunza bara bara zinazojengwa ili ziweze kudumu kwani serikali inatumia pesa nyingi katika barabara.
"Kitu kikubwa ni kutunza barabara wapo maadui yake kama mvua
na matendo ya wanadamu kuzidisha uzito kwenye magari yao, kuchimba mchanga kando kando ya barabara, kumwaga oil,na ndiyo sababu kila barabara wameweka mzani"alisema.
Naye Waziri wa Ujenzi John Magufuli akizungumza katika hafla hiyo alisema hajawahi kumpongeza mkandarasi yeyote yote lakini kulingana na utendaji kazi wa wanapaswa kupewa pongezi.
Kwa upande waMtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini,
Bw.Aaron Mfugale alisema ujenzi wa barabara hiyo upembuzi yakinifu
ulianza mwaka 1995 ambapo 2003 alipatikana mkandarasi na kutimuliwa kazi kutokana na uwezo mdogo na baadaye ilipatikana Kampuni ya Chicco waliojenga barabara hiyo kwa miezi 36 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.
Alisema jumla ya fedha zinazotumika katika mradi huo unaofadhiliwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 ni sh.bilioni 191.

Ziara ya Rais Kikwete ya siku sita mkoani Kagera

 Rais Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani BiharamuloRais Jakaya Kikwete akikata utepe kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya Kagoma-Lusahunga katika wilayani Biharamulo. 
Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo Jumamosi Julai 27, 2013Rais Kikwete akipiga picha ya kumbukumbu na wananchi wa Ngara baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo  Rais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani NgaraRais Kikwete akishiriki kupiga ngoma na kikundi cha utamaduni cha Ngara wakati wa uzinduzi wa kivuko cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo wilayani Ngara Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (1)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya KyerwaRais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa (2)Rais Kikwete akisimikwa kuwa chifu wa Wahaya na kukakabidhiwa mgolole na silaha za jadi za Wahaya katika sherehe ya kuzindua wilaya mpya ya Kyerwa.Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete aliposimama kwa muda kuwasslimia wilayani Karagwe akielekea Rusumo kuzindua kivuko cha Ruvuvu Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (1)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu jana Jumamosi Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua  kivuko cha MV Ruvuvu  Jumamosi Julai 27, 2013 (2)Wananchi wakimshangilia Rais Kikwete baada ya kuzindua kivuko cha MV Ruvuvu  Kivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto RusumoKivuko cha zamani kilichokuwa kikitumiwa na wananchi wa Ngara kuvuka mto Rusumo Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Jumamosi Julai 27, 2013Kivuko kipya cha MV Ruvuvu katika mto Rusumo kilichozinduliwa na Rais Kikwete Rais Kikwete akihutubia umati NgaraRais Kikwete akiongea na wananchi katika sherehe ya kuzindua mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Nyaishozi, Wilaya ya Karagwe Rais Jakaya Kikwete yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi ya siku nane.Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (2)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (3)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya KyerwaUmati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa (4)Umati uliojitokeza katika sherehe za uzinduzi wa wilaya mpya ya Kyerwa .(PICHA NA IKULU).

Nimechoka, JWT kufanya operesheni kuwasaka wahamiaji haramu na majambazi



Na Theonestina Juma, Biharamulo
 AMIRI Jeshi Mkuu,Rais Jakaya Kikwete amewatangazia kihama Majambazi, wanaomiki silaha kinyume cha sheria na wahamiaji haramu kujisalimisha na kusalimisha silaha zao ndani ya wiki mbili, baada ya hapo watakumbwa na msako mkali ambao haujawahi kutokea nchi hii.
Rais Kikwete ametoa agizo hilo jana katika hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi katika barabara ya Kagoma Lusahunga yenye urefu wa kilomita 154 iliofanyika wilayani Biharamulo.
"Nimechoka, Watanzania hawawezi kuwa watumwa ndani ya nchi yao, wakitaka kusafiri hadi magari yao yasindikizwe na askari wenye
silaha... maisha haya mpaka lini, ninataka Watanzaia waishi kwa raha zao na sitaki ugomvi na chi jirani"alisema.
Alisema Majambazi, wahamiaji haramu na wanaomiliki silaha kinyume cha sheria anawapatia wiki mbili kujisalimisha baada ya hapo watasakwa kila sehemu za mikoa ya Kagera, Geita na Kigoma hadi ndani ya nyumba zao wanakojificha kwa kutumia majeshi yote ya usalama.
"Upuuzi huo hatuuwezi kukubali, watu hao tutawasaka ndani ya nyumba zao,kwenye handaki wanakochimbia sialaha zao, kama ni wahamiaji haramu kutoka nchi jirani waondoke,warudi makwao, katika hili stanii...majeshi yote ya usalama, likiwemo Jeshi la wananchi na usalama wa taifa"alisema.
Nasema haya kwa macho makavu na mchana kweupe, na ole wao kwa wale watakao jaribu kuwafyatulia askari wetu risasi jeshi limkamate mateka nadhani nikisema hivyo kwa lugha ya kijeshi mnaelewa" alisisiza Rais Kikwete huku akishangiliwa na wananchi waliofurika kumsiliza.
Aidha Rais Kikwete ametoa tahadhari kwa Watanzania wanaojua wanaowahifadhi na kushirikiana na majambazi na wahamiaji haramu kuacha mara moja na watafute shughuli ya kufanya.
Alisema katika msako huo utakaoshirikisha JWT hakuna cha msalia mtume kwani tayari tumeshawapatia muda wa kuondoka hapa nchini.
Alisema kwa mhamiaji haramu anayetaka kuishi nchini heri afuate utaratibu wa kuingia na kusihi nchini lakini si vinginevyo.
Alisema tayari ameshatoa taarifa kwa vyombo vyote vya usalama kazi kwao kuanza utekelezaji baada ya wiki mbili kupita.

Kikwete:Nchi iko tayari wakati wote, muda wowote



Na Theonestina Juma,Kagera
AMIRI Jeshi Mkuu Jakaya Kikwete  amesema Tanzania haiko
tayari kuchezewa na nchi yoyote ile na kuwa nchi iko tayari kwa saa yoyote, muda wowote kutonana na kulinda usalama wa nchi inagharama
yake.
Rais Kikwete amesema hayo wakati akizungumza na mamia ya wakazi
wa Muleba waliohuria katika maadhimisho ya kumbu kumbu ya mashujaa619 yaliofanyika katika makaburi ya Kaboya wilayani hapa.
"Msiwe na wasi wasi nchi iko imara kijeshi, kiusalama, tutahakikisha tuna kuwa machomuda wowote,saa yoyote, tunawajibu wa kulinda nchi yetu, hatutamruhusu mtu yeyote kuchezea nchi yetu,tuatamfanya kama tulivyofanya kwa Idd Amin"alisema.
Na kuongoza" Wakazi wa Kagera mnajua vizuri yaliotokea ya mwaka 1979,mnajua maisha yalivyoku, hivyo wasiwe na shaka kwani
serikali haitathubutu kumruhusu mtu kuchezea ardhi yake wala kumega
nusu sentimita ya nchi hii".
 Alisema Tanzania haina nchi nyingine pa kukimbilia hivyo watailinda na kutetea na hatairuhusu mtu yeyote aichezee, wala kuimega kwa sababu yoyote ile, kwa mantiki hiyo hawatasita kumshughulikia atakayekuwa na nia kama hiyo.
Alisema chanzo cha yote hayo ni kutokana na Amin kudai kuwa eneo lote la Mtukula hadi mto Kagera ni sehemu ya Uganda hadi eneo hilo alitangaza kuwa niwilaya  mpya ya Rakai  ambapo alitakiwa kuondoka na kukaidi na hivyo hakukuwa jawabu lingine isipokuwa kumwondoa kwa nguvu,kazi ilifanyika na kukomboa mipaka yetu.
"Lakini wakati wao wakivamia waliharibu rasilimali zetu,amri ya Amiri Jeshi wa wakati huo naye alisema kuwa na wao licha ya kukomboa mipaka na hivyo wao walilazimika kusonga zaidi ili nao wapate uchungu wagharama ya kujenga kama sisi, na hii ndiyo maana ya Mbarara”.
Alisema kuna watu waliolipa gharama kwa kutoa maisha yao kwa ajili ya kukomboa Watanzania ambao ndiyo hao mashujaa 619 waliolala katika makaburi ya Kaboya.
Alisema kutokana na hali hiyo serikali itaendelea kuwahudumia
mashujaa waliotoa uhai yao kwa ajili ya kukomboa wananchi ili kuondoa malalamiko yaliopo ya kichini chini kuwa serikali imewasahau mashujaa hao kwani wapo ambao walipata ulemavu wa maisha.
Alisema kinachotakiwa ni Maofisa wa Jeshi kuieleza serikali ifanye nini kwa ajili ya mashujaa hao waliokuhani maisha yao,kwani walijitolea mhanga kukomboa nchi yetu.
Kamwe serikali haiwezi kuwasahau mashujaa wetu,kazi kwao
wanajeshi, kitu ambacho hakijafanyika niambieni, tuifanye,ili
ijulikane kuwa watu hawa walijitolea kwa ajili yetu,kwani wapo wale
ambao wako hai na baadhi ya viungo vyao havifanyi kazi hao tutaendelea kuwahudumia"alisema.
Alisema kulinda nchi ni kazi ngumu , kutetea taifa ni kazi ngumu,na kuna wakati unalazimika kufanya hivyo,kwa maisha yako
kama walivyofanya hao mashujaa waliolala hapo.
Awali Rais Kikwete alipomtaka Mkuu wa Majeshi Davis Mwamnyange kuwaeleza wananchi juu ya usalama wa nchi,alisema kuwa jeshi liko imara muda wote na wala wananchi wasiwe na wasi wasi kwani wako macho.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini,Charles Mwijage alimweleza Rais Kikwete kuwa wananchi wa maeneo hayo hawana mahusiano mazuri ya mipaka hivyo wananchi hao wanatakiwa kuelezwa mipaka.
"Wananchi hawana mahusiano mazuri kambi la Kaboya hivyo wanatakiwa wawekewe mipaka ili ijulikane kwani wewe ndiye msuluhishi wa mambo yote"alisema.
Hata hivyo Rais Kikwete alimwagiza Waziri wa Ardhi, Profesa Anna Tibaijuka kukaa na uongozi wa kambi ya Kaboya na viongozi wa wananchi ili wajadili tatizo hilo na kupatiwa ufumbuzi.



Katika maadhimisho hayo yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali kutoka ndani na nje ya nchi, viongozi wa dini, serikali,vyama vya siasa, mawaziri, Rais wa Zanzibar, Dkt.Mohamed Shein na Makamu wa Rais, Dkt.Ghalib Bilal.mwisho