Na Theonestina Juma, Muleba
MAJAMBAZI wenye silaha wamemuua, mlinzi wa kituo cha
mafuta cha JR Petrol Bw.Felix Tonswe (55) ameuawa na majambazi waliofika kituoni
hapo kumfuatilia mfanyabiashara mmoja wa duka wa Nshamba kwa lengo la kumpora
fedha milioni 60 alizokuwa nazo.
Tukio hilo lilitokea Novemba 12, mwaka
huu majira ya mchana wakati mfanyabiashara kutoka Nshamba aliyejulikana ka
jina la Cleophace Rweyemamu (32) aliyekuwa safarini kuelekea Jijini Mwanza
kulangua bidhaa.
Habari hizo zinasema kuwa, watu sita waliodhaniwa kuwa
ni majambazi wakiwa na silaha, walianza kumfuatilia mfanyabiashara huyo kutoka
Nashamba wakiwa na pikipiki tatu walizokuwa wamepakiana wawili wawili kama
abiria.
Majamjazi hayo walikuwa akifuatilia nyendo za mfanyabiashara huyo
bila kujua, ambapo alipofika katika kituo cha mafuta kwa jili ya kuwekewa mafuta
kwenye gari lake, majambazi hayo sita waliingia kituoni hapo na kukizingira
ambapo walimwamuru mfanyabiashara huyo kulala chini kifudi fudi.
Kutokana
na mfanyabiashara huyo kutii agizo la majambazi hayo, walimpora sanduku lake
lililokuwa na jumla ya sh. milioni 60 na kumwacha bila kumdhuru.
Hata
hivyo katika harakati hizo, mlinzi wa kituo hicho alianza kujihami nao kwa
kutumia silaha yake aliokuwa nayo lakini majambazi hayo walimuwahi na kumpiga
risasi sehemu za matakoni ambapo alianguka chini na kupoteza
fahamu.
Tukio hilo ambalo limethibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoani Kagera,
Phillip Kalangi , alisema watu watatu
wanashikiliwa na jeshi hilo kuhusika na tukio hilo ambapo msako bado unaendelea
wa kuwatafuta watu wengine waliohusika katika uporaji na mauji
hayo.
Katika tukio hilo Kamanda Kalangi alisema inasadikika kuwa aina ya
bunduki iliotumiwa na jambazi hayo ni kati ya SMG au ASR kutokana na risasi
zilizotumika.
Hata hivyo, kamanda huyo ametoa tahadhari kwa wafanyabiashara mkoani hapa kuacha kutembea na kiasi kikubwa cha fedha wakati ambapo mfumo wa utunzaji wa fedha umeboreshwa hapa nchini.
No comments:
Post a Comment