Na Theonestina Juma, Kagera
KATIKA hali
isiyo ya kawaida wahamiaji haramu waliorejeshwa nchini mwao na serikali ya
Tanzania kwa operesheni kimbunga
wamerejea kwa uwingi wilayani Kyerwa na kuwatishia wananchi kwa kujiita M23 na
kuwapora mali zao kwa nguvu.
Hayo
yamesemwa jana na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa, Mhandisi Benedict Kitenga wakati akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa
Kagera kanali, Massawe aliyembelea wilayani hapo kukagua maendeleo pamoja na ujenzi wa mabara
ya shule za sekondari za kata.
Alisema
kutokana kurejea kwa kasi ya ya ajabu kwa wahamiaji haramu katika kijiji na kata
ya Kibingo na kuwatishia wananchi wa kijiji
hicho kwa kujiita M23 kunawatia hofu wananchi hao.
“Wahamiaji
hao walikuwa wametengeneza makambi na kujihami kwa mapanga na marungu pia
walikuwa wakipita katika kijiji hicho na kuwatishia wananchi na
kuwanyanganya chakula kwa nguvu pia
kuwatishia maisha yao”alisema.
Hata
hivyo, Mkuu huyo wa wilaya alisema baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya kupata taarifa hizo walikwenda katika eneo hilo na kufanya operesheni
kubwa na kuwakamata wahamiaji haramu zaidi ya 20 pamoja na baadhi ya Watanzaia ambao walikuwa
wakishirikiana na wahamiaji haramu hao kuwahifadhi.
Alisema
Wahamiaji haramu hao waliokamtwa walirejeshwa kwenye nchi zao bila kutaja uraia
wao na watanzania walihusika walichukuliwa hatua kali za kisheria.
Kutokana
na hali hiyo, alisema wananchi wanatakiwa kutoa taarifa mara wawaonapo hao
wahamiaji haramu wakirejea au katika maeneo yao
Hata
hivyo, kwa upande wa Mkuu wa mkoa Kagera, kanali Fab ian Massawe alisema katika
operesheni Kimbunga waliondolewa wahamiaji haramu 31,000 badala ya 52,000 kwa hiyo
operesheni hiyo inaendelea ili kuhakikisha waliobaki wanaondolewa na hakuna wa
kurudi nchini.
“Chini
ya Kaulimbiu ya Hakuna wa Kubaki na
Hakuna wa Kurudi, tutahakikisha kila mhamiaji haramu anaondoka na watanzania
watakogundulika kushirikiana nao watachukuliwa hatua kali za kisheria, pia
naagiza Kamatia za Ulinzia na Usalaama kundelea na operesheni hiyo mpaka
kuwamaliza wahamiaji haramu.” Alisistiza Mkuu wa Mkoa.
Mkuu
wa mkoa alisema ili kushughulikia tatizo hilo kikamilifu wananchi wanatakiwa
kutoa taarifa hasa kwa viongozi wa juu mfano kwake na mkuu wa wilaya ambapo
alitoa namba za simu zake kwa wananchi pamoja na mkuu wa wilaya ili kupambana
na tatizo hilo.
Hata
hivyo, baadhi ya wananchi waliohojiwa walisema tatizo la wahamiaji haramu
linasababishwa na baadhi ya watendaji wa serikali katika ngazi za chini ambao
wanachukua hongo na kuwarudisha katika mazingira ya wananchi.
Wananchi
hao walisema inavyoonekana, viongozi wa chini kuanzia ngazi ya vitongoji,
vijiji hadi kata wamepewa mamnlaka makubwa mno na pia wamekuwa wakikaa muda
mrefu bila kubadilishwa vituo vya kazi na hivyo kujenga mazoea na wahamiaji
haramu hao.
“Kinachoitakiwa
kifanyike ni serikali kuanzia ngazi ya wilaya kuanza tabia ya kuwatembelea
viongozi wa serikali za vitongoji hadi kata kwa kushtukiza ili kuweza
kutokomeza hii tabia iliojengeka mikongoni mwao na kuonekana kama miungu watu katika
maeneo yetu’alisema mwananchi mmoja.
Operesheni
kimbunga iliendeshwa hivi karibuni na serikali kwa kushirikisha vyombo mbali mbali vya usalama baada ya Rais Kikwete
kutoa wiki mbili kwa wahamiaji haramu kuondoka nchini.
No comments:
Post a Comment