Friday, December 20, 2013

Waziri Kaghasheki atangaza kujiuzulu, mawaziri wengine watatu nao wafutwa kazi na Rais Kikwete


kagashekiWaziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamisi Kagasheki ametangaza nia ya kujiuzulu wadhifa wake dakika chache zilizopita bungeni  mjini Dodoma,sababu kubwa ya kujiuzulu ni baada ya kusomwa  ripoti ya kamati ya Bunge Kumtuhumu kuzembea na kukithiri kwa vitendo viovu vilivyofanywa na wanausalama wakati wa Operesheni Tokomeza.
Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imebainisha kuwa oparesheni Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa na Serikali ilikumbwa na unyanyasaji mkubwa wa wananchi, Ukatili, Udharirishaji, Ubakaji na Mauaji huku baadhi ya wazazi wakivuliwa nguo, kuteswa na kubakwa mbele ya wanafamilia.
Akiwasilisha bungeni taarifa ya kamati hiyo Mwenyekiti wake James Lembeli amesema pamoja na mateso hayo yaliyowakumba wananchi pia nyumba zao zilichomwa na mifugo kupigwa risasi huku mingine ikifa kwa kukosa maji, chakula na maziwa kwa ndama wadogo.
Kamati hiyo pia imebainisha kuwepo kwa vitendo vya Rushwa vilivyotawala oparesheni Tokomeza ambapo pia wananchi waliokuwa na mifugo walitozwa faini na mifugo mingine kuuzwa kwa bei nafuu ambayo haikulingana na faini iliyokuwa ikitoza na wafugaji walizuiwa kushiriki mnada wa uuzaji wa mifugo hiyo.
Mbali na Waziri Kaghasheki mawaziri wengine watatu walioonekana kuwa wagumu kutamka na vinywa vyao kuwa wanajiuzulu, wamefukuzwa kazi na Rais Jakaya Kikwete katika taarifa yake iliotolewa mbungeni humo leo na Waziri mkuu Mizengo Pinda baada ya kuwasiliana na naye akiwa nchini Marekani na kumwelezea Rais yote yanayojiri humo mjengoni.

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizfl9xTIA4YGERZa1hVrvMViAIO-CyQBxGTItNYudwN8nFpnZxwHfJ7n0abKNJWsUmRIFSIxMPdydixs0lVhe-yhifLDDzcRU6GJwfJza8uuKqAy3Vgrc9sbTOydu_S22GAo3uhWOIS3g/s1600/11_10_y7kr7s.jpg












 WWaziri wa Emmanuel Nchimbi aliyewajibishwa na Rais Kikwete
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgNp4eU6V6cPgh_0OiQzpvPpnhm4clZ226qs0Wq5OFxrTezYis2uy0KT04Yn6hWdm6zwRKYildGn18-Du467Pxz47S2nEvOeCtlnf1UhToYEsGadRtnFZuIhAxPTDaGXtjjtRkjWdu1aMM/s1600/26e22-HERM8393.JPG
Waziri wa Uvuvi na mifugo, Dkt. David Mathayo
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhOIzcgR7QpKv0kYsIIJiMImojfMm7-xPx2aL0DnQa1RUGibWv0MBdBjVeR_s46vzj4hggONK8xROOk1sQHTbYH2NJGpaGJdM_yzbxDtTWLpHs-6gtrcmNCZPwB5l1pBZGjW_J84YVSqVg/s1600/nahodhafinger1-e1334564790445.jpg
Waziri wa Shamsa Vuai Nahodha









No comments:

Post a Comment