Pata habari moto moto kila siku, kwa Mawasiliano zaidi piga Simu Na. 0755 856991/ 0712 992434 Email:-theonestinajuma@yahoo.com/rorya.09@gmail.com
Friday, November 30, 2012
Watu waliozimia wakati wa mazishi ya Sharo Milionea
Monday, November 26, 2012
Manispaa nipeni mkataba wa ujenzi wa soko nisome nielewe-Kagasheki
Na Theonestina Juma,
Bukoba
MBUNGE wa Jimbo la Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki ameutaka uongozi wa Manispaa ya Bukoba kutoa na kuweka wazi mkataba wa ujenzi wa soko kuu la Bukoba unaotarajia kugharimu jumla ya sh. bilioni 12 badala ya kuwa ya siri
Balozi Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema hayo jana katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mayunga mjini hapa.
“Mimi sijauona hata mkataba wa ujenzi wa soko kuu, nimeomba niuone , ili nijiridhishe sijapewa.... nawambieni hadi leo hii sijauona huo mkataba, hata sijui ni vitu gani vilivyomo katika mtakaba huo, kwa nini Watendaji wa Manispaa wabadilishe mktaba wa ujenzi huo kuwa wa siri”alisema.
Kutokana na hali hiyo, Balozi Kagasheki alisema soko hilo halitavunjwa januari 15, mwakani kama ambayo uongozi wa Manispaa ulivyopanga.
Alisema si kwamba anapinga maendeleo, lakini anachokipigania ni kutaka kujua mkataba uko vipi, isije ikafikia hatua serikali inakaanza kushtumia na vyama vya upinzani kuwa walisaini mktaba mbovu.
“Kumbukeni nchi yetu inazidi kuwa masknini kutokana na mikataba mibovu inayowekwa na baadhi ya watendaji wetu, kwa Jimbo la Bukoba sitaruhusu jambo kama hilo, mpaka nijirisheni na mkataba uliopo nijue fedha zitakazotumika katika ujenzi huo nani atawajibika kuzilipa”alisema
Na kuongeza”nipeni mkataba nisome nielewe, fedha hizo bilioni 12 zitatoka wapi, nani atazilipa, haziewezi kutoka hivi hivi wakati Manispaa iko hoi katika suala la maendeleo”
Alisema pamoja na kwamba yeye ndiye aliahidi kuleta mabadiliko ya mandhari ya Bukoba lakini si kwa mfumo wa mkataba kutowekwa wazi.
Alisema cha kushangaza katika mradi huo ni kutofanywa kwa utafiti wa Geological Technical survey kama eneo hilo kuna maji kiasi gani isije ikafikia hatua ya kuanza ujenzi wake wake na ukabainika kuwa kuna maji mengi na fedha zingine zaidi zitahitajika.
Nilipohoji juzi ndani ya Baraza la madiwani kama kuna utafiti wa ‘Geotec’ ulifanywa hapo kabla nilijibiwa kuwa bado wanatarajia kufanya jamani na hili nisihoji kama Mbunge”alisema
Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo aliushauri uongozi wa Manispaa ya Bukoba ili kurejesha imani kwa wananchi,waelekeze nguvu zake katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi katika kata ya Nyanga, badala ya kuburuza wananchi.
Aidha alisema kutokana na kwa sasa kuna kesi mahakamani ya kupinga kuhamishwa kwa wafanyabiashara ndani ya soko hilo wavute subira wakisubiri maamuzi ya mahakama ambayo yanatarajiwa kutolewa mwezi Machi mwakani.
Alisema wao viongozi pamoja na watendaji wa Manispaa ya Bukoba wanatakiwa kufanya kazi kama timu moja kwani hakuna kitakachowashinda na wasitishane kwa vitu vidogo.
Alisema lengo lao wote kwa pamoja ni kulinda maslahi ya mtu wa kawaida aliyewapa nafasi ya uongozi na wasiende kibabe.
Mwisho.

Bomu lazua tafrani Ngara
Na Theonestina Juma, Bukoba
WANANCHI wanaoishi karibu na uwanja wa ndege katika kijiji cha Ruganzo kata ya Kibimba wilayani Ngara wamegubikwa na hofu kubwa baada ya kitu kizito mithili ya bomu inayotoa hewa ya gesi ambayomtu akivuta anapiga chafya kudondoka chini kwa kishindo kutoka juu na kusababisha milipuko mingi kutokea.
