Na Theonestina Juma,
Bukoba
MBUNGE wa Jimbo la Bukoba mjini, Balozi Khamis Kagasheki ameutaka uongozi wa Manispaa ya Bukoba kutoa na kuweka wazi mkataba wa ujenzi wa soko kuu la Bukoba unaotarajia kugharimu jumla ya sh. bilioni 12 badala ya kuwa ya siri
Balozi Kagasheki ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, alisema hayo jana katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Mayunga mjini hapa.
“Mimi sijauona hata mkataba wa ujenzi wa soko kuu, nimeomba niuone , ili nijiridhishe sijapewa.... nawambieni hadi leo hii sijauona huo mkataba, hata sijui ni vitu gani vilivyomo katika mtakaba huo, kwa nini Watendaji wa Manispaa wabadilishe mktaba wa ujenzi huo kuwa wa siri”alisema.
Kutokana na hali hiyo, Balozi Kagasheki alisema soko hilo halitavunjwa januari 15, mwakani kama ambayo uongozi wa Manispaa ulivyopanga.
Alisema si kwamba anapinga maendeleo, lakini anachokipigania ni kutaka kujua mkataba uko vipi, isije ikafikia hatua serikali inakaanza kushtumia na vyama vya upinzani kuwa walisaini mktaba mbovu.
“Kumbukeni nchi yetu inazidi kuwa masknini kutokana na mikataba mibovu inayowekwa na baadhi ya watendaji wetu, kwa Jimbo la Bukoba sitaruhusu jambo kama hilo, mpaka nijirisheni na mkataba uliopo nijue fedha zitakazotumika katika ujenzi huo nani atawajibika kuzilipa”alisema
Na kuongeza”nipeni mkataba nisome nielewe, fedha hizo bilioni 12 zitatoka wapi, nani atazilipa, haziewezi kutoka hivi hivi wakati Manispaa iko hoi katika suala la maendeleo”
Alisema pamoja na kwamba yeye ndiye aliahidi kuleta mabadiliko ya mandhari ya Bukoba lakini si kwa mfumo wa mkataba kutowekwa wazi.
Alisema cha kushangaza katika mradi huo ni kutofanywa kwa utafiti wa Geological Technical survey kama eneo hilo kuna maji kiasi gani isije ikafikia hatua ya kuanza ujenzi wake wake na ukabainika kuwa kuna maji mengi na fedha zingine zaidi zitahitajika.
Nilipohoji juzi ndani ya Baraza la madiwani kama kuna utafiti wa ‘Geotec’ ulifanywa hapo kabla nilijibiwa kuwa bado wanatarajia kufanya jamani na hili nisihoji kama Mbunge”alisema
Kutokana na hali hiyo, Mbunge huyo aliushauri uongozi wa Manispaa ya Bukoba ili kurejesha imani kwa wananchi,waelekeze nguvu zake katika ujenzi wa kituo kipya cha mabasi katika kata ya Nyanga, badala ya kuburuza wananchi.
Aidha alisema kutokana na kwa sasa kuna kesi mahakamani ya kupinga kuhamishwa kwa wafanyabiashara ndani ya soko hilo wavute subira wakisubiri maamuzi ya mahakama ambayo yanatarajiwa kutolewa mwezi Machi mwakani.
Alisema wao viongozi pamoja na watendaji wa Manispaa ya Bukoba wanatakiwa kufanya kazi kama timu moja kwani hakuna kitakachowashinda na wasitishane kwa vitu vidogo.
Alisema lengo lao wote kwa pamoja ni kulinda maslahi ya mtu wa kawaida aliyewapa nafasi ya uongozi na wasiende kibabe.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment