MAUZO ya Dhahabu nje ya nchi yemeshuka kwa kiasi cha asilimia 14.8 wakati
mauzo ya almasi yakipaa maradufu kwa kipindi cha mwaka wa fedha
uliopita wa 2012/2013.
Kushuka kwa mauzo hayo ya wachimbaji wakubwa na wadogo, kulisababishwa
zaidi na kufungwa kwa migodi ya Tulawaka, Resolute, kushuka kwa kasi ya
uzarishaji na uuzaji wa nje na kushuka kwa bei ya dhahabu katika soko la
dunia.
Meneja wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Tawi la Mwanza, Mussa Mziya,
alisema katika kipindi hicho mauzo ya dhahabu kanda ya Ziwa kwa nje ya
nchi yalipungua kwa kiasi hicho kufikia dola za Marekani milioni 1,901.2
(karibu sh. 2.5) milioni kutoka dola 2,232.3 (zaidi ya sh. bilioni
tatu) kwa mwaka 2011/2012.
Kiasi cha dhahabu kwa wachimbaji wakubwa, kilipungua kutoka kilo
39,544.8 mwaka 2011/2012 hadi kufikia kilo 37,796.3 kwa mwaka wa fedha
uliopita wa 2012/2013 huku madini hayo yakianguka kwa asilimia 10.9
kutokana na kuimarika kwa dola.
Alisema katika kipindi cha mwaka wa fedha ulioisha Juni 2013, thamani ya
madini toka kwa wachimbaji wadogo pia iliporomoka kwa asilimia 55.8
kufikia dola milioni 5.5 (zaidi y ash. Bilioni saba) milioni kutoka dola
milioni 9.4 (zaidi ya sh. bilioni 1.7) zilizopatikana mwaka 2011/2012.
“Thamani ya dhahabu pekee kutoka wa wachimbaji wadogo kwa kipindi tajwa
ilishuka hadi dola milioni 3.9 kutoka dola milioni 8.3 milioni mwaka
2011/2012 kutokana na kuanguka kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia
wakati thamni ya almasi kutoka kwa wachimbaji hao wadogo ikipaa,”
alifafanua.
Alisema almasi ya wachimbaji hao ilipanda hadi dola milioni 1.8 kutoka
dola milioni 1.2 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wake.
Mauzo ya almasi nje ya nchi yaliongezeka mara dufu kufikia dola milioni
44.8 milioni katika mwaka 2012/2013 kutoka dola milioni 11.5 mwaka
2011/2012.
Kuongezeka kwa mauzo ya almasi kulichangiwa na uhuishaji mkubwa katika
mgodi wa almasi wa Williamson Diamond, ulioko Mwadui mkoani Shinyanga.
Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Sunday, January 26, 2014
Serikali yakatakiwa kufuta nauli za vivuko maeneo ya vijijini
Na
Theonestina Juma, Kagera
WAKALA wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Mkoa wa
Kagera wametakiwa kufuta gharama za
vivuko kwa watembeao kwa mguu kutokana na hiyo ni huduma kwa jamii na
sio biashara.
Ushauri huo
umetolewa jana na Mbunge wa Viti Maalum
(CCM), Bi. Elizabeth Batenga wakati akizungumza katika kikao cha bodi ya
barabara kilichofanyika mjini hapa.
Alisema”wanachi
wanaovuka vivuko vilivyoko katika mkoa wa Kagera wanatakiwa kufutiwa tozo,
kutokana na wanaovuka vivuko hivyo ni wale wasio kuwa na uwezo, wakati mnapanga
kuongeza gharama mimi ninaona mfute, kwani hiyo ni huduma kwa wananchi”
Hivi wale wanaotembea barabarani, wanatozwa na
nani si wanatembea bia kutozwa chochote si ni huduma inayotolewa kwa wananchi sasa
ni kwa nini wanaovuka vivuko wao watozwe fedha kwa ajili ya nini, hapa si
kuwaonea ?alihoji
Bi. Batenga
alisema wakati TEMESA wakiangalia kutaka kuongeza viwango vya nauli ya vivuko
vyake, wafikirie kutafuta ni kwa namna gani wanavyoweza kuondoa tozo hizo kwa
wananchi hasa ikizingatiwa kuwa vivuko hivyo viko maeneo ya vijijini ambako
kuna wananchi wengi.
“Huko
vijijini mwananchi kupata hata sh. 200 kwake ni shida, lakini cha kushangaza
mwananchi anayevuka kwenda ng’ambo ya pili kwenda kulima anatozwa, hela kwa
ajili ya kuvuka… si dhani kama ni haki… serikali itafute namna ya kuwafanya
hawa wananchi”alisema
Alisema
katika maeneo hayo ya vijijini, wananchi wanaoishi katika upande wa pili
wanalazimika kulipia nauli kuvuka kwenda upande mwingine kwenda msibani hali
inayowafanya kufikia hatua ya kushindwa kutembeleana kwa kukosa nauli.
Hata hivyo
kwa upande wa Mkuu wa mkoa Kagera, Kanali Fabian Massawe akizungumzia suala
hilo alisema TEMESA wanatakiwa kuangalia ni watu wa aina gani wa kuwatoza, kwa
wale wasiokuwa na uwezo waachwe wavuke bure.
Aidha
wanapaswa kuangalia kama ni vyombo vya moto to ndiyo vitozwe hela na wavuka kwa
miguu waruhusiwe kuvuka bila malipo.
Kwa upande
wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba, Kapteni Dauda Kateme
akizunguzia vivuko hivyo, alisema yeye anashindwa kuwaelewa TEMESA kwani wamekuwa
wakitoza ushuru magari ya halmashauri hiyo, wakati kivuko cha Kyanyabasa kiko katika halmashauri yake.
Alisema
TEMESA ikiwa ni kama chombo kinachofanya biashara wao wakitakiwa kulipa ushuru
wanakataa kwa madai kuwa wao wanatoa huduma na si biashara.
Awali Kaimu
Meneja wa TEMESA mkoa Kagera, Bw. Wilson Nyitwa, alisema kuwa TEMESA inampango
wa kupandisha nauli za vivuko vyake ambavyo ni Kyanyabasa na mto Ruvuvu
kutokana na kupanda kwa gharama za maisha.
Alisema wao biashara
bali ni huduma, ambapo kwa siku katika kivuko cha Kyanyabasa hupata kiasi cha
sh. 40,000 ilihali kivuko cha Kyanyabasa
hupata sh.70,000 kwa siku.
Alisema kwa
kiasi wanachotoza kwa sasa hakisaidii kitu chochote, wakati hata mishahara
imepanda kwa watumishi hivyo inafikia hatua wanashindwa kujiendesha hasa
ikizingatiwa kuwa wao hawapati ruzuku kutoka serikalini.
Hata hivyo,
kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Bi. Zipora Pangani alisema kulingana na uzoefu wake
katika kivuko cha mto Pangani, wananchi kuruhusiwa kuvuka bure kitawafilisi kabisa
TEMESA kwani kiasi hicho kidogo
wanachopata ndicho kinawasaidia katika kujiendesha.
Alishauri mpango huo wa kutaka wananchi wavuke
bure isubiriwe hadi uchaguzi Mkuu 2015 upite bila hiyo itasu
Kagasheki- Mtu asiyeraia ni kitanzi akipewa madaraka makubwa ya uongozi
Na
Theonestina Juma, Bukoba
ALIYEKUWA
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki amesema kwa sasa ameanza
kuongopa kwa mtu ambaye si raia wa nchi akaomba uraia akapewa na madaraka
makubwa ni kitanzi.
Balozi Kagasheki ambaye ni Mbunge wa jimbo la
Bukoba mjini alisema hayo mwishoni mwa wiki hii wakati akiwahutubia mamia ya
wakazi wa mjini Bukoba.
Alisema
katika nchi ya Marekani imo ndani ya sheria ukiomba uraia wa Marekani Katiba
yao iko sawa sawa yako maeneo wanakuambia umepewa uraia wala si wa kuzaliwa
pale yapo maeneo huwezi ukagusa wala hata usiombe.
