Monday, October 13, 2014

Haya ndiyo urithi wa Lady Jay Dee




Hili ni gari kwa ajili ya Bend yake inayojulikana kama Machozi Band






Hii ndo nyumba anayoishi mwanadada Lady Jay dee 




Hii ndo gari anayomiliki aina ni Super Murano 





Hu undo mgawa anaomiliki mwanadada lady Jay dee unaojulikana kama Nyumbani lounge 



Jide anajivunia kushinda Tuzo za Tanzania, Kilimanjaro Music (2004) kupitia kipengele cha Albamu Bora ya R&B (Binti), mwaka 2006 kupitia Tuzo za Pearl of Africa Music alizoshinda kama Mwanamuziki Bora wa Kike kutoka Tanzania

.Kama hiyo haitoshi, mwaka 2007, Jide alishinda Wimbo Bora wa kushirikiana (Hawajui) kupitia Tanzania Music Awards alioshirikiana na MwanaFA.

 Mwaka 2008, kupitia Tanzania Music Awards, Lady Jaydee alishinda Tuzo ya Mwanamuziki Bora wa Kike pamoja na za Pearl of Africa Music katika kipengele hichohicho, Kisima Music Awards (Wimbo Bora wa Mwaka) uitwao Anita alioshirikiana na Matonya.

Mwaka 2009, alishinda Tuzo za Tanzania Music (Wimbo Bora wa Mwaka), Anita kisha 2010 Tanzania Music Awards (Mwanamuziki Bora wa Kike), mwaka 2011 Mwanamuziki Bora wa Kike na Wimbo Bora wa Afrika (Nitafanya, aliomshirikisha Kidum kutoka Kenya na mwaka jana (Mwanamuziki Bora wa Kike).

Kwenye suala la kujitanua kibiashara ndiyo ilisababisha mwaka 2010 afikie makubaliano na Kampuni ya Mohamed Enterprises kuzalisha maji yenye nembo ya jina lake ingawa biashara hiyo haikudumu kwa muda mrefu. 

Hakukata tamaa, cheche zake kwenye ujasiriamali zilizaa matunda kwenye mgahawa wake wa Nyumbani Lounge uliopo Ada Estate, Kinondoni, jijini Dar ambao unamuingizia mkwanja hadi sasa.

Heshima kwake ilizidi kuongezeka, taratibu alifanikiwa kujijenga katika maisha yake binafsi kama ujenzi wa nyumba yake ya kifahari iliyopo Kimara, Dar.

 Mali kama magari ya kutembelea, magari ya kazi zake za muziki havimpigi chenga.

Katika kuonesha muziki na ujasiriamali kwake vimevuka mipaka, ilifika wakati walishauriana na mumewe aachane na kazi ya utangazaji kwa muda ili aweze kusimamia miradi yao ambayo ilihitaji kutanuka zaidi jambo ambalo limefanikiwa.

No comments:

Post a Comment