Na Theonestina Juma, Ngara
MWENYEKITI wa kijiji cha Kumwendo kata Mbuba Wilayani Ngara, Bw.Paul Rutishobwa (45) amehukumiwa kifungo cha maishajela na Mahakama ya Wilaya ya Ngara baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mtoto mwenye umri wa miaka minane.
Hukumu hiyo imetolewa juzi na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ngara,Bi.Mariam Lusewa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani.
Awali mwendesha mashtaka wa jeshi la polisi wilayani Ngara, Tumaini Membi aliiambia mahakama hiyo kuwa, Mwenyekiti huyo alitenda kosa hilo, Septemba 18, 2012 saa 2 usiku kijijini hapo.
Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa huyo alimwita mtoto huyo akiwa nyumbani kwao kwa lengo la kumtuma, ndipo alipomkamata na kumziba mdomo na kumvutia kwenye shamba la mihogo na kuanza kumbaka.
Alisema mtuhumiwa huyo alimvuta mtoto huyo umbali wa mita kama 15 kutoka nyumbani kwao ulikuwa na shamba la mihogo na kuanza kubaka.
Alisema mama wa mtoto huyo, Bi.Pelagia Gwassa
kwa wakati huo alikuwa akipika jikoni na alipomaliza shughuli za
mapishi ndipo alianza kumtafuta mwanae aje ale bila mafanikio, ndipo alipiga makelele kuwaita majirani ili wamsaidie kumtafuta
mwanae.
Alisema baadhi ya wananchi walijikusanya kuanza kumtafuta, ambapo walipofika kwenye shamba hilo la mihogo walisikia sauti ya mtoto huyo akisika kama anagugumia kwa maumivu.
Alisema walipomkaribia walimkuta akiwa anachuruzika damu kutoka sehemu zake siri huku akiwa amefungwa mdomo kwa kitambaa.
Alisema alipoulizwa amekuaje, alimtaja Bw.Rutishobwa kumvua nguo na kumwingilia na kisha kumwacha hapo.
Mtoto huyo alipelekwa katika hospitali ya Mabawe na kubaini kuwa amebakwa na kufikishwa mahakamani ambapo kipindi hicho chote alikuwa nje kwa mdhamana.
Hata hivyo, kwa upande wa mtuhumiwa akijitetea alidai kuwa hakumbaka mtoto huyo bali anasingiziwa.
Bw.Rutishobwa aliwaacha hoi mahakama hiyo baada ya kuhukumiwa maisha kwa kutoa hirizi mbili katika mkono wake wa kulia na kushoto na kuzitupa chini akidai kuwa mganga alimdanganya kuwa hatafungwa.
Hata hivyo, habari zaidi zinaeleza kuwa Bw. Rutishobwa, aliwahi kuoa dada yake baba yake mtoto aliyebakwa, na kuzaa nae watoto wanne,na baadaye kutengana na hivyo mtoto aliyembaka alimzoea kwa sabbau ya undugu huo.
No comments:
Post a Comment