“Hapa naweza
kusema kuna mtu … huwezi kwenda katika nchi za watu wakakupa uraia … tena uraia
wakupewa..wa kuomba .. .matokeo yake wewe unaanza sasa kuwahujumu, kuwaibia,
kuwakejeli,kuwakiburi na kujaa jeuri
haiwezekani kama umepewa uraia unapaswa kufanya kazi na wale raia wa
kuzaliwa wa nchi hiyo nenda kwa
utaratibu wa nchi hiyo”alisema
Alisema yote
yanafanyika kwa nia nzuri lakini mtu akipewa uraiwa anapaswa kufanya kazi vyema
na waliozaliwa pale na si kufanya unavyotaka.
“Nenda
kamulize hata leo kuhusu uraia wake umekaaje …. atakuwambia kuwa Waziri wa
mambo ya ndani alitia mkono wake pale ndiyo maana nikapewa, umeshapewa sasa
fanya vizuri …yote haya nayasema kwa nia nzuri sio kwa ubaya”alisema
Na kuhoji
kuwa … “Wazungu wanasema, After role …if we can not speak for her…. yaani baada ya yote hayo kama hawataisemea bchi yao
ni nani atakaye isemea? Hayupo!
Alisema
kutokana na hali hiyo, kwa sasa katika harakati zao za kuanza kujenga mji wa
Bukoba kwa wale ambao wana nia ya kuvuruga wawapishe wakae pembeni .
“Mnajua kuna
watu wengine wako humu mjini wana maneno sikuweza kuwataja majina yao … kwa
sababu hata nikiwataja nitakuwa nimejiteremsha kwao… ndiyo sababu sitaki
kuwataja “alisema.
Alisema kwa
sasa wataanza kuaza kukaa vikao mbali mbali kwa nguvu zote ili kujenga kwa
pamoja mji wao kwani Bukoba itajengwa na wana Bukoba wenyewe na kwamba katika
vita iliokuwemo ndani ya Manipaa hiyo, aliyeishinda ni WanaBukoba na wala si
Mbunge na baadhi ya Madiwani.
Alisema
upotevu wa sh. bilioni 2.5 zilizopotea ambazo zingewezesha kuleta mabadiliko
makubwa ndani ya Manipaa hiyo hakuna anayeiona zaidi ya kuona ‘kamunobele’.
Alisema
pamoja na kuwepo kundi la watu wanaosema
kuwa wapo watu wanaosema kuwa Kagasheki
ni mwiba anayewachuma yeye yuko na atakuna nao katika uchaguzi Mkuu unaoratajia
kufanyika mwakani.
“Mimi hapa
bado nilikuwa najifikiria, itakuwaje mwakani… kuna watu nasikia kuwa
wanamwandaa mtu I mwingine aje awe Mbunge wa Jimbo hili, kwa kuwa wapo watu
wanaojifanya wanajua siasa nawambieni fanyeni mtakavyofanya mtanikuta
uwanjani”alisema”
Alisema
waliosema kuwa Madiwani wa CCM wameungana na upizani kumwondoa meya hayo ni
maneno ya kahawa, kwani walikuwa wakitetea haki ya wana Bukoba na hatua
iliofikia ya kuwafukuza madiwani wanane,
hakuna chama chochote kinachoweza kufanya hivyo, kwani kuwafukuza wajue kuwa
CCM kwa heri.
“Hata ngazi
ya CCM haifanyi hivyo, kuna vitu vya
kuangalia… kwa watu wenye akili hawawezi kufanya kama nyie mlivyoamua”alisema
Matamshi
hayo ya Mbunge Kagasheki yanakuja siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi wa
mahesabu ya serikali (CAG ), Bw. Ludovick Utouh kutoa taarifa ya uchunguzi
maalum uliokuwa ukifanywa ndani ya Manispaa hiyo kufuatia ombi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutokana na mvutano uliodumu
kwa miaka miwili kati ya Mstahiki, Meya Dkt. Anatory Amani, Mbunge na baadhi ya
Madiwani kupinga uendeshaji wa Manispaa hiyo katika utekelezaji wa miradi.
