BUKOBA
JESHI la polisi Mkoani Kagera linamshikilia Bi. Johnmary Anthony kwa tuhuma ya kumuua
mwanae wa miezi mitatu kwa kumtwanga na kitu kizito kichwani na kufariki papo hapo na kisha kumfukia chap chap kwenye shimo la kutupia takataka akiwa amemfunga kwenye mifuko ya
plastic maarufu kama kiroba
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana mjini hapa na
kuthibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoani hapa, Phillip Kalangi tukio hilo la
aina yake na la kusikitisha limetokea
Novemba 16 mwaka huu katika kijiji cha Kyaitoke Bukoba vijijijini.
Kifo cha mtoto
huyo kiligunduliwa na uongozi wa kijiji hicho, baada ya mtoto huyo kupita
takribani siku nzima haonekani kama mama yake amembeba wala kumnyonyesha kama
ilivyozoeleka jambo lililolazimu uongozi wa kijiji hicho kutoa taarifa katika
kituo cha polisi.
Mwanamke huyo inadaiwa kuwa alihojiwa na uongozi wa
kijiji hicho aliko mtoto ambapo alikuwa akiwadanganya kuwa mtoto amepotea jambo
lililowatia hofu na kuamua kutoa taarifa kituo cha polisi .
Kutokana na hali hiyo, mwanamke huyo akihojiwa na
polisi alidai kuwa hajui mtoto alipo, hali lililolazimu jeshi hilo kuzidi
kumhoji kwa makini ambapo alisema kuwa mtoto huyo amemuua kwa kumpiga na kitu
kizito kichwani.
Kamanda Kalangi alisema pamoja na kuendelea
kuhojiwa kwa mwanamke huyo, hajakubali kumtaja hata jina la mtoto huyo, wala
hata sababu iliompelekea kumuua mwane kwa kumtwanga kichwani na kitu kizito.
Kamanda huyo alisema mwanamke huyo bado anaendelea
kuhojiwa, ambapo anatajiwa kupimwa akili kwanza ili kuangalia kama ni mgonjwa
wa akili kabla ya kupandishwa kizimbani.
mwisho
No comments:
Post a Comment