Tukio hilo la aina yake na ya mara ya kwanza kutokea wilayani humo ambalo linapakana na nchi zaidi ya nne za Afrika Mashariki lilitokea Novemba 22 mwaka huu saa 8 usiku wakati wananchi wakiwa wamelala.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkuu wa wilaya ya Ngara, Costantine Kanyasu alisema kitu hicho mfano wa chuma lenye umbo kama la yai linalotoa hewa ya gesi lilipodondoka chini kwa nguvu na kusababisha mtikisiko mkubwa wilayani humo jambo lililochangia wananchi kujawa na hofu kubwa.
Alisema pamoja na kutokea milipuko zaidi ya mara tatu wilayani humo haijajulikana kama yamesababishwa na kudondoka kwa chuma hicho ambacho hadi sasa hakijathibitishwa kama ni bomu.
Alisemakutokana na kuwepo sintofahamu kwa wananchi wanaoishi karibu na eneo hilo la uwanja wa ndege, kamati ya ulinzi na usalama umewashauri wananchi kukaa mbali na chuma hicho, kutokana na kutoa gesi ambayo mtu akivuta harufu yake hupiga chafya hivyo wanahofia huenda iwaka ni sumu.
“Hiki chuma, kinatoa moshi kama harufu ya gesi, ambayo mtu akivuta tu anapiga chafya, harufu hiyo ni mbaya, tunahofia huenda ikawa ni sumu hivyo tunawashauri wananchi kutokisogelea”alisema Bw. Kanyau.
Hata hivyo, Mkuu huyo amewataka wananchi wa wilayani humo kutokuwa na wasi wasi kutokana na tayari wataalamu wa kutegua mabomu kutoka Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ tayari wameshafika katikaeneo la tukio kuchunguza tukio hilo.
Akizungumzia juu ya kuwepo kwa taarifa zilizogaa mkoani hapa kuwa chuma hicho kimekuwa kikiongezeka ukubwa kadri muda unavyokwenda hadi kufikia mfano wa kichuguu, alisema si kweli kwani awali wananchi walikuwa wakiliiona kwa mbali lakini, walipofika JWTZ na kukichukua na kuiweka sehemu peupe, hakiongezeki bali kiko hivyo hivyo.
Alisema kitu hicho kwa ndani kuna vyuma na kwa nje kuna mipira na ina nyuzi nyuzi.
Aidha kuhusiana na tuhuma kuwa bomu hilo limetokana na mapigano yanayoendelea nchini Kongo, wapiganaji hao ndiyo wamerusha kombora na kutua wilayani humo, alisema si kweli kwani hadi sasa hawajajua limetokea wapi.
“Si kweli, hadi sasa hakuna anayejua hicho chuma kilichosababisha mtikisiko mkubwa kiasi hicho, hatuwezi kusema kuwa labda limetoka Rwanda ama Burundi…. Bado uchunguzi unaendelea”alisema.
Kwa upande wa Kamanda wa polisi Mkoani Kagera , Phillip Kalangi akizungumza na gazeti hili alikiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo halijaleta madhara yoyote kwa wananchi lakini hadi sasa wataalam wa mabomu wa mkoani hapa hawajalitumbua ni kitu gani.
“Unajua mabomu yanajulika, kuna zaidi ya aina ya mabomu 300 na tunayajua, ukifika tu unatambua kuwa hii ni aina fulani ya bomu lakini hili, halijulikani, kwani lipo kama mfono wa tufe”alisema Kamanda Kalangi.
Alisema hadi sasa kuna mawasiliano yanafanyika kati ya JWT ya mkoani hapa na Makao makuu kwani kitu hicho kinahitaji uchunguzi wa hali ya juu”alisema.
Oktoba 31 mwaka huu watoto watano wa kata ya Ihanda wilayani Karagwe waliuawa kwa kulipukiwa na bomu la kutupwa kwa mkono wakati walipoliokota kama vyuma chakavu.

Tuesday, November 20, 2012
Mwanamke amuua mwanae kwa kumtwanga kichwani na kisha kumzika chap chap
BUKOBA
JESHI la polisi Mkoani Kagera linamshikilia Bi. Johnmary Anthony kwa tuhuma ya kumuua
mwanae wa miezi mitatu kwa kumtwanga na kitu kizito kichwani na kufariki papo hapo na kisha kumfukia chap chap kwenye shimo la kutupia takataka akiwa amemfunga kwenye mifuko ya
plastic maarufu kama kiroba
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na
kuthibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Phillip Kalangi tukio hilo la
aina yake na la kusikitisha limetokea
Novemba 16 mwaka huu katika kijiji cha Kyaitoke Bukoba vijijijini.