Katika
ripoti ya CAG ulibaini kuwepo kwa ufisadi mkubwa uliofanywa katika Manispaa
hiyo wakati wa utekelezaji wa miradi mbali mbali kama viwanja 5,000 ujenzi wa
soko la kisasa, kituo cha kitega uchumi, kituo cha mabasi, kituo cha kuoshea
magari.
Pia si mara
ya kwanza Mbunge Kagasheki kusema kuwa ndiye alimpa urai Dkt. Amani ambaye inadaiwa
kuwa ni raia wa nchini Uganda ambapo pia amekuwa akieleza kuwa yeye ndiye
aliyemchonga hadi akafikia hatua ya kuwa Meya wa Manispaa hiyo, hali iliomfanya
kukorofishana na aliyewahi kuwa Meya wa Manispaa hiyo, Bw. Samuel Luangisa,
ambapo Balozi Kagasheki amekuwa akikiri wazi kumkosea Bw. Luangisa.
mwisho
Friday, January 10, 2014
Uuuuwiiiiii tembo wetu wanaisha Maliasili yatoa matokeo ya sensa yao
Wizara
kwa kushirikiana na wataalamu wa ndani na nje ya nchi imefanya sensa
katika Maeneo ya Mfumo ikolojia wa Selous – Mikumi na Ruaha – Rungwa
pekee kwa kuwa ni maeneo yenye tembo wengi nchini.
Matokeo
ya sensa hii yanaonyesha kwamba Mfumo wa ikolojia wa Selous-Mikumi kwa
sasa una tembo wapatao 13,084 na Ruaha–Rungwa una tembo wapatao 20,090.
Takwimu hizi zinaonesha kupungua kwa idadi ya tembo na hasa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi ikilinganishwa na Sensa za awali.
Takwimu
za muda mrefu zinaonesha kwamba mwaka 1976 katika mfumo ikolojia wa
Selous–Mikumi kulikuwa na tembo 109,419. Idadi hii ilipungua kufikia
22,208 mwaka 1991 kutokana na wimbi la ujangili uliokuwepo katika
kipindi cha mwaka 1984 -1989. Hata hivyo, idadi hiyo iliongezeka na
kufikia 70,406 mwaka 2006 baada ya Operesheni Uhai iliyofanyika mwaka
1989 na 1990 na juhudi za kimataifa za uhifadhi ikiwemo kusitisha
biashara ya meno ya tembo.
Aidha,
idadi ya tembo nchini ilipungua hadi kufikia jumla ya tembo 38,975
mwaka 2009 na kuendelea kupungua hadi kufikia tembo 13,084 hivi sasa.
Hali
kama hiyo inaonekana pia katika mfumo wa ikolojia wa Ruaha-Rungwa
ambapo sensa ya mwaka 1990 ilionesha kuwa na tembo 11,712 kutokana na
wimbi la
ujangili. Idadi hii iliongezeka na kufikia 35,461 mwaka 2006. Hata
hivyo, idadi hiyo imepungua na kubakia tembo 20,090 hivi sasa.
Kwa
matokeo haya inaonesha kuwa katika mfumo ikolojia wa Selous-Mikumi
idadi ya tembo imepungua kwa asilimia 66 ikilinganishwa na idadi ya
mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo 38,975. na katika Mfumo
ikolojia wa Ruaha–Rungwa Tembo wamepungua kwa asilimia 36.5
ikilinganishwa na idadi ya mwaka 2009 ambapo kulikuwa na jumla ya tembo wapatao 31,625.
Kupungua
huku kunathibitishwa na idadi ya mizoga ya tembo iliyohesabiwa wakati
wa zoezi la sensa. Jumla ya mizoga 6,516 na 3,496 ilihesabiwa katika
mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa. Katika zoezi hili
Wizara ilitumia vigezo vya uwiano wa mizoga na tembo hai waliohesabiwa
(carcass ratio) kubaini vyanzo vya vifo hivyo. Katika hali ya kawaida,
uwiano wa asilimia 7 – 8 unaashiria vifo vya asili kama vile ugonjwa na
uzee. Zaidi ya asilimia hiyo inaashiria vifo visivyo vya asili.
