Na Theonestina
Juma,Bukoba
MFANYABIASHARA
maarufu mjini Bukoba Mkoani Kagera, Bw.Leonard Mtensa (50) amefariki dunia ghafla
wakati akifanya mapenzi na
mwanamke mmoja ndani ya gari
lake.
Kwa mujibu wa
taarifa zilizopatikana mjini hapa na kusambaa kila kona ya mji wa Bukoba nakuthibitishwa na Kamanda wa polisi Mkoa Kagera Henry Mwaibambe
,tukio hilo la aina yake limetokea Novemba 18,mwaka huu saa 4.00 usiku katika maeneo
ya Buyekera mjini Bukoba
Kamanda Mwaibambe,alisema mfanyabiashara huyo ni mmiliki wa klabu maarufu
ya usiku Bukoba iitwayo Linas night club.
Alisema
kabla ya kufikwa
na umauti mfanyabiashara huyo alikuwa akifanya mapenzi ndani ya gari lake
lenye namba za usajili T.982 CQG
aina ya IST.
Alimtaja
msichana aliyekuwa akifanya mapenzi na mfanyabiashara huyo kuwa ni Bi. Jackline
Hassan (25 ) mkazi wa Buyekera.
Alisema wakati wapenzi
hao wakiendelea na mapenzi
ghafla hali ya mfanyabiashara huyo ilibadilika na kukimbizwa
katika kituo cha Afya cha
ELCT Ndolage kilichopo
Bukoba lakini alifia njiani.
Alisema
baada ya gari lake kupekuliwa kulikutwa
na vilevi mbalimbali ikiwemo Whisky aina
ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa.
Alisema jeshi la polisi mkoani hapa linamshikilia,
Bi. Jackline kwa ajili ya kusaidia upelelezi na kuwa chanzo cha kifo hicho
hakijajulikana
No comments:
Post a Comment