Kifo cha mtoto
huyo kiligunduliwa na uongozi wa kijiji hicho, baada ya mtoto huyo kupita
takribani siku nzima haonekani kama mama yake amembeba wala kumnyonyesha kama
ilivyozoeleka jambo lililolazimu uongozi wa kijiji hicho kutoa taarifa katika
kituo cha polisi.
Mwanamke huyo inadaiwa kuwa alihojiwa na uongozi wa
kijiji hicho aliko mtoto ambapo alikuwa akiwadanganya kuwa mtoto amepotea jambo
lililowatia hofu na kuamua kutoa taarifa kituo cha polisi .
Kutokana na hali hiyo, mwanamke huyo akihojiwa na
polisi alidai kuwa hajui mtoto alipo, hali lililolazimu jeshi hilo kuzidi
kumhoji kwa makini ambapo alisema kuwa mtoto huyo amemuua kwa kumpiga na kitu
kizito kichwani.
Kamanda Kalangi alisema pamoja na kuendelea
kuhojiwa kwa mwanamke huyo, hajakubali kumtaja hata jina la mtoto huyo, wala
hata sababu iliompelekea kumuua mwane kwa kumtwanga kichwani na kitu kizito.
Kamanda huyo alisema mwanamke huyo bado anaendelea
kuhojiwa, ambapo anatajiwa kupimwa akili kwanza ili kuangalia kama ni mgonjwa
wa akili kabla ya kupandishwa kizimbani.
mwisho
Saturday, November 17, 2012
Wananchi muda wa kufungwa viongozi wetu pingu na kuletwa mbele yetu ni enzi za wakoloni
Na Theonestina Juma, MISSENYI
KITENDO cha Jeshi la polisi Wilayani Missenyi, kumfunga
pingu Mwenyekiti wa Kitongoji cha Mutukula, Bw.Hamidu Mugarula na kuanza
kumzungusha mtaa mzima kwa ajili ya
kumtaka awaoneshe wananchi aliowauzia maeneo kwa ajili ya kufanyiabiashara kimezua
mapambano makubwa kati ya polisi na wananchi hadi kusababisha polisi kupiga
risasi kadhaa hewani na mabomu la machozi
Tukio hilo la aina yake lililoonekana kama sinema na
kuwalazimu baadhi a wanachi kukimbia upande wa Uganda kujiokoa kilitokea hivi
karibuni (Novemba 6) mwaka huu saa 8 mchana katika eneo la Mutukula mpakani mwa
Tanzania na Uganda.
Mapambano hayo yaliodumu kwa saa 5 ililazimu polisi wengine kuitwa kutoka mjini Bukoba, kwenda kuongeza
nguvu ambapo muda huo wote shughuli za biashara na usafirishaji katika eneo
hilo la mpakani zilisimama.
Wakizungumza na gazeti
hili, baadhi ya wananchi na
wafanyabishara walioshuhudia tukio hilo walisema chanzo cha mapambano hayo kati
ya polisi na wananchi ni baada ya wananchi kuchukizwa na kitendo cha kiongozi
wao akiwa amefungwa pingu huku akiwa ametangulizwa mbele na polisi akizungushwa
mtaa mzima wakimtaka awaoneshe watu aliowakatia risiti za kuuziwa maeneo kwa
ajili ya kufanyia biashara.
Walisema kutokana na hali hiyo, kuliibuka mzozo mkubwa kati ya
polisi na wananchi hao, ambao waliwasihi polisi kumfungua pingu kiongozi wao
kama wanataka waongee nao.
Alisema wananchi hao walidai kuwa kiongozi wao hawezi
kuletwa mbele yao akiwa amefungwa pingu kama mwizi wakati alikuwa akifanya kazi
za serikali.
Kutokana na hali hiyo, huku jeshi la polisi, wakiwa
hawaelewani na wananchi hao, kwa hasira walianza kufanya vurugu ikiwa ni pamoja
na kuwarushia mawe polisi waliokuwa na mwenyekiti huyo, ambapo polisi walipoona
hali ni mbaya walilazimika kumbeba mwenyekiti huyo kama ng’ombe na kumtumbukiza
ndani ya gari waliokuwa nao na kumkimbiza katika kituo cha polisi cha Kyaka.