Sensa
iliyofanyika mwaka huu imeonesha uwiano wa asilimia 30 kwa mfumo
ikolojia wa Selous-Mikumi na asilimia 14.6 kwa Ruaha–Rungwa. Kwa mujibu
wa matokeo hayo, idadi kubwa ya vifo vya tembo vimetokana na vifo
visivyo vya asili.
Uchambuzi
wa kina umebainisha kuwa asilimia 95 na 85 ya mizoga iliyoonekana
katika mifumo ikolojia ya Selous-Mikumi na Ruaha–Rungwa ni ya zaidi ya
miezi 18 iliyopita.
Hii
inaonesha kuwa juhudi za makusudi zilizofanywa na serikali ikiwa ni
pamoja na kuimarisha doria na operesheni maalum mbalimbali za hivi
karibuni zimesaidia kupunguza wimbi la ujangili kwa kiasi kikubwa.
Aidha,
kukamatwa kwa meno ya tembo yenye uzito wa kilogramu 32,987 ndani na
nje ya nchi katika kipindi cha 2008 hadi Septemba 2013 ni ishara tosha
kuwa ujangili ni mojawapo ya sababu kubwa za kupungua kwa idadi ya tembo
nchini.
Sababu
nyingine ni kuongezeka kwa mifugo katika maeneo yaliyohifadhiwa na
shoroba za wanyamapori. Mathalan, katika Pori Tengefu la Kilombero
ambalo ni sehemu ya ikolojia ya Selous – Mikumi, mwaka 2002 lilikuwa na
tembo 2,080, katika sensa ya mwaka huu, hukukuwa na tembo hata mmoja.
Ongezeko
la bei katika masoko ya biashara haramu ya meno ya tembo hususan katika
nchi za Mashariki ya mbali ni kichocheo na kisababishi kikubwa.
Kufuatia
hali hii, Wizara inaimarisha ulinzi wa wanyamapori kwa kushirikiana na
vyombo vya ulinzi na usalama na taasisi nyingine za kanda na kimataifa
pamoja na kuelimisha na kushirikisha wananchi katika masuala mbalimbali
ya uhifadhi.
Ili
kuimarisha na kuboresha shughuli za uhifadhi, Wizara iko katika hatua
za mwisho za kuanzisha mamlaka mpya ya wanyamapori. Vilevile sheria za
uhifadhi zinapitiwa ili kuruhusu kuanzishwa kwa mfumo wa kijeshi kwa
watumishi wa sekta ya wanyamapori.
Wizara
inapenda kuwatambua na kuwashukuru wafadhili wote waliofanikisha sensa
hii iliyogharimu kiasi cha dola za kimarekani 160,000ikiwa ni fedha za
serikali na wafadhili. Wafadhili hao ni Shirika la Misaada ya Kiufundi
la Ujerumani (GIZ) kupitia Frankfurt Zoological Society (FZS) na Shirika
la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kupitia Mradi wa TANAPA wa
SPANEST.
Imetolewa na
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii
Mhe. Lazaro Nyalandu (MB)
10/01/2014
Rais Jakaya Kikwete akutana na Mabalozi na Wawakilishi wa Taasisi za Kimataifa Ikulu
Wednesday, January 1, 2014
Rais Kikwete amwapisha IGP mpya, ni Afande Mangu
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha Inspekta Generali wa Polisi (IGP)
mpya Afande Ernest Mangu katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam
jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpatia nyenzo za kazi baada ya kumuapisha
Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Abdulrahman Kaniki
katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali na
Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja na Inspekta
Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu wake Naibu
IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es
salaam jioni hii
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali
Mawaziri na Katibu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue katika picha ya pamoja
na Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande Ernest Mangu na naibu
wake Naibu IGP Afande Abdulrahman Kanini katika viwanja vya Ikulu jijini
Dar es salaam jioni hii
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande
Ernest Mangu, Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande
Abdulrahman Kaniki pamoja na IGP mstaafu Afande Saidi Mwema katika
viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni hii
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na IGP mpya Afande
Ernest Mangu, Naibu Inspekta Generali wa Polisi (IGP) mpya Afande
Abdulrahman Kaniki katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam jioni
hii. PICHA NA IKULU
IDARA YA HABARI MAELEZO
Rais
Dk. Jakaya Kikwete amemwapisha Mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini
Inspekta Generali wa Polisi Ernest Jumbe Mangu na Naibu wake
Kamishna Abdulrahan Omar Juma Kaniki katika viwanja vya Ikulu, Dar es
Salaam jana jioni.
Katika
hafla fupi hiyo iliyoshuhudiwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Ghalib
Bilal, mawaziri kadhaa, viongozi wa Serikali na baadhi ya makamanda wa
jeshi la polisi kiongozi huyo baada ya kiapo cha kulitumikia jeshi hilo
na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, amewaambia waadishi wa
habari kuwa kazi yake kubwa itakuwa ni kupambana na uhalifu na
kufuatailia migogoro miongoni mw a jamii na makundi mbalimbali, pia
ameahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuboresha mifumo
ndani ya jeshi lake.
Kwa
upande wa naibu wake, Bw. Kaniki amesema mbali na majukumu yake ya
kumsaidia Mkuu wake wa kazi ataongeza juhudi za ufuatiliaji katika ngazi
ya tarafa na vijiji ili kujenga uwezo wa ulinzi shirikishi na
kusisistiza kuwa jamii ina fursa kubwa katika kufanikisha suala la
ulinzi katika maeneo wanayoishi.
Naye
aliyekuwa Inspekta Jenerali wa Polisi , Said Mwema ameishukuru jamii kwa
ujumla kwa ushirikiano mkubwa ambao amekuwa akiupata, kadhalika
kumtakia mwenzake aliyempokea kazi ya mafanikio na amesihi jamii
iendelee kumpa ushirikiano.
Kuhusu
maendeleo ya jeshi hilo Bw. Mwema amesema pamekuwepo na kasi ya
uimarishaji wa vitendea kazi katika kipindi kifupi, uimarishaji wa
miundombinu ndani ya jeshi hilo na amesema kuna kazi mbili za utafiti wa
kisayansi kuhusu mwenendo wa utendaji zilizo katika hatua ya mwisho
kukamilishwa zitakazobaini ufanisi na changamoto za jeshi la polisi na
kutoa mapendekezo ya kuboresha upande wa jeshi la polisi kadhalika
kubaini kiwango cha mahusiano ya jeshi hilo na umma.
Salaam za Rais Kikwete mwaka mpya 2014
SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2013
UtanguliziNdugu zangu;
Watanzania Wenzangu;
Niruhusuni nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa rehema, kwa kutujalia uzima mpaka kufika na kuiona siku hii ya leo ya kuuaga mwaka 2013 na kuukaribisha mwaka 2014. Wapo ndugu, jamaa na marafiki zetu wengi ambao hawakupata bahati tuliyoipata sisi kwa vile wametangulia mbele ya haki. Tuendelee kumwomba Mola wetu awape mapumziko mema na azilaze roho zao mahali pema peponi. Ameen.
Hali ya Usalama
Ndugu Wananchi;
Tunaumaliza mwaka 2013 nchi yetu ikiwa salama na tulivu. Mipaka iko salama na ile hali ya wasiwasi tuliyokuwa nayo kwa nyakati fulani mwaka huu sasa haipo tena. Uhusiano wetu na majirani ni mzuri na tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa hali inaendelea kuwa hivyo au hata kuwa bora zaidi mwaka 2014 na daima dumu.
Hali ya usalama wa ndani ya nchi nayo ni nzuri. Hali ya wasiwasi tuliyokuwa nayo mwaka wa jana na mwanzoni mwa mwaka huu kuhusu uhusiano baina ya Wakristo na Waislamu haipo. Ni matumaini yangu kuwa haitajirudia tena. Pepo mbaya amepita tuombe atokomee kabisa.