Hata hivyo, kitendo hicho kinaelezwa kuwa kilionesha kuzidi
kuwakasirisha wananchi hao, na kuamua kukimbia kwenda kufunga kizuizi na kuanza
kupanga matairi kwa lengo la kutaka kuharibu gari la polisi ili kumtoa kiongozi
wao.
Polisi waliwawahi kupita eneo hilo, ambapo baada ya kuona
polisi hao wameondoka na kiongozi huyo, walihamishia hasira zao kwenye mali za serikali .
Wananchi hao walivamia
ofisi ya kijiji cha Mutukula na kung’oa mlango na madirisha na kuchoma moto bendera ya Chama cha
mapinduzi (CCM) kilichokuwa kikipepea maeneo hayo na kisha kuhamia katika jengo
lililokuwa likitumia na halmashauri ya missenyi kwa ajili ya kukatia ushuru na
kuliteketeza kwa moto pamoja na nyaraka zote zilizokuwemo.
Mwenekiti wa Katibu wa soko na wafanyabiashara katika eneo
hilo la Mutukula, Bw. Theophil Kaembe akizungumza na gazeti hili alisema katika eneo la Mutukula, kuna eneo
lililotengwa na serikali kwa ajili wa ujenzi wa kituo cha mabasi ambapo eneo
hilo kutokana na kukaa wazi muda mrefu, huku wananchi wakihangaikia kutafuta sehemu pa kufanyia biashara,mwenyekiti
huyo kwa kushirikiana na Mtendaji wa Kata, Bw.Mukasa Mugarula waliamua
kuwagawawia wananchi hao.
Alisema maeneo hayo waligawa kwa kulipia sh. 10,000 ambapo
walielezwa kuwa maeneo hayo wamegawawiwa kwa muda kutokana na eneo hilo ni la serikali na linaweza kuhitajiwa kwa matumizi aliolengwa kwa muda
wowote.
Bw. Kaembe alisema “hata risiti tulizokatiwa zimeandikwa kuwa
ni kwa muda si za kudumu, risiti walizozitumia ni ya halmashauri namba HW5”.
Mapambano hao ambayo ililazimika polisi kutolewaa mjini
Bukoba kwenda kuongeza nguvu kutuliza ghasia hizo, ilivutia hisia za viongozi,
wa mkoani hapa, ilimlazimu hadi Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Phillip Kalangi
na Mkuu wa wilaya hio, Issa Njiku kufika eneo hilo.
Hata hivyo, Kamanda Kalangi akizungumzia vurugu hizo,
alisema kuwa imetokana na malalamiko yaliotolewa na baadhi ya wananchi kuwa
wanatakiwa warudishe maeneo hayo wakati waliuziwa kati ya sh. 200,000 hadi
350,000.
Alisema pamoja na vurugu hizo kutokea na kusababiasha shughuli
nyingi za kibiashara kusimama kwa muda lakini tayari walishafanya mazungumzo na
wananchi wa maeneo hayo na nchi jirani na kusawazisha na hivyo hali imerudi ya
kawaida.
Alisema viongozi hao wanaoshikiliwa na jeshi hilo
wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote, kwa tuhuma a kutumia ofisi ya
na wameuziwa maeneo na viongozi wa serikali kutumia vibaya ofisi ya serikali.
mwisho
Thursday, November 15, 2012
Majambazi wateka Muleba, wampora mfanyabiashara milioni 60 na kumuua mulinzi
Na Theonestina Juma, Muleba
MAJAMBAZI wenye silaha wamemuua, mlinzi wa kituo cha mafuta cha JR Petrol Bw.Felix Tonswe (55) ameuawa na majambazi waliofika kituoni hapo kumfuatilia mfanyabiashara mmoja wa duka wa Nshamba kwa lengo la kumpora fedha milioni 60 alizokuwa nazo.
Tukio hilo lilitokea Novemba 12, mwaka huu majira ya mchana wakati mfanyabiashara kutoka Nshamba aliyejulikana ka jina la Cleophace Rweyemamu (32) aliyekuwa safarini kuelekea Jijini Mwanza kulangua bidhaa.
Habari hizo zinasema kuwa, watu sita waliodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha, walianza kumfuatilia mfanyabiashara huyo kutoka Nashamba wakiwa na pikipiki tatu walizokuwa wamepakiana wawili wawili kama abiria.
Majamjazi hayo walikuwa akifuatilia nyendo za mfanyabiashara huyo bila kujua, ambapo alipofika katika kituo cha mafuta kwa jili ya kuwekewa mafuta kwenye gari lake, majambazi hayo sita waliingia kituoni hapo na kukizingira ambapo walimwamuru mfanyabiashara huyo kulala chini kifudi fudi.
Kutokana na mfanyabiashara huyo kutii agizo la majambazi hayo, walimpora sanduku lake lililokuwa na jumla ya sh. milioni 60 na kumwacha bila kumdhuru.
Hata hivyo katika harakati hizo, mlinzi wa kituo hicho alianza kujihami nao kwa kutumia silaha yake aliokuwa nayo lakini majambazi hayo walimuwahi na kumpiga risasi sehemu za matakoni ambapo alianguka chini na kupoteza fahamu.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoani Kagera, Phillip Kalangi , alisema watu watatu wanashikiliwa na jeshi hilo kuhusika na tukio hilo ambapo msako bado unaendelea wa kuwatafuta watu wengine waliohusika katika uporaji na mauji hayo.
Katika tukio hilo Kamanda Kalangi alisema inasadikika kuwa aina ya bunduki iliotumiwa na jambazi hayo ni kati ya SMG au ASR kutokana na risasi zilizotumika.
Hata hivyo, kamanda huyo ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara mkoani hapa kuacha kutembea na kiasi kikubwa cha fedha wakati ambapo mfumo wa utunzaji wa fedha umeboreshwa hapa nchini.

Wavuvi saba wafa maji Ziwa Victoria
Na Theonestina Juma, Bukoba
WAVUVI saba katika Ziwa Victoria wakati wakitoka kuvua samaki katika eneo la hifadhi serikali la Rubundo katika kisiwa cha Ikuza wlayani Muleba Mkoani Kagera.

wamefariki dunia katika matukio
mawili tofauti wilayani Muleba Mkoani Kagera likiwemo la wavuvi saba kufa maji
katika ziwa Victoria wakati wakitoka kuvua samaki na mtu mmoja kuuawa na
majambazi.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana kutoka wilayani Muleba tukio la kwanza la wavuvi kufa maji lilitokea Novemba 10, mwaka huu saa 9 usiku katika eneo la hifadhi ya Rubondo na Kambi ya wavuvi ya Kaziramtemwa katika kisiwa cha Ikuza wilayani humo.
Wavuvi hao walikufa maji wanadaiwa kuwa walikuwa ni wavuvi haramu, ambao walienda kuvua samaki katika hifadhi ya akiba ya Rubondo ambalo limetengwa rasmi na serikali kwa ajili ya mazalia ya samaki.
Imeelezwa kuwa chanzo cha wavuvi hao kufa maji ndani ya ziwa Victoria, ni kutokana na mtumbwi waliokuwa nao ulielemewa na mzigo mkubwa wa samaki waliokuwa wamevua katika eneo hilo la hifadhi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika wa habari hizi, wavuvi hao wakati wakienda kuvua samaki katika eneo hilo hawakuwenda na mtumbwi wa mashine bali la makasia, ambapo wakati wakirejea mtumbwi huo ulielemewa na mzigo na hivyo maji yalikuwa yalikuwa ndani ya mtumbwi huo ambao ulisababisha kupinduka na kuzama.
Katika mtumbwi huo uliokuwa na jumla ya watu tisa wavuvi saba walifariki na wengine wawili waliokoka baada ya kuogelea hadi nchi kavu.
Wavuvi waliokufa maji wametambuliwa kuwa ni pamoja na Baluya Masala (28), Obeid Yohana (33), Juma Kengele (35) wote wakazi Muganza wilayani Chato mkoani Geita.
Wengine ni pamoja na Alex Mwita (40) mkazi wa wilayani Tarime na Kipara Kasukari (40) mkazi wa wilayani Muleba.
Wengine waliotambuliwa kwa jina moja moja ni pamoja na Nicko (33) mkazi wa wilayani Sengerema Jijini Mwanza na Robert (32) mkazi wa Wilayani Biharamulo mkoani Kagera na kwamba kati ya watu hao wanne wamesafirishwa na wengine wamezikwa kisiwani humo.
Aidha walionusurika katika ajali hiyo wamejulikana kuwa ni pamoja na Robert Abdul (37) mkazi wa wilayani Tarime na Khamis Musa (28) mkazi wa Muganza wilayani Chato.

wavuvi wanne tayari wameshasarishwa na kuzikwa huku wengine watatu wakizikwa kisiwani humo.
Mwisho.
Mwisho.
Subscribe to:
Posts (Atom)