Ndugu zangu;
Watanzania wenzangu;
Napenda kurudia kuwasihi kuwa tuchague kuendelea kuishi pamoja kwa upendo, umoja, kuvumiliana na kushirikiana. Tuepuke kugeuza tofauti zetu za kisiasa, kidini, rangi, kabila au maeneo tutokayo kuwa chanzo cha uadui na mifarakano. Kwa sasa tuna mwelekeo mzuri nawaomba tuudumishe. “Mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi ni mwananchi”. Tuchague kuijenga nchi yetu badala ya kuibomoa. Tusiwasikilize watu hasidi wanaochochea uadui na mifarakano miongoni mwetu. Watatuvurugia nchi yetu nzuri.
Uhalifu
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2013 vyombo vya dola vikishirikiana na wananchi viliendelea kupambana na vitendo vya uhalifu. Mafanikio ya kutia moyo yameendelea kupatikana ingawaje bado kuna kazi kubwa ya kuendelea kufanya mwaka 2014 na miaka ijayo.
Dawa za Kulevya
Ndugu Wananchi;
Kati ya Januari na Desemba 2013, kilo 1,261 za heroin, kilo 3 za cocaine na kilo 89,293 za bangi zimekamatwa na watuhumiwa 1,631wametiwa mbaroni. Tatizo la biashara na matumizi ya dawa za kulevya ni kubwa na mapambano yanazidi kuwa makali. Mafanikio yanaendelea kupatikana ingawaje bado tuna kazi kubwa na ngumu ya kufanya mbele yetu. Ni makusudio yetu kuongeza maradufu nguvu ya kupambana dhidi ya uhalifu huu.
Tupo hatua nzuri katika matayarisho ya kuanzisha Kikosi Maalum cha Kupambana na Dawa za Kulevya katika mwaka wa fedha 2014/15. Pia tutaitazama upya sheria ya adhabu kwa makosa ya kufanya biashara ya dawa za kulevya ili kuifanya iwe na meno makali zaidi. Vilevile, tutaongeza uwekezaji katika vituo vya tiba na kuwarekebisha watu wanaotumia dawa za kulevya. Mafanikio yanayopatikana Muhimbili na Mwananyamala yanatupa moyo wa kufanya zaidi.
Ujambazi
Ndugu wananchi;
Jeshi la Polisi limeendelea kupambana na ujambazi wa kutumia silaha na mafanikio yameendelea kupatikana. Matukio ya ujambazi yemepungua mwaka 2013 ukilinganisha na mwaka 2012. Takwimu zifuatazo zinathibitisha ukweli huo. Mwaka 2012 matukio ya ujambazi yaliyoripotiwa yalikuwa 6,872 na kwa mwaka 2013 yameripotiwa matukio 6,409. Mwezi Julai mwaka huu, niliamua kulihusisha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania katika kupambana na ujambazi wa kutumia silaha na utekaji wa magari katika Mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma. Katika Mikoa hiyo tatizo la ujambazi lilikuwa limefikia kiasi cha kulazimisha watu kusindikizwa na Polisi kutoka Ngara kwenda Karagwe, Biharamulo kwenda Muleba na kutoka Nyakanazi hadi Kakonko. Hali hii haikubaliki na hatuwezi kuiacha iendelee.
Ndugu Wananchi;
Uamuzi wangu huo ndiyo ulioanzisha Operesheni Kimbunga ambayo imekuwa na mafanikio ya kutia moyo. Hali ya usalama katika Mikoa hiyo inaelekea kuimarika ingawaje ni mapema mno kusema tatizo limedhibitiwa. Silaha nyepesi na nzito zipatazo 650 zikiwemo za kijeshi na za kiraia pamoja na mabomu ya kutupwa kwa mkono 11 zilikamatwa kwenye operesheni hiyo. Aidha, watu 31,203waliokuwa wanaishi nchini kinyume cha sheria walirudi makwao. Kati yao, watu 21,758 walirudi kwa hiari na 9,445 walirudishwa wakati wa Operesheni.
Subscribe to:
Posts (Atom)






